Mtemi Mirambo VS Mtemi Mkwawa

Mtemi Mirambo VS Mtemi Mkwawa

Umekuza sana story za Mtemi Mirambo.

Jamaa alikuwa mtemi wa kawaida sana, ila alikuwa anajimwambafai kama Magufuli.

Hivi unajua Mirambo ndio mtemi maarufu aliyekuwa akipenda hongo?

Hivi unajua Mtemi Mirambo alikuwa mfanyabiashara maarufu wa watumwa kwa huku bara?

Hivi unajua Mtemi Mirambo alikuwa mtemi aliyekuwa na mikataba mingi zaidi ya kibiashara za kilaghai ambayo alifanya na waarabu, wajerumani.

Kuhusu Mtemi Mkwawa hiyo ni level nyingine kabisa. Misimamo yake isiyoyumba, nidhamu ya askari wake na mbinu za medani za kivita alizokuwa nazo, mpaka leo hii wajerumani wanampigia saluti.

Kama hujui tu, Mkwawa aliwachinja mpaka wamisionari wa kizungu waliofika kwenye himaya yake ambao kiasili walikuwa hawaguswi maana enzi zile walionekana kama wajumbe wa amani (malaika!).
Toa mkeka boss ututoe tongotongo
 
Toa mkeka boss ututoe tongotongo
Nyegge za utawala,milambo akaitaka tawala ya mjomba wake huko kahama,mjomba akamwambia dada "unamuona mwanao"!!..milambo akaitwa kwenye kikao Cha ukoo Cha upatanishi,palikua na nyama,kumbe nyama ya mbwa imefanyiwa utaalamu,alipokua tu,akasema mjomba umeniweza,tangu hapo akaanza kuugua,akiongoza mapigano toka kwenye hanga,mpaka alipokufa
 
Nyie paka,acheni kumfananisha MKWAWA na vitu vya kipuuzi visivyoeleweka..hivi mnajua kwanini makao makuu ya jeshi la ulinzi la Tanzania panaitwa LUGALO?
where in History ya nchi yetu mmeona kuna utukufu umetolewa kwa Mirambo?
Why Germans tooks MKWAWA SKULL?
ukipata majibu ya hayo mwaswali machache ambayo ni sensitive,basi utajijua ni kwa namna gani mleta mada ni kiazi na hasara kwa kabila na mji wake wa Tabora...anawadhalilisha wenzie huyu mpuuzi..
 
Hizo ni propaganda tu, hakukuwa na watu bogus katika bara hili kama hao machifu. Wao ndio waliofanikisha biashara haramu ya utumwa.

Wageni waliwatumia kukamilisha azma yao ya kupata watumwa na kwa hili hakuna chifu ambaye alisimama kupinga huu ufidhuli kwani machifu, sawa na watawala wa sasa wa kiafrika, walikuwa ni watu wenye tamaa sana ya utajiri.

Pia upotoshaji mwingine ni kuhusu kifo cha Mirambo, hakufa sijui kwa ugonjwa gani bali aliuwawa kwa sumu aliyowekewa kwenye chakula na moja ya shemeji zake kama sijakosea.
 
tuanzie hapa hivi vitabu vyetu vya historia viliandikwa wapi na nani walihusika , aalah kumbe ukiitwa mlugaluga si tusi bali ni shujaa/mjeshi
ooya walugaluga wa humu ndani mko poa?
hakuna jambo linanichefua kama kusoma historia eti mzungu kagundua mlima kilimanjaro mara sijui kagundua ziwa victoria uduwanzi tu kusema wenyeji wa hayo maeneo walikua hawajui kwamba hivo vitu vipo hapo na kwa majina yaani mpaka ziwa letu likapewa jina la malikia wa kizungu victoria bora hata lingeitwa mirambo.
 
Wewe bhana ni ama huifahamu historia ya Mtemi Mirambo au unaifahamu lakini unaamua kuipotosha kwa makusudi kama ilivyo ada yetu!!

Mosi, Machifu/Watemi wengi wa Kiafrika walikuwa ni wafanyabiashara ya Watumwa, na Mtemi Mirambo ni miongoni mwa Watemi ambao walibobea sana kwenye biashara hii!!

Pili, ni kweli Mtemi Mirambo alikuwa very powerful kijeshi na alitumia jeshi lake ku-block route kuu ya Msafara wa Watumwa kutoka Magharibi! Hata hivyo, hakufanya hii blocking kwa sababu alikuwa anapambana na biashara ya utumwa bali alikuwa analinda interests zake dhidi ya Wafanyabiashara wa Kiarabu!!

