Wewe bhana ni ama huifahamu historia ya Mtemi Mirambo au unaifahamu lakini unaamua kuipotosha kwa makusudi kama ilivyo ada yetu!!
Mosi, Machifu/Watemi wengi wa Kiafrika walikuwa ni wafanyabiashara ya Watumwa, na Mtemi Mirambo ni miongoni mwa Watemi ambao walibobea sana kwenye biashara hii!!
Pili, ni kweli Mtemi Mirambo alikuwa very powerful kijeshi na alitumia jeshi lake ku-block route kuu ya Msafara wa Watumwa kutoka Magharibi! Hata hivyo, hakufanya hii blocking kwa sababu alikuwa anapambana na biashara ya utumwa bali alikuwa analinda interests zake dhidi ya Wafanyabiashara wa Kiarabu!!
Umemshusha sana Mkwawa kuhusu uwezo wake kivita compared to Mirambo! Unafanya hivyo huku ukisahau au labda hujui kwamba Mkwawa alikuwa anapambana na Watawala (Wajerumani) wakati Mirambo vita zake nyingi kama sio zote zilikuwa ni dhidi ya Watawala wenzake wa Kiafrika au Wafanyabiashara wa Kiarabu!
Unlike Mkwawa, Mirambo hakuwahi kupigana na madola makubwa ya magharibi kwa sababu mwaka aliokufa ndio huo huo ambao Mabeberu walikutana kumegeana bara letu!!
Kwamba, unlike Mkwawa aliyekuwa na silaha duni kabla hajapewa bunduki moja na Mwarabu huku Mirambo akitengeneza bunduki hizo mwenyewe, hapo unaonesha upotoshaji wako mwingine ama kwa makusudi au kwa kutojua!!
Ukiisoma historia ya Mirambo wala hutachelewa kufahamu Mirambo kapewa sana bunduki na Wafanyabiashara wa Kizungu, na hivyo kuchangia sana kuwa na jeshi lenye nguvu!
Ni kumkosea heshima Mkwawa kudharau uwezo wake simply because alishindwa vita dhidi ya Mjerumani aliyekuwa sio tu Mtawala bali alikuwa na zana za kisasa za Kivita!! Mjerumani ambae hata leo bado ana uwezo wa kututwanga taifa zima let alone a portion of the country!
Aidha, nikukumbushe kwamba, hao ambao umesema "Hapakuwa na Wazungu wa kuleta fyoko"; nikifahamishe tu kwamba, hao hawakuwa Wazungu Watawala bali Wazungu Wafanyabiashara na Mawakala ambao hawakuwa na dola wala jeshi ndani ya ardhi yeu! Na ndio maana hata wewe mwenyewe unakiri kwamba:-
Wazungu baada ya kubanwa sana waliomba nguvu ya jeshi kutoka kwa sultan wa Zanzibar wakimwambia kwamba Napoleon wa Afrika anataka kuiharibu biashara yako kwakuwa ndiye alikuwa mnunuzi mkubwa wa pembe za ndovu na watumwa kutoka Zaire na Zambia.
Huo ni ushahidi tosha kwamba hao Wazungu unaosema hawakuleta fyokofyoko ni Wazungu ambao hawakuwa na jeshi wala dola na ndio maana wakaomba msaada kwa Sultani...
Hawa sio Wazungu aliopambana nao Mkwawa unyemdharau ambae yeye alipambana na Wazungu wenye Jeshi la Kisasa na Dola!!
Mkwawa unayemdharau hakupigana na Wazungu Wafanyabiashara/Mawakala wasio na dola wala jeshi bali alipigana na Wazungu wenye dola na jeshi lenye silaha za kisasa!!
Kwamba,
Bila kufa mapema Chief Mirambo huenda mpaka sasa Afrika mashariki ingekuwa nchi moja.
Kifupi Mirambo alikuwa mpingaji wa biashara ya watu. Mzungu sio tu kulipa kodi kwa wananchi wa Mirambo, alikuwa akifanya fyoo mali zote zinachukuliwa na Mirambo.
Man, sio kwamba tunawasujudia Wazungu lakini uhalisia sio rahisi kama unavyodhani! Kudai kwamba endapo asingekufa mapema huenda bado Afrika Mashariki ingekuwa moja unamaanisha Mirambo angewashinda Wajerumani kivita!!!
Yaani unatuambia Mirambo aliyekuwa anatumia mikuki na pinde angeweza kumshinda Mjerumani ambae hadi anaingia Tanganyika, tayari alikuwa ameshafanya uvumbuzi wa mambo mengi tu huko kwao ikiwa ni pamoja na treni ya umeme?!
Hicho ni kichekesho!
Kwamba eti kuna Mtemi mmoja kutoka Afrika Kusini alitaka kuja kupigana na Mirambo ili achukue himaya yake, hicho ni kiroja kwa sababu hai-make sense Chifu avuke nchi kadhaa zilizopo Kusini mwa Afrika hadi aingine Tanzania ya leo, kisha aendelee kuvuka milima na mabonde hadi central Tanzania eti ili akapigane na Mirambo ili apore Dola la Mirambo!!
Ukweli ni kwamba, Mtemi unayemsema hakutoka South Africa ili kwenda kupambana na Mirambo bali alikuwa ni Kiongozi wa Wangoni ambao mwanzoni walitoka South Africa baada ya kushindwa vita, na hivyo wakatimuliwa!! Kundi la Wangoni lililokuwa linaongozwa na Zwangendaba ndilo lilivuka milima na mabonde na kuingia Tanzania!
Kundi hili liligawanyika, na moja wapo likaongozwa na Mpangalala na ndilo liliingia hadi Kanda ya Ziwa. Kabla ya kuingia Tabora, walianzia Usukumani, na Tabora walianza kupigana na Dola Dogo lililokuwa chini ya Dola ya Unyamwezi!
Dola hili dogolilikuwa chini ya Mtoto wa Chifu Fundikila ambae alikuwa ameolewa na mtoto wa Tippu Tip! Nadhani kwa mara ya kwanza baada ya kushinda vita kadhaa huko nyuma, hapa Wangoni walikula kichapo kichapo, possibly kutokana na huyo Binti kuungwa mkono na Waarabu!!
Baada ya kukimbia Kichapo huko Unyamwezini, ndipo Mpangala na watu wake wakaingia Urambo iliyokuwa inaongozwa na BABA YAKE Mtemi Mirambo na sio Mtemi Mirambo!!! Hapa napo Wangoni wa Mpangala wakachezea kichapo lakini walifanikiwa kutoroka mateka kadhaa including huyo Mirambo ambae by the time alikuwa just a boy!
Aidha, kumbukumbu zinaonesha kwamba, ni hawa Wangoni ndio ambao walimfundisha Mirambo mbinu za Kivita wakati akiwa mateka wao, na ndio maana hata pale Mirambo alipotwaa madaraka, jeshi lake lilikuwa linafahamika kama Warugaruga lenye asili ya Wangoni.
Na hata hiyo unayosema eti hao jamaa walichapwa wakaamua kuomba poo na kuungana nao, kimsingi hawa walikuwa Washirika wenye common interest dhidi ya Waarabu ambao hapo kabla walimsaidia mtoto wa Fundikira kupigana na Wangoni; na ni Waarabu hao hao ambao mara kwa mara walikuwa wanakwaruzana na Mirambo kugombea umiliki wa trading route!