Salaam..
Nimekaa nikajiuliza, hasa baada ya timu pendwa ya Simba Sc kuwa matokeo yasiyoridhisha kwa mechi za hivi karibuni baada, hii ni baada ya kuchapwa 0-3 na mwarabu, na jana usiku, kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam.
Tukiondoa sababu nyingine kama wachezaji kukosa nafasi za wazi, ambalo limeonekana kuwa tatizo kwa sasa pale Simba Sc, umri wa wachezaji na uchovu kwa kucheza mfululizo miaka mingi, lakini pia naona bado kuna tatizo jingine kubwa ambalo nalo hatujalitazama kwa umakini.
Nimekaa nikajiuliza, hivi ni ipi mantiki kwa Simba Sc, hasa viongozi wake, kuamua kuwa na makocha wawili, wote wenye sifa za kuifundisha timu, wenye umri mkubwa, kwa wakati mmoja?
Kama walishaamua kufuata maoni ya mashabiki kwamba Mgunda alikuwa hatoshi, wakaamua kumleta Mzungu, sasa ni sababu ipi inayowafanya waendelee kuwa na Mgunda pale kwenye benchi la ufundi?
Huu mkanganyiko unaojitokeza sasa matokeo yake ni kama vile Simba Sc imegawanyika makundi mawili, ina kocha wa viongozi, Mgunda, na kocha wa mashabiki waliotaka Mgunda aondoke kwa kura, mzungu.
Sijui ni kitu gani kinachowashinda viongozi wa Simba Sc kumwambia Mgunda asante kwa kazi yako, wamlipe chake, kisha aondoke, wamwambie ukweli sasa tumeamua kwenda na uelekeo tofauti, uwepo wake kwneye benchi naamini unawavuruga wachezaji kwa namna fulani.
Tumeona nyakati kadhaa Mgunda akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati mechi ikiendelea, huyu mtu anaweza kuwa anatoa malekezo tofauti na kocha mkuu anachotaka, matokeo yake ni kuwachanganya wachezaji, kwanini kocha mkuu asiachwe huru kufanya majukumu yake kwa nafasi?
Kwangu, viongozi wa Simba Sc ndio chanzo cha hili tatizo, kwani sijawahi kuona timu zinazojielewa hapa duniani zinakuwa na makocha wakuu wawili, hapa wanaajiri kocha mpya, na pale bado wanaendelea kubaki na yule wa mwanzo!, halafu tunajitapa tunakwenda kimataifa, mataifa yapi hayo?!
Viongozi wa Simba Sc pamoja na Mo wabadilike, waachane na mambo ya kimazoea na uswahili mwingi kwenye uendeshaji wa timu, tusipoamka mapema itakuwa too late.