Umemshusha sana Mkwawa kuhusu uwezo wake kivita compared to Mirambo! Unafanya hivyo huku ukisahau au labda hujui kwamba Mkwawa alikuwa anapambana na Watawala (Wajerumani) wakati Mirambo vita zake nyingi kama sio zote zilikuwa ni dhidi ya Watawala wenzake wa Kiafrika au Wafanyabiashara wa Kiarabu!

Unlike Mkwawa, Mirambo hakuwahi kupigana na madola makubwa ya magharibi kwa sababu mwaka aliokufa ndio huo huo ambao Mabeberu walikutana kumegeana bara letu!!

Kwamba, unlike Mkwawa aliyekuwa na silaha duni kabla hajapewa bunduki moja na Mwarabu huku Mirambo akitengeneza bunduki hizo mwenyewe, hapo unaonesha upotoshaji wako mwingine ama kwa makusudi au kwa kutojua!!

Ukiisoma historia ya Mirambo wala hutachelewa kufahamu Mirambo kapewa sana bunduki na Wafanyabiashara wa Kizungu, na hivyo kuchangia sana kuwa na jeshi lenye nguvu!

Ni kumkosea heshima Mkwawa kudharau uwezo wake simply because alishindwa vita dhidi ya Mjerumani aliyekuwa sio tu Mtawala bali alikuwa na zana za kisasa za Kivita!! Mjerumani ambae hata leo bado ana uwezo wa kututwanga taifa zima let alone a portion of the country!

Aidha, nikukumbushe kwamba, hao ambao umesema "Hapakuwa na Wazungu wa kuleta fyoko"; nikifahamishe tu kwamba, hao hawakuwa Wazungu Watawala bali Wazungu Wafanyabiashara na Mawakala ambao hawakuwa na dola wala jeshi ndani ya ardhi yeu! Na ndio maana hata wewe mwenyewe unakiri kwamba:-

Huo ni ushahidi tosha kwamba hao Wazungu unaosema hawakuleta fyokofyoko ni Wazungu ambao hawakuwa na jeshi wala dola na ndio maana wakaomba msaada kwa Sultani...

Hawa sio Wazungu aliopambana nao Mkwawa unyemdharau ambae yeye alipambana na Wazungu wenye Jeshi la Kisasa na Dola!!

Mkwawa unayemdharau hakupigana na Wazungu Wafanyabiashara/Mawakala wasio na dola wala jeshi bali alipigana na Wazungu wenye dola na jeshi lenye silaha za kisasa!!

Kwamba,

Man, sio kwamba tunawasujudia Wazungu lakini uhalisia sio rahisi kama unavyodhani! Kudai kwamba endapo asingekufa mapema huenda bado Afrika Mashariki ingekuwa moja unamaanisha Mirambo angewashinda Wajerumani kivita!!!

Yaani unatuambia Mirambo aliyekuwa anatumia mikuki na pinde angeweza kumshinda Mjerumani ambae hadi anaingia Tanganyika, tayari alikuwa ameshafanya uvumbuzi wa mambo mengi tu huko kwao ikiwa ni pamoja na treni ya umeme?!

Hicho ni kichekesho!

Kwamba eti kuna Mtemi mmoja kutoka Afrika Kusini alitaka kuja kupigana na Mirambo ili achukue himaya yake, hicho ni kiroja kwa sababu hai-make sense Chifu avuke nchi kadhaa zilizopo Kusini mwa Afrika hadi aingine Tanzania ya leo, kisha aendelee kuvuka milima na mabonde hadi central Tanzania eti ili akapigane na Mirambo ili apore Dola la Mirambo!!

Ukweli ni kwamba, Mtemi unayemsema hakutoka South Africa ili kwenda kupambana na Mirambo bali alikuwa ni Kiongozi wa Wangoni ambao mwanzoni walitoka South Africa baada ya kushindwa vita, na hivyo wakatimuliwa!! Kundi la Wangoni lililokuwa linaongozwa na Zwangendaba ndilo lilivuka milima na mabonde na kuingia Tanzania!

Kundi hili liligawanyika, na moja wapo likaongozwa na Mpangalala na ndilo liliingia hadi Kanda ya Ziwa. Kabla ya kuingia Tabora, walianzia Usukumani, na Tabora walianza kupigana na Dola Dogo lililokuwa chini ya Dola ya Unyamwezi!

