Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mtembea kwa miguu aliyegongwa na Basi la Abiria la "Mwendokasi" wiki iliyopita ambaye ndiye alikuwa Majeruhi pekee wa ajali hiyo aliyesalia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), ameondolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodi nyingine ya HDU baada ya afya yake kuzidi kuimarika.
Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amesema pamoja na mambo mengine Majeruhi huyo ameanza kuongea na amejitaja kwa jina moja kwamba anaitwa Osam na Makazi yake ni Manzese, Dar es salaam “Tunaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki wanaomfahamu wajitokeze ili kushirikiana nasi kumuhudumia na kumfariji”
Chanzo: Ayo Tv
Pia soma:
- MOI: Mwanaume aliyegongwa na Basi la Mwendokasi yuko ICU
- Ajali ya Mwendokasi makutano ya Jamhuri na Morogoro Road
UPDATE
Ndugu na mke wa wa majeruhi wa mwendokasi wamejitokeza na kumtambua
Zaidi soma: Aliyegongwa na mwendokasi atambuliwa na mkewe na ndugu yake