Mtazamo Wangu: Tatizo la Simba SC kuwa na matokeo mabovu linaanzia hapa...

Mtazamo Wangu: Tatizo la Simba SC kuwa na matokeo mabovu linaanzia hapa...

Mlikuwa busy kufanya harakati za kuanzisha uzi wa feitoto na sportpesa mkasahau kuwa timu yenu mbovu
Uzi unaanzishwa JF, mambo ya timu ni kambini kati ya kocha, wachezaji, na viongozi, kama Fei anawaburuza hapa JF ndio uwanja rasmi wa kuwajuza mnavyoteswa na dogo..
 
Hao wawili walikuwa huru kutimiza majukumu yao, hawakubanwa na kocha aliyetangulia.
hapana, kocha msaidizi hawez kua kikwazo, tatizo robertinyo anaanza upya kati kati ya msimu, alipaswa kuendelea alipoishia mtangulizi wake coz timu ilikua na run nzuri then pre season ndo aanze upya.
 
Yanga inanolewa na Nabi, akisaidiwa na Kaze. Kaze ni kocha mzuri, na mkubwa, ananitosheleza kupewa timu peke yake, na alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga.

Man UTD, Ina Ten Hag, ila moja kati ya walio chini yake ni Steve Maclaren. Huyu alishawahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya England, lakini pia alishawahi simamia vilabu kadhaa pale EPL.

So, hapo Simba acheni kuangushia jumba bovu kwa Mgunda, nyie mnamatatizo binafsi mengi.

Timu yenu ni nzuri, Ina wachezaji wenye experience, ila wengi hawakustaili kuendelea kuwepo pale.

Mechi ya jana, Azam hata hawakutumia nguvu nyingi, kazi ilirahisishwa na ninyi. Ushawahi angalia Azam vs Yanga inavyokuwaga? Huwa wanakamiaga sana, wangekamia ya jana, basi mlikuwa mnakufa goli nyingi.

Matola hakuwahi kuwa tatizo pale Simba, Mgunda pia sio tatizo, tatizo lipo kwa viongozi wenu, ambao wanamleta Manzoki kwenye kampeni, alaf kwenye usajili wanaleta Sawadogo. Simaanishi kuww Sawadogo ni mbaya, ila timu ilihitaji mfungaji zaidi kuliko kiungo.

Simba mnaendekeza sana loyalty kuliko reality. Wote tunajua, Bocco pale ni legend, ila kiuhalisia ilibidi awe ameshaondoka kitambo, au la, basi asiwe chaguo la kwanza au tegemezi.

Kiombo hana tofauti na Mzize, hawa wote ni back up strikers, ila tofauti yao ni kwamba, Mzize hana presha kubwa, maana mbele yake kuna Mayele na Musonda, so hata akikosa nafasi za wazi, halaumiwi sana. Ila Kiombo ni back up strikers anayetakiwa kuibeba timu kwa kufunga magoli kila mechi, maana mbele yake kuna Baleke (ambae bado anajaribu kuizoea timu) na Bocco ambae mwili na akili vinashindana.

Mpira ni mchezo wa wazi. Kila kinachotokea kinajionesha, wala hakuna uchawi. Mfano mdogo Liverpool, kabla ya msimu huu kuanza, wachambuzi wengi walisema wanahitajika kusajili kiungo mkabaji, maana form ya Fabinho ilionekana kushuka, pia Henderson peke yake huwa anastruggle, kwa kipindi kile haikuleta maana, ila sasa hivi ndio kila kitu kipo wazi.

Simba, Mgunda sio tatizo. Acheni ubishi.
Nimependa sana ulichoandika.

Hapo kwa Kaze na Nabi, hawa nakubaliana nawe wanafanya kazi vizuri na wote wana sifa stahiki, kwani Kaze pia alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga Sc.

Tatizo lililopo Simba, Mgunda aliondolewa kwa kuonekana uwezo wake ni mdogo, ameletwa kocha mpya ambaye kwanza nina mashaka kama huwa wanaelewana kwenye mambo mbalimbali 100% kwa sababu ya lugha, tofauti na Kaze na Nabi ambao wote kifaransa kinapanda, lakini pia, tabia zetu waswahili tunazijua wenyewe, hasa majungu, fitna nk.

Mpaka hapo utaona mifano ya kina McLaren na Ten Hag pale Man utd, haifanani na hapa kwetu, waswahili tuna vitabia vyetu vya chini chini ambavyo wazungu hawana, ndio maana nikataka kocha mzungu aachwe huru kufanya majukumu yake.
 
