Ni kweli Mtemi Mirambo( Maana ya mirambo ni " maiti nyingi" alikuwa hatari sana...
1) Alikuwa anatengeneza silaha mwenyewe...Magobole ( Hata ile nyimbo ya Oooh Tanu yajenga nchi) imechukuliwa kutoka kwenye nyimbo ya walugaluga waliokuwa wakiimba Kinyamwezi kuwa risasi zinabomoa vichwa" bela mitwi"
2) Alikuwa ana wanajeshi hodari sana ( walugaluga) sifa yao hawa jamaa walikuwa wanavuta bangi kama wanavuta sigara...wakishapiga vitu vyao walikuwa ni wakali kama pilipili au sungusungu weusi
3) Alikuwa ana wataalam (wachawi) wa maana hasa, ambao walikuwa wana uwezo wa kuona mambo kabla hata hayajatokea. Hivyo hata kama kuna adui ana mipango ya kuja kumshambulia, anakuwa ameishaonekana na kujulikana atatokea pande gani.
4) Alikuwa ni chief mwenye nguvu za kiuchumi zaidi hata ya Mkwawa, kwasababu alikuwa kwenye route kuu ya kutoka nchi za Congo, Burundi na Rwanda, hivyo ilikuwa lazima kumlipa kodi. Waarabu, wazungu na wafanyabiashara mbalimbali walipokuwa wanapitisha dhahabu,almasi, pembe za ndovu na watumwa, walikuwa wanaacha mzigo wa kutosha! Hiyo ikamfanya awe mwenye nguvu Sana.
Ni kichekesho sana kumlinganisha Mkwawa na Mirambo