Mtei Express Babati - Dar mna huduma mbovu sana zisizoendana na nauli

Mtei Express Babati - Dar mna huduma mbovu sana zisizoendana na nauli

Joseph Gadiel

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2022
Posts
407
Reaction score
713
Hili basi lilipoanza huduma ya Luxury mara ya kwanza lilikuwa vizuri ila kadri siku zilivyoenda huduma zimegeuka kuwa za hovyo sijui tatizo ni nini, Usimamizi mbovu no customer care at all imagine na hii ni Luxury na imeidhinishwa kama gari la level ya Luxury na wanatambulika LATRA kama Luxury bus na abiria wanalipa nauli level ya Luxury.Picha linaanza,

Vinywaji ni maji na soda kwa siti, ukikosa soda hutaki maji shauri zako!

Vinywaji vinagaiwa vinaishia siti kadhaa za mbele, waliopo nyuma imeisha hiyo!

Mwanzoni walikuwa wanagawa chai na kahawa vimefungwa vyema ndani ya takeaways siku hizi mhudumu anatembea na vikombe na maji ya moto huku vijiko na sukari amevibania kwapani! Unaulizwa chai au kahawa, unamiminiwa anatoa kijiko kwapani anakuweke sukari, majani anakukorogea 😄

Wamejaza vistuli na ndoo ndani ya basi na wanaokota okota abiria njiani ndani wamejazana utadhani gari za mbagala

Hawana customer care kabisa lugha mbovu jeuri viburi wanafoka balaa! 😄 Ukimgusa bega kumnong'oneza jambo utasikia anapayuka "Sasaa kaka nilishasema abiria blah blah blah!" Hapo anatoa sauti kubwa basi zima wanasikia!

Mengine nitarudi kumalizia...


20230620_120641.jpg
 
Narudia kusema Tz hakuna luxury bus na hata kukiwepo watafanya huduma nzuri na standard kwa muda mfupi sana na wataendelea na huduma mbovu za bora liende.

Juzi nilisafiri na dogo mmoja ana smart phone yake alivyoingia kwenye bus alijua atatumia WiFi safari yake yote akawa ananiuliza namna ya kukonekti WiFi nikamwambia ni waongo tu wameandika kwenye bus ila ndani ya bus hakuna huduma hiyo ni wezi na matapeli tu.

Dogo alikuwa mnyonge na mpole na smart phone yake ya Kichina.

Hii ndio Tz kila sehemu ahadi hewa kama issue ya DP World leo wanasema ajira zitakuwa nyingi mradi ukianza hakuna ajira kwa watz labda kwa hao watoto wa machawa na mataga.
 
Pole mkuu kwa yaliokukuta kwenye kampuni hiyo ambayo imeitaja jina, jibu ni dogo tu ,acha kutumia fedha zako kwenye kampuni hiyo,unless unataka wa improve service standards zao ,ila hili lingekuwa Sawa kama uzi huu ungewapelekea kwanza wao ili kuwapa nafasi ya kujibu, kwa sasa labda haya ni majungu tu, pls mtoa hoja cc uzi huu kwao (definitely ticket yao ina contact details),then uje hapa na malalamiko yako na majibu yao
 
Ukitaka huduma nzuri babati upande shabiby au maning nice
 
Back
Top Bottom