Kwa haya matokeo mtazunguka sana kutafuta wapi mmejikwaa, lakini mbona mambo mepesi tu, kabla msimu mpya tulipiga sana kelele kuwa yapaswa kuja kivingie katika Usajili.

Kwa Simba ilihitaji walau kuwepo na Wachezaji watano wenye viwango vya CAF, wenye kuonyesha ushindani haswa ya michuano ya Kimataifa kwasababu Simba SC kwa sasa lengo ni Nusu Fainali au Fainali, hayo huwezi kufika bila wachezaji wenye hadhi ya juu.

Kocha atapewa lawama bure tu, ndo hata yule Zoran Maki baada ya kupewa malengo alisema wachezaji hawa hawawezi ndo maana Kwangu shida sio Kocha wala sijui Mangungu.

Lengo lako la mafanikio linaendana na maandalizi? Kama hatuwezi kusajili wachezaji wa viwango vya CAF tupige kimya na tusiumize vichwa bure.
 
Yanga inanolewa na Nabi, akisaidiwa na Kaze. Kaze ni kocha mzuri, na mkubwa, ananitosheleza kupewa timu peke yake, na alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga...
Ukweli mtupu, shida Simba sio makocha shida usajili mbovu na kuendelea kuwakutumia wazee km kina Boko wanakimbizwa ulimi nje
 
Kwa haya matokeo mtazunguka sana kutafuta wapi mmejikwaa, lakini mbona mambo mepesi tu, kabla msimu mpya tulipiga sana kelele kuwa yapaswa kuja kivingie katika Usajili...
Tatizo linakuja pale ambapo viwango vya wachezaji vinaonekana kushuka na kupanda kama homa za vipindi, hasa baada ya ujio wa makocha wapya, ndio maana ya hoja yangu kwamba, inawezekana uwepo wa Mgunda pale kwenye benchi la Simba Sc unampoteza mbwa kwa miluzi mingi.
 
Ukweli mtupu, shida Simba sio makocha shida usajili mbovu na kuendelea kuwakutumia wazee km kina Boko wanakimbizwa ulimi nje
Usajili ungekuwa mbovu sana kama mnavyosema, basi inawezekana leo timu ingekuwa nafasi ya nne au tano, lakini mbona bado tunaikomalia nafasi ya pili bila kushuka? ina maana hao wengine ni wabovu kupitiliza?
 
Nimependa sana ulichoandika.

Hapo kwa Kaze na Nabi, hawa nakubaliana nawe wanafanya kazi vizuri na wote wana sifa stahiki, Kaze pia alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga Sc...
Mkuu, hata Kaze ni hivyo hivyo. Tofauti yao ni kwamba Mgunda hajawahi kufukuzwa. Kama kumbukumbu zako ziko vizuri, Kaze alitimuliwa akarudi kwao Burundi, alivyoletwa Nabi, na yeye ndio akarudishwa kama msaidizi.

Alaf kingine mkuu, kocha msaidizi hawezi kutoa maelekezo kinyume na kocha mkuu. Nabi ni francophone, hajui English hata kidogo, dhumuni la Yanga kumrudisha Kaze kama msaidizi wake, ni ili aweze kutrasmit direct msg kwa wachezaji bila kikwazo maana yeye anajua Kiswahili.

Hata kwa Mgunda Iko hivyo, unapomuona amesimama kwenye touch line, basi jua anafikisha ujumbe wa Robertinho kwa wachezaji, kwa lugha wanayoielewa.

Zipo lugha za kimpira/ za ishara ambazo kocha anaweza kuzionesha, alaf wachezaji wakaelewa, lakini kuna ujumbe ambao hauwezi kuwasilishwa kwa ishara, na huo ujumbe unakuta ni lazima mchezaji/wachezaji fulani waupate, huo sasa ndio unapitishwa kwa Kaze na Mgunda.

Hiyo Simba kwasasa, hata abaki Robertinho peke yake, mtamuona hafai. Kama kumbukumbu zako ziko vizuri, kipindi cha nyuma mlikuwa mnasema Matola ndio tatizo. Sasa hivi hayupo, jumba bovu linaangukia kwa Mgunda. Tatizo lipo kwenye timu mliyonayo, na siasa za uongozi wenu.

Kipindi kile mnachukua ubingwa back to back, Yanga kila msimu walikuwa wanabadilisha almost timu nzima, maana kila usajili ilikuwa tunasajili wachezaji hata 5, 6 au 7. Wakishindwa kuperform, msimu unaofata wanatoka, wanaleta wengine wengi, mpaka siku tulipopatia, now ndio unaona tunanunua wachezaji wachache, na kuuza wachache.