Dola hili dogolilikuwa chini ya Mtoto wa Chifu Fundikila ambae alikuwa ameolewa na mtoto wa Tippu Tip! Nadhani kwa mara ya kwanza baada ya kushinda vita kadhaa huko nyuma, hapa Wangoni walikula kichapo kichapo, possibly kutokana na huyo Binti kuungwa mkono na Waarabu!!

Baada ya kukimbia Kichapo huko Unyamwezini, ndipo Mpangala na watu wake wakaingia Urambo iliyokuwa inaongozwa na BABA YAKE Mtemi Mirambo na sio Mtemi Mirambo!!! Hapa napo Wangoni wa Mpangala wakachezea kichapo lakini walifanikiwa kutoroka mateka kadhaa including huyo Mirambo ambae by the time alikuwa just a boy!

Aidha, kumbukumbu zinaonesha kwamba, ni hawa Wangoni ndio ambao walimfundisha Mirambo mbinu za Kivita wakati akiwa mateka wao, na ndio maana hata pale Mirambo alipotwaa madaraka, jeshi lake lilikuwa linafahamika kama Warugaruga lenye asili ya Wangoni.

Na hata hiyo unayosema eti hao jamaa walichapwa wakaamua kuomba poo na kuungana nao, kimsingi hawa walikuwa Washirika wenye common interest dhidi ya Waarabu ambao hapo kabla walimsaidia mtoto wa Fundikira kupigana na Wangoni; na ni Waarabu hao hao ambao mara kwa mara walikuwa wanakwaruzana na Mirambo kugombea umiliki wa trading route!
Umeeleza vizuri sana
 
Kama hajui tu, waunguja wengi wa leo hapa Zanzibar, babu na bibi zao walikuwa wanyamwezi, waliuzwa na mtemi Mirambo. Asili ya sisi wazanzibar wengi ni unyamwezini (waunguja) na Uarabuni (wapemba...
Ni kweli ukiangalia tabora wapemba kwaaman ya waarabu Koko wako wengi
 
Ee kaka sasa unakimbia. Labda ulisikia jambo bila uhakika sasa huwezi kutuambia kitu tuende google?
Wanyakyusa wakati wa mwanzo wa ukoloni hawakuwa na nguvu maana walikuwa na machifu wadogowadogo tu. Merere wa Usangu aliwavamia bado mwaka 1892 akapora mifugo na wanawake.
Wajerumani walifika baada ya 1890 tu, maana walianza utawala pwani walipopambana an Abushri na baadaye na Wahehe. Hapakuwa njia hadi Tukuyu kenye nchi kavu. Wamisionari wa kwanza walifika 1891 kupitia Ziwa Nyasa.
Hali halisi eneo lilikuwa nje ya upeo wautawla wa kikoloni kwa miaka, na mwaka 1900 tu serikali ya koloni iliunda kituo cha utawala Neu Langenburg (leo Tukuyu) bila mapigano, baadaye walianzisha kituo cha kijeshi Masoko ambo waliweka kombania moja, lakini hapakuwa na mapigano.
Je vita yako ilitokea wapi na lini?
Mmmh!Msumari huo.
 
Milambo alikuwa genius. Alimwacha mbali Babu yangu Mkwawa linapokuja suala la ubora wa jeshi na uongozi
 
Kama hujui tu, Mkwawa aliwachinja mpaka wamisionari wa kizungu waliofika kwenye himaya yake ambao kiasili walikuwa hawaguswi maana enzi zile walionekana kama wajumbe wa amani (malaika!).
Hii ni sifa ya kipumbavu! Yaani anaenda kuchinja watu wasiokuwa na silaha halafu unamsifia? Mwenzake Chief Mirambo alifika level ya kukusanya kodi na ndiye alikuwa Chief tajiri kuliko wote wakati wa Tanganyika!
 
NI UKWELI MTUPU


Mirambo: the Black Napoleon​

On May 5, 2014 By Dr. Y.In Great Civilizations, Great Moments, Great People
View attachment 3089850
Mirambo, towards the end of his life
Mirambo, towards the end of his life
Today, I will talk about Mirambo, the man the explorer Henry Morton Stanley first referred to as a bandit, and later on as the Napoleon of Africa for his military prowess. Who was Mirambo?

