Mtembea kwa miguu aliyegongwa na basi la mwendokasi atolewa ICU

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731

Mtembea kwa miguu aliyegongwa na Basi la Abiria la "Mwendokasi" wiki iliyopita ambaye ndiye alikuwa Majeruhi pekee wa ajali hiyo aliyesalia katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), ameondolewa katika Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) na kuhamishiwa wodi nyingine ya HDU baada ya afya yake kuzidi kuimarika.

Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amesema pamoja na mambo mengine Majeruhi huyo ameanza kuongea na amejitaja kwa jina moja kwamba anaitwa Osam na Makazi yake ni Manzese, Dar es salaam “Tunaomba Ndugu, Jamaa na Marafiki wanaomfahamu wajitokeze ili kushirikiana nasi kumuhudumia na kumfariji”

Your browser is not able to display this video.

Chanzo: Ayo Tv

Pia soma:


UPDATE

Ndugu na mke wa wa majeruhi wa mwendokasi wamejitokeza na kumtambua

Zaidi soma: Aliyegongwa na mwendokasi atambuliwa na mkewe na ndugu yake
 
Kuna wapuuzi walishazusha kuwa kafa, MUNGU anawaumbua

USSR
 
Mungu ni mwema! Shukrani kwa madktari waliompambania afya yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…