Yanga inanolewa na Nabi, akisaidiwa na Kaze. Kaze ni kocha mzuri, na mkubwa, ananitosheleza kupewa timu peke yake, na alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga.
Man UTD, Ina Ten Hag, ila moja kati ya walio chini yake ni Steve Maclaren. Huyu alishawahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya England, lakini pia alishawahi simamia vilabu kadhaa pale EPL.
So, hapo Simba acheni kuangushia jumba bovu kwa Mgunda, nyie mnamatatizo binafsi mengi.
Timu yenu ni nzuri, Ina wachezaji wenye experience, ila wengi hawakustaili kuendelea kuwepo pale.
Mechi ya jana, Azam hata hawakutumia nguvu nyingi, kazi ilirahisishwa na ninyi. Ushawahi angalia Azam vs Yanga inavyokuwaga? Huwa wanakamiaga sana, wangekamia ya jana, basi mlikuwa mnakufa goli nyingi.
Matola hakuwahi kuwa tatizo pale Simba, Mgunda pia sio tatizo, tatizo lipo kwa viongozi wenu, ambao wanamleta Manzoki kwenye kampeni, alaf kwenye usajili wanaleta Sawadogo. Simaanishi kuww Sawadogo ni mbaya, ila timu ilihitaji mfungaji zaidi kuliko kiungo.
Simba mnaendekeza sana loyalty kuliko reality. Wote tunajua, Bocco pale ni legend, ila kiuhalisia ilibidi awe ameshaondoka kitambo, au la, basi asiwe chaguo la kwanza au tegemezi.
Kiombo hana tofauti na Mzize, hawa wote ni back up strikers, ila tofauti yao ni kwamba, Mzize hana presha kubwa, maana mbele yake kuna Mayele na Musonda, so hata akikosa nafasi za wazi, halaumiwi sana. Ila Kiombo ni back up strikers anayetakiwa kuibeba timu kwa kufunga magoli kila mechi, maana mbele yake kuna Baleke (ambae bado anajaribu kuizoea timu) na Bocco ambae mwili na akili vinashindana.
Mpira ni mchezo wa wazi. Kila kinachotokea kinajionesha, wala hakuna uchawi. Mfano mdogo Liverpool, kabla ya msimu huu kuanza, wachambuzi wengi walisema wanahitajika kusajili kiungo mkabaji, maana form ya Fabinho ilionekana kushuka, pia Henderson peke yake huwa anastruggle, kwa kipindi kile haikuleta maana, ila sasa hivi ndio kila kitu kipo wazi.
Simba, Mgunda sio tatizo. Acheni ubishi.