Mtazamo wangu: Walimu wa diploma ni bora kuliko ambao hawajapitia diploma wakapata degree


umenena mkuu Dip ipo juu.
 
..Nonsense. Labda mseme mwalimu wa diploma ana uzoefu zaidi-hakuna la zaidi hapo. Kama utawapima kwa uzoefu wa kufundisha, hata mwenye degree atakuwa mzoefu baada ya muda mfupi. Kwa ujumla, waalimu, hasa wa kizazi hiki hamna cha kujivunia ktk taifa hili. Waalimu wengi ni vilaza mwanzo mwisho. Mnaenda ualimu kwakuwa mna four point 28 na kwakuwa mmeshinda kupata credit za kuendea chuo kikuu. Kiingereza mnachofundisha ni uongo mtupu na hata kwenye kiswahili ni shida tupu.

Nini maana ya elimu kama haiwezi kukukomboa? Mbona mmeshindwa kudai haki zenu kama kweli mnafundishwa vizuri? Mbona mmeshindwa kudai posho kama askari pamoja na kwamba mazingira ya kazi yanafanana? Hamjui kwamba chaki ni silaha kali kuliko bunduki? Shame on you!
 

Mkuu umeamua kutukana. Acha siasa. Jenga hoja
 
Mkuu umeamua kutukana. Acha siasa. Jenga hoja

Ndugu yangu sikuhizi watu hawajengi hoja zaidi ya kutoa povu kwa kuhusisha kila kitu na siasa. Ukimuuliza yeye aliyepata div one amedai nini na kufanikisha katika mfumo wa leo atakupa bonge la tusi.
 
1.Je mfumo wa wa2 wanofeli ksomea dploma/cheti/bachelor vp?!2.Elimu ya vacty ni closed clas bt open library,colej nyng za edu ktk vacty TZ zpo so equipd!3.Kuna utofaut ktk levoz za taluma & jins ya kdeliver MATERIALS!4.Mhadhiri hawez fana2 & mkufunz!
 
1.Je mfumo wa wa2 wanofeli ksomea dploma/cheti/bachelor vp?!2.Elimu ya vacty ni closed clas bt open library,colej nyng za edu ktk vacty TZ zpo so equipd!3.Kuna utofaut ktk levoz za taluma & jins ya kdeliver MATERIALS!4.Mhadhiri hawez fana2 & mkufunz!

mkuu sijapata msimamo wak
 
ahsante MPATANISHI kwa upatanishi wako

mkuu nimepitia dip marangu TTC mkuu,pale unapikwa unapikika haswaaa sitapasahau ni hatua moja muhimu katika maisha yangu. Ualimu ni zaidi ya kufundisha. Wakati nipo field himo niliwafunika masharobaro wa degree wa Mwuce. Mpaka naondoka wanafunzi wamelia machozi. Najivunia kuwa na Dip mkuu na sasa nipo shahada.
 
Mkuu umeamua kutukana. Acha siasa. Jenga hoja

hata mm namshangaa eti 4.28 ndio tumeshindwa kwenda university?!!

Nimepita dip nikitokea advance na div II.10 safi na chuo nilipata udom na mzumbe ila mkopo walinipa 40% b'se A level nilipiga private.

Kwa kuwa sikua fit financialy na sikutaka kusumbuana na bodi mana walishakataa kuniongeza nikaamua kukamata dip 2 years na sasa namalizia shahada mbali na ualimu.

Huyu jamaa anaonekana hata ualimu haujui mana div 4 hata iwe ya 26 tangu lini akaenda university kusoma Ba. Ed?!
 

haswa ndo lengo la mada yangu. Hongera mkuu
 

kwa mara nyingine umekuwa mpatanishi
 

Hiyo ratio uliyoitoa nadhani niyakufikirika zaidi kuliko uhalisia!!! Wewe unatakakusema unawafahamu walimu wote waliyoko shule zote za tanzania?
Unapashwa kuwa na mtizamo chanya vinginevyo shule zote za nchi hii zingekuwa na daraja la nne na zeros basi. Nashawashika kuamini kuwa walimu unaowahamu ni wale waliyokufundisha wewe na kwa maana hiyo ni wale walikufundisha masomo uliyoyasoma tu. Hivyo kuna weza kukawa na walimu wazuri tu kwenye shule hiyihiyo ila tu hawajakufundisha nao umewapeleka kule kwenye walimu wasiojua kazi yao au hawana ari ya kufundisha. Badilika bana!!!
 

mkuu umemaliza.
 


