Mtazamo Wangu: Tatizo la Simba SC kuwa na matokeo mabovu linaanzia hapa...

Atalaumiwa sana Mgunda. Atalaumiwa sana Robetino. Na hata uongozi kwa kujisafisha wanaweza timua mmojawapo au wote wawili. Wapenzi na mashabiki wa Simba tena wengine wana uelewa mkubwa tu nao sijui wamelogwa hawaoni tatizo sio makocha bali tatizo ni viongozi kufanya usajili wa hovyo kabisa.

Msimu mmoja kabla Kagere na Mugalu hawajaondolewa Simba uwezo wao wa kufunga pamoja na mwenzao Boko ulishaanza kushuka kwa kasi sana. Lakini mpaka leo takribani msimu wa pili sasa hakuna straika hata mmoja wa maana aliyesajiliwa mwenye uwezo wa kuwazidi Mugalu na Kagere sasa sijui waliwaondoa wa nini. Simba ndio timu inayoongoza kwa kutengeneza nafasi kwenye ligi ya NBC wanaweza hata kutengeneza nafasi hata 10 za wazi kabisa na hata mchezo wa juzi na Azam walifanya hivyo lakini inayotumika ni moja tu zikizidi sana mbili. Halafu leo watu wazima na akili zao wanasema eti Mgunda aondolewe wapuuzi kabisa. Anguko la Simba ni la lazima hata kipofu anaona huwezi kumtegemea Boko eti akupe ubingwa wa ligi na kukuvusha makundi kwa kweli ni kumuonea tu.

Wakuondolewa hapo Simba wa kwanza ni Mo wa pili ni Try Again watatu ni Mangungu. Badala ya kulipa millioni 400 kumsajili Manzoki wanamleta kwenye uchaguzi auze sura halafu wanachama wanashangilia wakifika uwanjani timu ikishindwa wanawatukana makocha hiyo ni akili kweli? Simba inashindwa mechi zake kwa sababu inakosa magoli ya wazi hata 10 kwenye mechi moja full stop. Na hao viongozi wakiendelea na ubahili huu huu wa usajili aisee kwenye Africa Super League inayoanza August kila timu itajipigia tu kama inavyotaka lakini wazinduke wasajili wachezaji wa maana.

Tatizo la pili kubwa Simba ni kiungo mkabaji mwenye uwezo wa kuilinda "back four" yake isipate madhara. Tangu kuondoka kwa Lwanga na Fraga viongozi hawajajikita kutafuta watu sahihi wa kuziba hiyo nafasi. Kila siku nasema Onyango na Inonga tutwalaumu bure lakini watateseka mpaka msimu muishe. Na mashabiki wa Simba wasitake aibu kubwa waombe tu Simba iishie makundi maana ikitokea bahati wakapita huko mbele watakutana na dhahama.
 
Nimekusoma hebu nikujibu kama ifuatavyo;

Kuhusu kuondolewa kwa Kagere na Mugalu, unadai tangu waondoke hapakuwahi kuletwa striker mwingine mwenye uwezo kama wao, hapa nakupinga.

Tumemuona Moses Phiri alivyokuwa na kasi nzuri kwenye ufungaji wa mabao mpaka akawa anamkaribia Mayelle kwa karibu kabisa, bahati mbaya majeruhi yakamkuta na kuathiri kiwango chake, mpaka hapo hii pointi yako ya kusema hakupatikana striker mwenye uwezo wa kina Kagere au kuwazidi naipinga.

Pia, unaonekana kutoshangazwa na uwepo wa makocha wakuu wawili ndani ya Simba Sc, kwako unaona hiyo ni hali ya kawaida, hii ni ajabu kabisa, hebu nikuulize; umewahi kuona timu gani inayojielewa hapa duniani ikaona kocha wake mkuu hafai, halafu badala ya kumuondoa, ikambakisha na kumuongezea kocha mwingine?

Hawa makocha wana falsafa tofauti, sawa, hata kama kocha msaidizi hana last say, lakini kwa nini akae pale ambapo falsafa yake haitumiki tena? au ameamua kubadili falsafa yake? kwangu kuwaacha hawa wawili pamoja ni sawa na kuchanganya mahindi na mchele, vurugu tupu, kwako kama hii vurugu unaiona jambo la kawaida, hongera zako!.

Ajabu zaidi, unasema Mo aondolewe bila kutuwekea mbadala wake, unataka Mo aondoke halafu aje nani kuchukua nafasi yake? huo muda ambao timu itakuwa bila mfadhili itakuwa inawezeshwa vipi? au unawaamini hawa wanachama na mashabiki ambao licha ya kuwepo miaka yote lakini timu ilikuwa inakosa mpaka chai asubuhi? hapo umeandika mihemko, umeridhika na kile anachotoa Mo sasa huoni tena umuhimu wake, umekuwa kama mlevi, ila akiondoka ndio akili itakukaa sawa..

