Mtemi Mirambo VS Mtemi Mkwawa

pole sana homie, kama kawaida yako jana usiku hujala sio!!! nikupitishie viazi na karanga tena baadae najua haujashiba vizuri.

amenishangaza ujue, Milambo na waruguru wapi na wapi mh! haya mjukuu wa mtemi Milambo....ushinde salama.


Homie....!

Karibu matobolwa...😋 Na maziwa...😋
 
Kwa nini umemaliza na neno magufuli4life?
 
Mirambo alikufaje??
Ni saratani ya koo au alinyongwa koo mpaka kufa??
Inaonekana alifariki katika umri mdogo miska 44
 
Mirambo alikufaje??
Ni saratani ya koo au alinyongwa koo mpaka kufa??
Inaonekana alifariki katika umri mdogo miska 44
"Near the end of his life he grew ill, and died, age 44. It is possible that he was strangled to death, since an old Nyamwezi custom was to strangle their mtemi when they became unfit to rule."
 
Why was he unfit to rule?
Nimeleta nukuu tu, sikuweza kuthibitisha chanzo cha habari. Naielewa hivyo.
Mirambo alikuwa kiongozi wa kivita, alipanusha himaya yake kwa njia ya vita. Mamlaka yake juu ya rugaruga ilitegemea uwezo wake kumshinda mpinzani wowote.
Sijui historia ya Wanyamwezi, lakini najua mifano mbalimbali kutoka tamaduni mbalimbali ambako mfalme aliuawa akizeeka mno au kuwa mdhaifu kutokana na ugonjwa. Maana hakufaa tena kama hana nguvu.
menginevyi nimekuta kwamba alikuwa na kansa. Vita yake ya mwisho dhidi Burundi alishindwa kuongoza menyewe akamtuma
Why was he unfit to rule?
 
Kitabu cha "Imperial Footprints: Henry Morton Stanley's African Journeys" cha mwaka 2004 kimesema " Mirambo passed away on December 2,1884 probably due to throat cancer and his empire died with him.

Angeuwawa sababu ya kunyonywa ili apatikane kiongozi mwingine jasiri basi inawezekana ngome yake isingekufa.

 
Ni kweli Mtemi Mirambo( Maana ya mirambo ni " maiti nyingi" alikuwa hatari sana...
1) Alikuwa anatengeneza silaha mwenyewe...Magobole ( Hata ile nyimbo ya Oooh Tanu yajenga nchi) imechukuliwa kutoka kwenye nyimbo ya walugaluga waliokuwa wakiimba Kinyamwezi kuwa risasi zinabomoa vichwa" bela mitwi"
2) Alikuwa ana wanajeshi hodari sana ( walugaluga) sifa yao hawa jamaa walikuwa wanavuta bangi kama wanavuta sigara...wakishapiga vitu vyao walikuwa ni wakali kama pilipili au sungusungu weusi
3) Alikuwa ana wataalam (wachawi) wa maana hasa, ambao walikuwa wana uwezo wa kuona mambo kabla hata hayajatokea. Hivyo hata kama kuna adui ana mipango ya kuja kumshambulia, anakuwa ameishaonekana na kujulikana atatokea pande gani.
4) Alikuwa ni chief mwenye nguvu za kiuchumi zaidi hata ya Mkwawa, kwasababu alikuwa kwenye route kuu ya kutoka nchi za Congo, Burundi na Rwanda, hivyo ilikuwa lazima kumlipa kodi. Waarabu, wazungu na wafanyabiashara mbalimbali walipokuwa wanapitisha dhahabu,almasi, pembe za ndovu na watumwa, walikuwa wanaacha mzigo wa kutosha! Hiyo ikamfanya awe mwenye nguvu Sana.
Ni kichekesho sana kumlinganisha Mkwawa na Mirambo
 
Kuna ushahidi gani kuwa alikuwa anatengeneza magobore?
 
Mkutano wa Berlin uliharibu mno mfumo wetu wa maisha - sasa hivi tungekuwa na tawala nyingi tu ambazo tungeshindana kwa maendeleo badala ya hii dola moja ambayo tunasonga hatusongi miaka inayoyoma.
 
Kwahiyo hilo unaona ni ushujaa?
 
Kuna ushahidi gani kuwa alikuwa anatengeneza magobore?
Sasa kutengeneza magobori si teknolojia kubwa wakati wa karne ya 19 . . . Kama angeishi miaka 6,7 zaidi angekutana na askari Wasudani wa Wajerumani asingekuwa na uwezo wa kupinga tena.
 
Rungwe huko Mjerumani na watu wake walichapwa mpaka sijui wakaangukia Nyasaland huko tena kimyakimya.
Nenda uliza kilichofanyika mwakaleli na Rungwe.
 
Google tu Germany east africa kyusaland.
Ee kaka sasa unakimbia. Labda ulisikia jambo bila uhakika sasa huwezi kutuambia kitu tuende google?
Wanyakyusa wakati wa mwanzo wa ukoloni hawakuwa na nguvu maana walikuwa na machifu wadogowadogo tu. Merere wa Usangu aliwavamia bado mwaka 1892 akapora mifugo na wanawake.
Wajerumani walifika baada ya 1890 tu, maana walianza utawala pwani walipopambana an Abushri na baadaye na Wahehe. Hapakuwa njia hadi Tukuyu kenye nchi kavu. Wamisionari wa kwanza walifika 1891 kupitia Ziwa Nyasa.
Hali halisi eneo lilikuwa nje ya upeo wautawla wa kikoloni kwa miaka, na mwaka 1900 tu serikali ya koloni iliunda kituo cha utawala Neu Langenburg (leo Tukuyu) bila mapigano, baadaye walianzisha kituo cha kijeshi Masoko ambo waliweka kombania moja, lakini hapakuwa na mapigano.
Je vita yako ilitokea wapi na lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…