Alivyoondoka konde boy na chama, mlisajili wachezaji wengi, alaf wengi mkaendelea kuwashikilia hata walivyoflop.

Kwa jinsi timu yenu ilivyokuwaga vizuri, mngekuwa mnafanya direct replacement ya mchezaji mmoja mmoja, msingepoteana. Huwezi ondoa Kagere ambae ni crucial player, alaf ukamleta Kiombo ambae ni squad player, Kisha unataka azibe pengo.
 
Yanga inanolewa na Nabi, akisaidiwa na Kaze. Kaze ni kocha mzuri, na mkubwa, ananitosheleza kupewa timu peke yake, na alishawahi kuwa kocha mkuu wa Yanga.

Man UTD, Ina Ten Hag, ila moja kati ya walio chini yake ni Steve Maclaren. Huyu alishawahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya England, lakini pia alishawahi simamia vilabu kadhaa pale EPL.

So, hapo Simba acheni kuangushia jumba bovu kwa Mgunda, nyie mnamatatizo binafsi mengi.

Timu yenu ni nzuri, Ina wachezaji wenye experience, ila wengi hawakustaili kuendelea kuwepo pale.

Mechi ya jana, Azam hata hawakutumia nguvu nyingi, kazi ilirahisishwa na ninyi. Ushawahi angalia Azam vs Yanga inavyokuwaga? Huwa wanakamiaga sana, wangekamia ya jana, basi mlikuwa mnakufa goli nyingi.

Matola hakuwahi kuwa tatizo pale Simba, Mgunda pia sio tatizo, tatizo lipo kwa viongozi wenu, ambao wanamleta Manzoki kwenye kampeni, alaf kwenye usajili wanaleta Sawadogo. Simaanishi kuww Sawadogo ni mbaya, ila timu ilihitaji mfungaji zaidi kuliko kiungo.

Simba mnaendekeza sana loyalty kuliko reality. Wote tunajua, Bocco pale ni legend, ila kiuhalisia ilibidi awe ameshaondoka kitambo, au la, basi asiwe chaguo la kwanza au tegemezi.

Kiombo hana tofauti na Mzize, hawa wote ni back up strikers, ila tofauti yao ni kwamba, Mzize hana presha kubwa, maana mbele yake kuna Mayele na Musonda, so hata akikosa nafasi za wazi, halaumiwi sana. Ila Kiombo ni back up strikers anayetakiwa kuibeba timu kwa kufunga magoli kila mechi, maana mbele yake kuna Baleke (ambae bado anajaribu kuizoea timu) na Bocco ambae mwili na akili vinashindana.

Mpira ni mchezo wa wazi. Kila kinachotokea kinajionesha, wala hakuna uchawi. Mfano mdogo Liverpool, kabla ya msimu huu kuanza, wachambuzi wengi walisema wanahitajika kusajili kiungo mkabaji, maana form ya Fabinho ilionekana kushuka, pia Henderson peke yake huwa anastruggle, kwa kipindi kile haikuleta maana, ila sasa hivi ndio kila kitu kipo wazi.

Simba, Mgunda sio tatizo. Acheni ubishi.
Great great analysis....
 
Tumeona nyakati kadhaa Mgunda akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati mechi ikiendelea, huyu mtu anaweza kuwa anatoa malekezo tofauti na kocha mkuu anachotaka, matokeo yake ni kuwachanganya wachezaji, kwanini kocha mkuu asiachwe huru kufanya majukumu yake kwa nafasi?
Hii inawezekanaje? Yaani mgunda amwambie chama piga shuti ulenge mwamba tu? Au amwambie bocco jifanye huna control uwe unapoteza mipira?

My friend haya ni mambo ya kiswahili tu tumezoea wabongo. Hakuna hujuma yoyote kiufupi selection za wachezaji mzungu yuko hovyo sana. Baleke anauwezo wa kucontrol ball kuliko bocco, anauwezo wa ku-dribble mpira kuliko bocco na hata mashuti ya baleke atleast yanatia moyo.

kingine hivi mtu ambae hajacheza mechi 6 za ligi na bado top scorer wa timu anawezaje kukaa benchi akaingia kyombo?

Mwingine atasema ni majeraha kwenye game ya raja shuti la maana la langoni alipiga phiri kwa kucheza dk zisizozidi ishirini. Hii hata haikupi picha kuwa huyu mzee ni ujinga wake mwenyewe?
 
Mkuu, hata Kaze ni hivyo hivyo. Tofauti yao ni kwamba Mgunda hajawahi kufukuzwa. Kama kumbukumbu zako ziko vizuri, Kaze alitimuliwa akarudi kwao Burundi, alivyoletwa Nabi, na yeye ndio akarudishwa kama msaidizi...
Haya yako ndio madini yanayotakiwa..