mimi mwenyewe ni matunda ya hao jamaa ulio wataja.baada ya hapo nlipitia ualimu na nikawa mkufunzi wa chuo ingawa niliacha na kusomea professional tofauti sana na ualimu ila kuna mambo ambayo nime observe ktk miaka yote ya shule kuanzia primary,sec na finaly kuwa mkufunzi.mnaomba niwashirikishe;
  • katika vyuo vya ualimu(diploma & certificate) kuna aina mbili za wanachuo,ya kwanza ni wale ambao wanaamini kuwa hawana namna ingine ya kutoka kimaisha hivyo wanaamini kuwa ualimu ndio professional itakayawatoa,hawa hujituma kujifunza mbinu bora (ubunifu) na namna gani watakuwa waalimu wazuri,pia kuna wa aina ya pili ambao wao wanaona ualimu ni kazi ya bahati mbaya kwao na wamelazishwa na wajomba,shangazi baba etc kusomea hawa huwa wanaenda tu ili mradi hawana ubunifu wanapomaliza masomo mara nyingi ni wavivu na wana discourage wanafunzi hawana positive motivation hata mfumo wa kuwaadhibu wanafunzi kwao ni tofauti wanachukulia adhabu kuwa ni kumkomoa mtoto na si kumsaidie abadilike positvely(as suggested in ed. psychology)
  • jambo lingine ambalo nimelishuhudia ambalo lilinifanya niwakumbuke walimu wangu wa tuition nliopitia wakina Ngida,mudi,hidden,busanji,mkanda na mama shija; ni kuwa unapoenda kusomea ualimu kama ulikua academically fit ulipokuwa secondary basi unayo nafasi nzuri ya kuwa mwalimu bora na hii ndio inayo wagusa waalimu wengi wa tuition kama hao nliowataja ambao wanaonekana walikua fit enzi zao wakiwa wanafunzi,tatizo kubwa linalowakumba waalimu wengi now days ni kuwa unaenda ualimu kama last option na mbaya zaidi kama ukiwa sec mambo yalikua yanakugonga na mbaya zaidi huna motivation ya kujituma ni balaa
  • Kwa upande wa dp.ed teachers hawa wana nafasi nzuri ya kuwa waalimu wazuri(sio wote) kutokana na kutumia muda mwingi katika teaching methodology,strategies etc,pia wanaimarishwa sana kwenye maeneo ya ed psychology(applications),curriculum and teaching etc na mengine ila graduates wanajikita zaidi kwenye nondo(theories etc) hapa ndo utofauti unapotokea,kwa upande mwingine vyuo vya ualimu wa diploma kuna mfumo ambao mwanachuo analelewa katika maadili ya kumbana ili awe mlezi mzuri katika every aspects wakati kwenye degree ni utawala huria no one cares mradi hujasup unaendelea semister ingine suala la maadili ya ualimu kwa graduates ni utawala binafsi!!!!!! so kwa ujumla wake most of diploma holder teachers wako more professional ingawa si wote but graduates wa ualimu si wengi ambao wako highly commited wengi husema "mi napita tu bwana kwenye ualimu"............za mwenzio changanya na zako!
 

Ndiyo maana kuna seminar, na mjadala mzito wa yaliyofundishwa kupitia njia ya lecture hujadiliwa kwenye seminar kwa hiyo sio njia ya kukaririsha wafundishwa endapo seminar zinazingatiwa ipasavyo.
 
@planner, ahsante sana kwa uchambuzi wako mzuri. Nimejifunza mengi na mada yangu imekuwa ni changamoto nzuri
 
Ndiyo maana kuna seminar, na mjadala mzito wa yaliyofundishwa kupitia njia ya lecture hujadiliwa kwenye seminar kwa hiyo sio njia ya kukaririsha wafundishwa endapo seminar zinazingatiwa ipasavyo.

kwa hiyo tatizo liko wapi
 

Hao walimu watakuwa bora kwa vigezo vyako kama watabaki na diploma zao ila wakienda kusoma degree wakirudi watakuwa na vigezo sawa na waliounganisha degree bila kupita diploma. Sababu kubwa wa dip. wanafundishwa sana utii 'ndiyo mzee' kuliko kuhoji (nadhani) na hawaoni future nyingine zaidi ya ualimu na hutenda kazi kwa bidii wakiwaza kufikiriwa kwenye vyeo vya ngazi ya shule ambavyo wa degree huwa haviwazii sana. Nasema hawahoji mfano nshawahi kufanya field chuo cha ualimu Songea kwanza nkagundua wimbo wa chuo wanaouimba kila j'tatu ulikuwa na baadhi ya mistari inayomalizikia "ualimu ni witooo" sa unategemea akienda kazini atahoji chochote. Pia nilikuta walimu vijana wenye degree pale wako busy na mambo yao (kazi za nje) ya kuongeza kipato mfano wengine wanapiga dili hadi open university na hao wenye dip. ndo wengi walikuwa wamekamata vyeovyeo vya idara na wanaonesha kuridhika. Mambo mengi sana yanawafanya wa diploma wawe walimu 'haswa'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…