Naungana nawe kwenye suala la "holding midfielder", hapo ni kweli, timu haijawa na kiungo mkabaji wa maana wa kuwalinda mabeki wa kati, kama ulivyosema, tangu waondoke kina Fraga, bado hatujapata mbadala wao wa maana.
 
Kwanza niseme tu naheshimu sana mawazo yako. Na nilchoandkia ni mtizamo wangu tunaweza tusikubaliane kwenye baadhi ya mambo lakini ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa:-

1. Phiri siyo repalcement ya Mugalu na Kagere. Phiri ni mshambuliaji wa pembeni na mshambuliaji nyuma ya mshambuliaji wa kati. Pia mara chache anaweza kutumika kama kiungo mshambuliaji na kiungo mkabaji (ila hii ya kiungo mkabaji ni wakati anaanza career yake zamani hizo). Kuchezeshwa kwake kama mshambuliaji wakati pale Simba kwanza ni kuficha aibu/madhaifu tu ya viongozi kwa kutosajili mtu sahihi wa hiyo nafasi na pili ni kuokoa jahazi tu.
2. Hata ukiwaondoa makocha wa sasa hao wapya utakaowalete utawatimua tu baada ya mechi chache kwa sababu timu haina mshambuliaji wa kati na kiungo mkabaji wa kukupa matokeo. Sasa kwa nini Mgunda apelekewe lawama na si Mo na viongozi ambao wao jukumu lao ni kuleta wachezaji wenye uwezo kwenye hizo nafasi mbili muhimu kwenye timu yoyote ile?
3. Mo aondoke maana yake sio aiche Simba afungashe virago ni kuwa auze hisa zake (zote au baadhi) kwa watu wenye uwezo wa kifedha zaidi yake kwani Simba ni kampuni na inaonekana uwezo wa Mo kuwekeza umeishia hapo ilipofika sasa Simba. Kama mwekezaji hawezi kununua mchezaji wa millioni 400 anasubiri amalize mkataba halafu anaota kuipeleka Simba nusu fainali kwenye CL maana yake kampuni imeweka malengo ya uongo kwani haina rasilimali ya kufikia malengo hayo hivyo basi inahitaji mtaji kutoka kwa wawekezaji wapya aidha kwa kuuza hisa zote au baadhi ya hisa.

Ni mtizamo tu.
 
Usajili ungekuwa mbovu sana kama mnavyosema, basi inawezekana leo timu ingekuwa nafasi ya nne au tano, lakini mbona bado tunaikomalia nafasi ya pili bila kushuka? ina maana hao wengine ni wabovu kupitiliza?
Mimi ukiniuliza kipimo cha Simba kwenye ligi kwa kiasi flani ntakwambia ni Azam na yanga hao wengine mipira ya maguvu na kukamia, kwa hiyo kushika nafasi pili sio kigezo cha kuwa timu bora, keshokutwa tunacheza na vipers ukiniuliza kama tutashinda naona ndoto na hapa ndio mtifuano utakapoongezeka ndani ya Simba
 
Kwanza niseme tu naheshimu sana mawazo yako. Na nilchoandkia ni mtizamo wangu tunaweza tusikubaliane kwenye baadhi ya mambo lakini ukweli utabaki kuwa ukweli kuwa:-

1. Phiri siyo repalcement ya Mugalu na Kagere. Phiri ni mshambuliaji wa pembeni na mshambuliaji nyuma ya mshambuliaji wa kati. Pia mara chache anaweza kutumika kama kiungo mshambuliaji na kiungo mkabaji (ila hii ya kiungo mkabaji ni wakati anaanza career yake zamani hizo). Kuchezeshwa kwake kama mshambuliaji wakati pale Simba kwanza ni kuficha aibu/madhaifu tu ya viongozi kwa kutosajili mtu sahihi wa hiyo nafasi na pili ni kuokoa jahazi tu.
2. Hata ukiwaondoa makocha wa sasa hao wapya utakaowalete utawatimua tu baada ya mechi chache kwa sababu timu haina mshambuliaji wa kati na kiungo mkabaji wa kukupa matokeo. Sasa kwa nini Mgunda apelekewe lawama na si Mo na viongozi ambao wao jukumu lao ni kuleta wachezaji wenye uwezo kwenye hizo nafasi mbili muhimu kwenye timu yoyote ile?
3. Mo aondoke maana yake sio aiche Simba afungashe virago ni kuwa auze hisa zake (zote au baadhi) kwa watu wenye uwezo wa kifedha zaidi yake kwani Simba ni kampuni na inaonekana uwezo wa Mo kuwekeza umeishia hapo ilipofika sasa Simba. Kama mwekezaji hawezi kununua mchezaji wa millioni 400 anasubiri amalize mkataba halafu anaota kuipeleka Simba nusu fainali kwenye CL maana yake kampuni imeweka malengo ya uongo kwani haina rasilimali ya kufikia malengo hayo hivyo basi inahitaji mtaji kutoka kwa wawekezaji wapya aidha kwa kuuza hisa zote au baadhi ya hisa.