Born Mbula Mtelya, Mirambo is the man who revolutionized nineteenth century Tanzania, and made it hard for the Germans to conquer the region: he united the numerous Nyamwezi tribes, and gained control over Swahili-Arab trade routes. Mirambo was the leader of the Nyamwezi people on a 200,000 km2 territory south of Lake Nyanza (Lake Victoria), and east of Lake Tanganyika. He was not a vulgar chief of brigands as the Arab traders made Stanley believe in 1871, but his links to different families of Ntemi (kings) were a little bit blurred as many historians had mixed up dynastic and genealogical lineages, different in a matrilineal system such as that of the Nyamwezis. In 1858, Mirambo managed to inherit the chiefdom of Uyowa from his father, Kasanda, who was a renowned warrior; he was only 18 years old. In 1860, he joined two chiefdoms located 100 km west of Tabora, in the kingdom of Unyanyembe. He learned the Ngoni language (Ngoni people trace their origin to the Zulu people of KwaZulu Natal), as well as their military techniques. Later in 1860, he conquered the neighboring territory of Ulyankuru.
Map of Mirambo's kingdom's kingdom
Map of Mirambo’s kingdom
He then moved his capital to Iseramagazi where he built a Boma, a fortified residence, with walls made up of dry bricks, retrenchments and hedges of euphorbia flowers. From his father and mother, he was a descendent of Mshimba (lion), the last ruler of the legendary kingdom of Usagali, and Mirambo was thus recreating the old empire. Thus in 1860, he created a new Nyamwezi state, the Urambo, from the name he had adopted for himself, ‘corpses‘ in kinyamwezi, Mirambo. From 1860 to 1870, he strengthened his authority along the banks of the river Gombe, i.e. on the road to Ujiji, thereby threatening to block the Arab commerce in the area. In 1871, he defeated the Arab traders at Tabora. The Sultan of Zanzibar, Barghash bin Said, retaliated by sending 3000 soldiers (2000 Swahili, and 1000 Balutchi). Mirambo’s resistance was one of the most fierce: Nyamwezi’s fighters would go as far as melting their copper bracelets to make bullets for their guns. A compromise was made to keep commerce flowing with the coast: caravans could pass after paying a tax (hongo) to Mirambo.

Every year, during the dry season, Mirambo would dispatch his ruga-ruga in all directions to continue the expansion of his territory. From 1876 to 1878, the territory was expanded to the north, up to the southern banks of Lake Victoria. From 1879 to 1881, expansion to the west toward Uvinza, for the control of Lake Tanganyika. The Muhambwe of King Ruhaga fell under Nyamwezi domination, and the Ruguru of King Ntare had to seek protection from Mirambo and agree to the presence of a ruga-ruga post on the eastern border of his kingdom. In 1879, there was also the expansion towards Burundi. His alliance with the Ngoni fell apart in the early 1880s. He was greatly hated by the Arabs who used to dominate the commerce in the region, and other neighboring kings who feared him, and the Europeans who saw in him as a powerful adversary. After 1881, the Arabs managed to convince the International African Association (AIA – Association Internationale Africaine), a European power created under King Leopold II’s initiative to inflict an embargo on arms and munitions on Mirambo (yup… European unions already inflicted embargo on arms back then). The goal of the AIA was to “open up central Africa to civilization.” At first Mirambo’s army succeeded in entering Burundi by surprise using a feud between the local king and his brother, but in 1884, his army was defeated by Burundi warriors (aided by Ngoni warriors). After his defeat in Burundi, and another defeat against the alliance of the Arabs and the Ntemi of Bukune, Mirambo’s troops were led by Mpandashalo as he was increasingly sick. Mirambo died on 2 December 1884.
Mirambo was a strong and ambitious leader. He expanded his authority and influence over a number of Nyamwezi chiefs. One of his challenges was to devise a political system that would allow him to consolidate his power, while ever expanding his territory. For that, he made sure not to change the structure of the Nyamwezi’s society: once in power, he would usually choose a successor from the same family. As long as the new chiefs pledged allegiance to him, they would be left to go about their political duties. The conquered chiefs had to provide troops at all times. His greatest strength was military. He used surprise as a tactical ploy. His capital was both a military and economic center. He had two residences: Iseramagazi from 1879, and Ikonongo from 1881.
Mirambo was actually a simple man, deeply rooted in his culture and traditions, but also very curious of the world. He was a man of order and progress, who will set the price of commodities in the capital’s markets, and regulated the consumption of alcohol in his kingdoms (he thought that alcohol weakened societies – just like Gungunyane), and meditated on the decadence of Africa in the 19th century. He was nostalgic of the magnificent ancient African capitals, and kingdoms. In essence, Mirambo had 4 faces: the traditional king, the warrior leader, the state builder, and the modernizer. To learn more, go to: ThinkAfricaPress.com, BlackPast.org, and Les Africains, Vol. 6, editions J.A, C.-A. Julien, P. 127-157, (1977).
Thank you.
 
Back
Top Bottom