Mtego Aliojitegea Rais Samia, nani atauvunjilia?

NImemtafsiri vibaya?! Tatizo wewe umejikita kwenye conclusion yake na umeacha utangulizi wake!

Ndugai anaanza kwa kusema:

"Lakini fikiria, nyinyi ndo wasomi. Kwa mfano Mama juzi ameenda kukopa 1.3 Trillion. Deni. Na tuna majengo hivi sasa, ya madarasa, vituo vya afya, ambavyo yanajengwa, kwa tozo. Hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni, au tubanane banane hapa hapa tujenge wenyewe bila ya madeni haya makubwa makubwa yasiyoeleweka? Ni lini sisi tutafanya wenyewe? And how? Tutembeze bakuli? Ndiyo heshima?"

Hivi huoni hapo anamshutumua Mama, tena PERSONALLY na sio serikali, Kwamba mama ameenda kukopa 1.3 Trillioni wakati tuna majengo ya madarasa na vituo vya afya ambavyo yanajengwa kwa tozo! Yaani kwa maana nyingine, ni kama anatuambia hata hizi habari za madarasa kujengwa kwa mkopo wa COVID ni uongo kwa sababu yanajengwa kwa pesa za tozo!! Ni kutokana na hivyo, ndo maana Ndugai anamshangaa Mama kukopa kwa madai ya kujenga madarasa wakati madarasa yanajengwa kwa tozo!!!

Hivi hadi hapo hujaona Ndugai alitakiwa kutuambia Watanzania kama hayo majengo yanajengwa kwa tozo, sasa Mama kapeleka wapi hizo 1.3 Tillion alizotudanganya zinajenga madarasa na vituo vya afya wakati according to Ndugai, huo ni uongo?

Na ndugai anaendelea kusema "madeni haya makubwa makubwa yasiyoeleweka!"

Tafakari hiyo kauli na kauli ya mwanzo! Of course, kama hayo majengo yanajengwa kwa tozo na sio mkopo, basi mama katuingiza kwenye madeni yasiyoeleweka!! Mwanzoni tulikuwa tunalielewa deni husika kwa sababu mama alitudanganya anajengea madarasa na vituo vya afya, kumbe according to Ndugai, huo ni uongo, na kama ni uongo ana kila sababu ya kuita madeni yasiyoeleweka kwa sababu Ndugai, pamoja na kuwa spika anayetoka chama kile klle lakini hafahamu tozo hizo zinafanya kazi ipi!
 
Kwa Hali ulivyo sioni namna ya ndugai kuendelea kuwa spika kwa Hilo lililotokea, anapaswa kujiuzulu au kuondolewa.Mama kakataa msamaha wake
Sasa hapo unatakiwa ujiongeze. Leo ni siku ya tatu Ndugai hajajiuzulu, unadhani wana weza kumuondoa kwa kura ya kuto kuwa na imani? Rais Samia atapata wapi theluthi mbili ya wabunge? Kumbuka Ndugai haja sema kila kitu........( ) unajua ni kwanini mkopo huu umekopwa bila kupitia Bungeni?? TAFAKARI.
 
Kama vipi avunje bunge aone kama hajarudi kwao Zanzibar.
 
Namkubali mama kwa kuacha unafiki na kumpasulia Ndugai mayai viza. Unafiki wa viongozi waliopita kusameheana kienyeji ndio ulioifikisha nchi hii hapa ilipo. Hongera mama Rais Samia kwa kuonyesha msimamo thabiti na ukomavu wa kisiasa. Tupo nyuma yako ✍️
 
Tunasimama na Mama.

Jambo la Mama ni Jambo letu
 
Wale wagonga meza ni wazee wa tumbo-cracy na ugali-nomics
 

Sasa mkuu kwani wanafanana kweli kwa tabia? Binadamu tunatofautiana.
 
Na raha ya mama yuko wazi kwa anachokisudia na hapepesi macho kudangaya Ili apate sifa za kipumbavu.

Umpende au umchukie she doesn't care.La Ndugai ni onyo kwa wengine wawe na adabu.
 
Akigombea 2025 na kufanikiwa kuwa rais hysee anguko lake litaitikisa dunia nzima
 
Mtego umenasa.... wataenda kumvua uanachama na hivyo kupoteza Ubunge.. ataungana na G19.
 
Nakiona kibarua kizito hapo mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duh! hii series ni ndefu alafu...
 

Kwamba hatuku capitalize kwenye mtafaruku huu, haifahamiki ni magoli ya namna gani tunataka kufunga!

Kujiuzulu kwa Ndugai: Hongereni CHADEMA na NCCR japo haikutosha

Cc: Babati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…