Ni mtizamo tu.
- Kwangu Phiri hata kama sio replacement ya Mugalu na Kagere, lakini kama alisimamishwa pale kati akapatendea haki kabla ya kupata majeraha, kwangu naona hayo majaribio yalifanikiwa siwezi kulaumu chochote.

- Tumeona Phiri kabla ya kupata majeruhi, alikuwa akifunga magoli ya kutosha, licha ya timu kutokuwa na mshambuliaji wa kati na kiungo mkabaji kama unavyodai, hivyo kama timu ilifanya vizuri mwanzo, basi ikifanya vibaya, makocha kufukuzwa kwangu watakuwa hawajaonewa.

- Kuliko Mo aondoke moja kwa moja, au auze baadhi ya hisa zake, kwangu naona bora zile hisa nyingine za Simba Sc 51% apewe huyo mwekezaji mwingine atakayetaka kuja Simba Sc, kwa mtazamo wangu, naona kama zile hisa 51% zimekaa tu, hazina matumizi yoyote wala manufaa yoyote kwa timu.
 
MO ana 49% pekee
Hao wenye 51% wao hutoa nini?
Huu mchakato uliendeshwa bila kuwaelimisha na kuwapa nafasi hao 51% in short MO alitaka awe major shareholder serikali ikampiga stop.Ndio maana ukaona hao wanachama hawana power yeyote
 
Matokeo yake hizo hisa 51% mpaka leo zipo tu, bado hazijatumika vyovyote kuinufaisha klabu.
 
Ukiacha uliyoandika tatozo jingine kubwa ni mashabiki wa simba kudharau wapinzani na kuishi katika fantasy kwamba hii simba ina uwezo wa kushinda kila mechi. Horoya na azam sio timu mbovu kwaiyo hakuna maajabu yoyote kupata point kwa simba hao raja casablanca wamewazidi ubora sasa ulitegemea matokeo ya aina gani. Ifike hatua mashabiki wa simba anzeni kuwaheshimu wapinzani wenu na mkubali timu yenu haina ubora mkubwa ambao mnafikiri inao na hii itawasaidia kujiandaa kisakolojia kwa matokeo yoyote kwenye kila mechi.
Na hili la kudharau wapizani chanzo chake ni viongozi wanawaaminisha mashabiki ubora wa Simba ilihali wanajua sajili za kibailina mbovu zilizofanyika, we ukitakakujua Simba Kuna shida angalia angalia wachezaji wanaotaka kuwasajili kwa maneno ila vitendo hakuna, utoaji wa jezi hii mara ya pili zinachelewa kutoka na kiwango sio cha kurizisha.
 
Matokeo yake hizo hisa 51% mpaka leo zipo tu, bado hazijatumika vyovyote kuinufaisha klabu.
Kabla ya kufanya mabadiliko uongozi ulipaswa kufanye review ya wanachama(wangefanya massive campaign ya ku-register wanachama wapya wengi na wangetumia muda huo kuwaelimisha wanachama kuwa wao ni sehemu ya umiliki wa klabu na contribution ambayo wanachama wanaweza kuchangia kwa klabu.Majority ya wanachama wa Simba ni wazee ni hivi karibuni na hivi karibuni hawajaandikisha wanachama wapya ,bado wanatumia kadi za kizamani na wengi wanalipiwa kadi zao na wagombea kipindi cha uchaguzi.Yanga at least wanafanya registration ya wanachama wapya na imetawasaidia sana wakianza kutumia capital kutoka kwa wanachama
 
Hili suala la elimu ya umiliki hisa kwa wanachama ni muhimu lingefanyiwa kazi, watu wapo tu hawana habari na chochote kuhusu zile 51%
 
Mashabiki walimkataa kwa kura twitter, bosi akabadilisha kocha, na habari ikaishia hapo.
Ilikuwa uchaguzi wa kimhemko unadhani waliopiga kura wote walikuwa simba? Hata uto wanaweza wakapiga kura pia
Moja kosa kubwa Mo na simba kufanya ni kumtompa mgunda ukocha rasmi wa simba na kumfanya kocha msaidizi
 
Sasa mbona matatizo ndani ya Simba Sc yanazidi kuonekana ni mengi kupitiliza🫣🫣🫣
 
Salaam..

