Mtego wa kuoa/kuolewa na mtu wa dini yako unavyoweza kukucost maishani

Mtego wa kuoa/kuolewa na mtu wa dini yako unavyoweza kukucost maishani

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
5,771
Reaction score
17,849
Kuna baadhi ya madhehebu ya dini yameweka msimamo kwamba muumini haruhusiwi kuoa/olewa na mtu wa dhehebu lingine.

Binafsi nimeona watu wakipata matatizo yafuatayo kutokana na msimamo huo;

1. Baadhi ya madhehebu hayo unakuta vijana (hasa wanaume) ni wachache. Kwahiyo linapokuja suala la kuolewa unakuta wadada wengi wanaishia kukosa waume wa kuwaoa. Hii nimeishuhudia "live"

2. Wengi wanafanya kigezo cha dini kwamba ndio kigezo kikuu cha kupata mwenza. Matokeo yake, mtu akishapata wa dini yake basi anakua haangalii tena au haweki umakini kwenye kuona kama huyo mtu ana vigezo vingine. Matokeo yake ni kubeba "bomu" ilimradi tu ni la dini yako!

3. Wengi wameacha/achwa na watu waliowapenda sana kutoka moyoni kisa sio wa dini yao. Matokeo yake wanaishia kuoa/olewa na watu wa dini zao ambao kiuhalisia unakuta hawana mapenzi nao ya dhati zaidi tu ya kwamba ni dini moja. Matokeo wote tunayajua

4. Inapotokea mtu kaolewa na huyo wa dini yake na mambo hayaendi, wengi wanashindwa/wanaogopa kuchukua hatua, hata tu kulalamika, kwa kuhofia waumini wenzao, wazee wa kanisa nk watawachukuliaje? Wengi wanavumilia mateso kimya kimya kwa kulinda "heshima" ya wenza/wazazi nk kule kanisani.

5. Madhehebu mengi (hasa wakristo) hayana utaratibu wa kuvunja ndoa. Mkishaoana, hata uteswe vipi wao watashauri "uvumilivu" labda mpaka mmoja auawe ndio wataingilia. Ikumbukwe kuuawa sio lazima kimwili, kuna watu wameuawa kiroho, kisaikolojia, kihisia nk kupitia hizi ndoa.

Nini kifanyike?

Kijana kabla ya kuoa/olewa tambua kwamba hizi dini zimekuja zimetukuta. Pia tambua kwamba kwenye hiyo dini yako pia kuna "mbwa mwitu waliovaa ngozi za kondoo." Usidhani kwamba wanaume/wanawake wa dini yako ndio "malaika". Fungua akili na upeo wako dunia hii ina watu wengi sana wazuri, kwanini ujifungie kwenye "boksi" la udini?

Jiulize ni kwanini hapa duniani unaruhusiwa kuoa/kuolewa;
  • na mtu wa kabila lolote
  • na mtu kutoka nchi yoyote
  • na mtu wa rangi yoyote
  • na mtu wa chama chochote
  • na shabiki wa timu yoyote

LAKINI SIO MTU WA DINI YOYOTE!?
 
Gen Z hawafungwi na dini walio wengi, elimu imefuta huo ujinga labda wachache waliokosa ilimu dunia
 
Back
Top Bottom