Hapo kwa Kaze na Nabi ni sahihi kusema kwamba Kaze anatumika kupeleka ujumbe wa Nabi kwa wachezaji, lakini pia kumbuka, hata ujumbe kati ya kocha na kocha pia ni muhimu sana kwa maendeleo ya timu uwanjani, hapa ndipo Kaze na Nabi wanapo win, hawa wanaelewana lugha.

Kuhusu ubovu wa wachezaji nakubaliana nawe, hasa pale uliposema hata Matola nae alikuwa akiharibu tukawa tunamlaumu, hii inaonesha matatizo yetu hayapo kwa makocha wanaopita, bali kwa wachezaji wabovu tulionao, lakini pia kwangu ndio nikaingiza kigezo cha mawasiliano kati ya makocha wawili, Nabi na Kaze wote kifaransa kinapanda, Mgunda na Mzungu?

Hapo kwenye replacement ya wachezaji umemamaliza, siongezi wala kupunguza neno.
 
Hii inawezekanaje? Yaani mgunda amwambie chama piga shuti ulenge mwamba tu? Au amwambie bocco jifanye huna control uwe unapoteza mipira...
Hoja.ya Mgunda kumuingilia mzungu nimeijenga kwenye nasharia kwamba, timu lazima icheze kwa mipango ya kocha mkuu, sasa anachowaambia wachezaji Mgunda inawezekana kikaingiliana na kile anachotaka kocha mkuu, hapa suala sio kuwaambia tu wachezaji piga shuti nk..

Suala jingine kuhusu Phiri, mbona kabla ya Phiri kuumia kocha mzungu alikuwa akimtumia vizuri kwa kumuanzisha? kwanini baada ya Phiri kuumia ndio kocha mzungu ameacha kumuanzisha?

Kwangu naona majibu ya hayo maswali hapo juu ni match fitness, hiki ndio kinaeza kuwa kigezo cha Robertinho kutomuanzisha Phiri, kwasababu yuko nae mazoezini kila siku.
 
Salaam..

Nimekaa nikajiuliza, hasa baada ya timu pendwa ya Simba Sc kuwa matokeo.yasiyoridhisha kwa mechi za hivi karibuni baada, hii ni baada ya kuchapwa 0-3 na mwarabu, na jana usiku, kulazimishwa sare ya 1-1 na Azam...
Usajili uliofanyika Simba kwa msimu huu na hata dirisha dogo umeshindwa kuleta tija iliyotegemewa, wachezaji karibia wote hasa wa kigeni ni wa kawaida mno.

Yule mlinzi wa kati sijui Qatara anasugua benchi tangia amefika
Simba kila mechi wanayocheza beki wa kushotoTshabalala, kulia Kapombe wakiumia pengo lao linaonekana dhahiri.

Ubingwawa Tanzania tusahau, tusipoangalia kwenye Champions league tutashikilia mkia kwenye group leyu
 
Hoja.ya Mgunda kumuingilia mzungu nimeijenga kwenye nasharia kwamba, timu lazima icheze kwa mipango ya kocha mkuu, sasa anachowaambia wachezaji Mgunda inawezekana kikaingiliana na kile anachotaka kocha mkuu, hapa suala sio kuwaambia tu wachezaji piga shuti nk..
Kwa sababu umesema ni nadharia okey, lakini maelekezo ya kocha yeyote yakitolewa kama yako kinyume hata uchezaji tu utaona unabadilika, siamini katika nadharia yako ila uko sahihi.
 
Kwa sababu umesema ni nadharia okey, lakini maelekezo ya kocha yeyote yakitolewa kama yako kinyume hata uchezaji tu utaona unabadilika, siamini katika nadharia yako ila uko sahihi.
Asante.
 
Maoni yako kuhusu Baleke ni dalili ya umbumbumbu na wewe ni ni moja ya watu wasiojielewa hata kidogo.

Mayele hivi karibuni amekuwa anakosa magoli kwa hiyo naye aitwe mshambuliaji machachari?

Hii Simba kweli ina watu wapumbavu sana
Mpumbavu mwenyewe heshimu maoni ya wenzako shenzi
 
Kwa hiyo kwako Mayelle kukosa nafasi kwenye mechi mbili ndio aitwe mbovu licha ya kuwa kinara wa mabao?

Wewe ni mpumbavu, tuvumiliane tu.
Hilo jamaa n jinga Sana na kilaza bin mbumbumbu katika ugaa huu wa soka
 
Back
Top Bottom