Nimekaa nikajiuliza, hasa baada ya timu pendwa ya Simba Sc kuwa matokeo yasiyoridhisha kwa mechi za hivi karibuni baada, hii ni baada ya kuchapwa 0-3 na mwarabu, na jana usiku, kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam.

Tukiondoa sababu nyingine kama wachezaji kukosa nafasi za wazi, ambalo limeonekana kuwa tatizo kwa sasa pale Simba Sc, umri wa wachezaji na uchovu kwa kucheza mfululizo miaka mingi, lakini pia naona bado kuna tatizo jingine kubwa ambalo nalo hatujalitazama kwa umakini.

Nimekaa nikajiuliza, hivi ni ipi mantiki kwa Simba Sc, hasa viongozi wake, kuamua kuwa na makocha wawili, wote wenye sifa za kuifundisha timu, wenye umri mkubwa, kwa wakati mmoja?

Kama walishaamua kufuata maoni ya mashabiki kwamba Mgunda alikuwa hatoshi, wakaamua kumleta Mzungu, sasa ni sababu ipi inayowafanya waendelee kuwa na Mgunda pale kwenye benchi la ufundi?

Huu mkanganyiko unaojitokeza sasa matokeo yake ni kama vile Simba Sc imegawanyika makundi mawili, ina kocha wa viongozi, Mgunda, na kocha wa mashabiki waliotaka Mgunda aondoke kwa kura, mzungu.

Sijui ni kitu gani kinachowashinda viongozi wa Simba Sc kumwambia Mgunda asante kwa kazi yako, wamlipe chake, kisha aondoke, wamwambie ukweli sasa tumeamua kwenda na uelekeo tofauti, uwepo wake kwneye benchi naamini unawavuruga wachezaji kwa namna fulani.

Tumeona nyakati kadhaa Mgunda akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati mechi ikiendelea, huyu mtu anaweza kuwa anatoa malekezo tofauti na kocha mkuu anachotaka, matokeo yake ni kuwachanganya wachezaji, kwanini kocha mkuu asiachwe huru kufanya majukumu yake kwa nafasi?

Kwangu, viongozi wa Simba Sc ndio chanzo cha hili tatizo, kwani sijawahi kuona timu zinazojielewa hapa duniani zinakuwa na makocha wakuu wawili, hapa wanaajiri kocha mpya, na pale bado wanaendelea kubaki na yule wa mwanzo!, halafu tunajitapa tunakwenda kimataifa, mataifa yapi hayo?!

Viongozi wa Simba Sc pamoja na Mo wabadilike, waachane na mambo ya kimazoea na uswahili mwingi kwenye uendeshaji wa timu, tusipoamka mapema itakuwa too late.
Yalikua ni mawazo ya kipuuzi tu kumwacha Mgunda na kuleta kocha mwingine. Huyu kocha wa sasa hana mbinu. Mgunda mnamsingizia tu,angalia historia ya huyo kocha. Toka mwaka 2009 mpaka anakuja Simba,ni mwaka 2014-2016 pekee ndio alikaa na timu miaka miwili. Minginw yote alikua anakaa na timu mwaka mmoja mmoja pekee
 
Pamoja na yote hayo ya benchi la ufundi na mambo yao kwangu tatizo mama la Simba ni kufeli kwenye sajili zake toka msimu uliopita.

Msimu ulipoita kati ya wachezaji wote tuliosajili ni Inonga na kanoute ndio ambao wanaoneoana kua sawa kiasi japo nao wana mapungufu yao weingine wote hamna lolote,Inonga ana makosa kadhaa ikiwemo na kucheza sana na majukwaa, overconfidence inayofanya kumsababishia hatari nyingi golini japo baadhi hua anazifanyia recovery.

Kanoute ana tank kubwa energy ya kutosha but not skilful hana maarifa mengi uwanjani yeye ni kukaba tu na rafu.

Sacko utoto mwingi hawezi kuku guarantee chochote anaweza cheza vibaya mna mwingi akafanya jambo moja likakufanya utabasamu inamana sio mchezaji wa kumtumainia.

Msimu huu yale yale katika wachezaji wote tuliosajili ni Phiri tu ndie tumeona kua tumepata wengine wote magalasa na anagalau Saidoo kaja kutupush kidogo January hapa lasivyo hali ingekua mbaya zaidi.

Leo hii kama tungefanya usajili vizuri Onyango asingeanza pale nyuma,Mzamiru asingeanza pale kati Bocco asingeanza pale mbele,Nakama nna mido mwingine wa maana hata kanoute haanzi,Sacko haanzi vilevile.

Tukajipange msimu ujao huu ushaisha
 
Back
Top Bottom