Bando la wiki
JF-Expert Member
- May 23, 2023
- 911
- 3,017
Hello!
Natumai mu wazima!
Nchi ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ni yetu sote watanzania ila kitu kibaya kuna baadhi ya kundi dogo la watu kuona nchi hii ya Tanzania inapaswa kuwa mali yao binafsi.
Hilo ni kosa kubwa kwa chama tawala kudhani wao ndio wanapaswa kutawala nchi hii miaka yote. Sasa anguko lao litakuja ghafla wakati ambao hawakuutegemea.
Lakini kwa miaka ya hivi karibuni nadhani watawala wanaona namna mwanga wa mapinduzi unavyozidi kuchomoza kwa jamii kubwa ya watanzania.
Zile blah blah kwamba sijui chama cha mapinduzi ni chama cha mababu, hivyo vijana wakipende hizo stori kizazi hiki hakitaki kuzisikiliza kwa sababu ni wao wanaumia na mifumo mibovu ya wizi, ufisadi na rushwa kutoka kwa mamlaka vinavyokwamisha mstakabali wa maisha yao yaliyo bora.
Sasa hawa vijana kuchoma tairi na kuingia barabarani ni suala la muda tu na kupata mtu wa kuwaaminisha kufanya hayo. Vivyo wana CCM msichukulie powa kabisa wananchi wa Tanzania hasa tunapoelekea uchaguzi wa 2025.
Mtego wenu upo kwenye WIZI WA KURA kama kawaida yenu.
Msijichanganye mkaenda na hayo mazoea kwenye uchaguzi mkuu wa 2025.
Mkilazimisha mkaiba kura, wananchi watawafurahisha mipango hiyo nadhani mnaiona hamasa kwa wananchi inaendelea vizuri.
Lakini kama kawaida mkilazimisha, wakurugenzi wenu kutangaza wanachama wa ccm wote kuwa ndio washindi wa uchaguzi kama yule mwendazake. Wakurugenzi nao wataitikia kwa moyo wote ili kuifurahisha mwajiri wao.
Hapo ndipo mtego mwingine utaibukia kwa sababu nchi itajikuta wabunge wote na madiwani wote ni wa chama kimoja hivyo swali kwa jumuiya ya kimataifa itakuwa inawezekana vipi ninyi mnajiita nchi ya kidemokrasia ya mfumo wa vyama vingi ila tunaona uchaguzi wote wanachama wa chama tawala ndio wameibuka washindi?
Hilo swali litakuwa gumu sana kwa serikali ya CCM kwa sababu kuna baadhi ya kamati za bunge zinapaswa kuongozwa na kambi rasmi ya upinzani ambao watakuwa hawapo. Hivyo madhara yake ni kuanza kukosa mikopo ambayo mingi yao inazingatia hali ya utawala bora.
Lakini ule mtelezo ambao ccm iliupata kwa kupata wale wabunge 19 (COVID-19) wa CHADEMA 2020. Hautakuwepo kwa sababu CHADEMA now kinaenda kusukwa upya. Habari za kupitia nyuma ya milango na kufanya maridhiano hayatakuwepo tena.
Hivyo ccm kila hatua ambayo mtachukua kinyume na utaratibu mjue mnajiingiza wenyewe kwenye mdomo wa mamba.
Suluhisho: mje na tume huru ili uchaguzi uje uwe wa uhuru na haki anaishinda kwa haki atangazwe kwa haki, kinyume chake mtafurahishwa na wale msiowategemea kabisa.