Mtemi Ng'wanamalundi (Mwanamalundi) - Yesu wa Afrika?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
Nilikuwa Mwanza na nilitembelea wilaya za Magu na Sengerema. Huko nilikutana na ngoma za kina Ng'wana Ituli,wanacheza MBINA. Hii ni ngoma inayochezwa kipindi cha kiangazi baada ya mavuno.

Wanajivunia uchawi na nguvu za miujiza walizonazo,wanawataja mashujaa wao kuwa ni kina Ng'wana Malundi, Iwambangulu, na Mtemi kapela.

Wanajivunia maajabu aliyoyafanya Ng'wana Malundi, ikiwa ni pamoja na kutembea juu ya bahari kule Zanzibar, kukausha misitu kwa kidole.

Kwa kweli ni historia nzuri sana na ya kujivunia na kuvutia pia, lakini kwa bahati mbaya hamna sehemu zilipo andikwa, ni masimulizi ya midomoni kwa watu.

Kuna haja sasa wataalam wetu wa historia, waende huko Usukumani wakasiklie na kuandika.

Inasikitisha kuona taifa letu halithamini historia yake yenyewe.

========================


 
Hakuna hifadhi mahali alipokanyaga Ng'wanamalundi.

Wednesday, 13 July 2011 20:34
Na Charles Kayoka.

Kwa Watanzania wa umri wangu waliopata kusoma historian au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng'wanamalundi. Aliyezaliwa katika ukoo wa kiuganga na uchifu aliyehesabiwa kuwa ni mmoja ya watu wenye miujiza mingi.

Ng'wanamalundi anaelezewa kuwa na uwezo wa kufika mahali mbali kutoka nyumbani kwa muda mfupi, sijui alitumia nguvu gani? Aliweza kutibu watu kwa
uganga wake kwani alifahamika sana kwa hilo; na alikuwa anaweza kuvuka maji marefu kwa kuweka dawa na maji yakajitenga na yeye akapita.

Nilipokuwa ziarani wilayani Kahama hivi karibuni,nikifuatilia mahali alipofia Mtemi Mirambo wa Unyamwezini (nitaelezea habari zake katika moja ya makala zijazo), nikaambiwa "huko nilikotoka, kijiji cha Nyandekwa, kuna jiwe ambako Ng'wanamalundi alikuwa amelikanya na alama ya unyayo wake hadi leo uko.

Siku ya pili nikafunga safari hadi kijijini Nyandekwa, kiasi cha kilomita kumi kutoka makao makuu ya wilaya ya Kahama katika njia iendayo Urambo kupitia Uyogu.

Hapa nilipofika na wenzangu tukabahatika kukutana na kaka wa umri wa makamo aliyejitolea kutupeleka kwenye "jiwe" hilo.

Ni kiasi cha kilomita moja toka barabara ya Uyogu na hakuna barabara ya gari zaidi ya njia za wafugaji wa ng'ombe. Tukaifuata njia hiyo tukiwa ndani ya Landcruiser,maana sidhani kama unaweza ukaenda na gari dogo zaidi ya hilo likarudi salama, hasa kama mvua imenyesha.

Ninaeleza hivyo kwa sababu nilidhani hiki ni moja ya kivutio kikubwa sana cha kiutamaduni na historia na kingejengewa barabara ili watalii wa ndani na nje wangeweza kufika kutembelea.

Hapo ni mahali penye mwamba mkubwa wa jiwe. Tukaona watoto na akina mama wakianika nafaka kwenye jiwe hilo.

Tulipofika na kuwauliza kama wanajua habari za Ng'wamamalundi na uhusiano wake na jiwe lile walisema hawajui chochote, na mwingine alisema yeye ni
mgeni eneo lile.

Tulipanda mpaka juu na kuona alama tatu za nyayo za binadamu. Alama ya tatu imefutikafutika lakini mbili zilizobaki zilikuwa bado zinaonyesha vizuri. Moja
ilikuwa ndogo, kiongozi wetu alisema kuwa ile ndogo ilikuwa ya mke wa Ng'wanamalundi.

Na ingine iliyokuwa kubwa ilikuwa ndiyo ya Ng'wanamalundi mwenyewe. Na hadithi zinasema Ng'wanamalundi alikuwa na miguu mikubwa, huenda ndio sababu ya kuitwa Malundi- miundi- Miguu. Yaani mtu mwenye "mamiguu". Alama ya unyayo huu ilikuwa kubwa, na ilikuwa na alama ya kukatwa katikati.

Tuliambiwa kuwa ni mkewe ndiye aliyeikata ile lama, hatukuelezwa ni kwa kusudi gani. Lakini fikiria binadamu kuwa na uwezo wa kukanyaga kwenye jiwe na kuweka alama iliyodumu kwa zaidi ya miaka sabini.

Pembeni yake palikuwa na jiwe la mviringo ambalo huwezi kulinyanyua, labda uwe na nguvu za Ng'wanamalundi mwenyewe. Jiwe hili lilikuwa na mashimo yaliyokuwa katika mistari iliyonyooka na nilipochunguza nilihisi kuwa ni mashimo ya kuchezea bao,ule mchezo wa kienyeji unaochezwa na watu wawili hadi wanne kwa kutumiamawe kwenye mashimo.

Niliona kuwa kulikuwa na mashimo ya kutosheleza watu wanne kucheza- yaani mabao mawili.

Tulielezwa kuwa hapo ndipo Ng'wanamalundi alipopenda kucheza bao na rafiki zake. Alitengeneza lile bao kwa kufinya mkono wake wenye nguvu za ajabu
kwenye lile jiwe na mashimo kutokezea.

(Hii sio hadithi ya kwanza kusikia, hata huko milima ya Uluguru kuna mahali ambapo Chifu Kingalu na wenzake walikuwa wakishindana kuonyeshana nguvu za uchawi KWA kutengeneza mashimo ya bao kwenye mawe kwa kutumia visigino vya miguu.

Moja ya bao hilo liko hadi leo pembeni ya mto huko milimani- Morogoro- picha ninazo). Na wengi kule Kahama wanasema kuwa mashimo kama hayo ya
Ng'wanamalundi aliyatengeneza sehemu nyingine nyingi, maeneo ya Shinyanga na Mwanza.

Mahali hapo pamesahaulika, huenda kwa waganga wachache wanapopakumbuka hapo kwa ajili ya matambiko yao. Lakini hakuna ulinzi, hakuna kumbukumbu, na miguu hii ya Ng'wanamalundi na mkewe inafutika kutokana na upepo, mchanga, jiwe kutumika na binadamu na mvua.

Huu ni utalii wa kihistoria lakini hautumiwi. Wiki ijayo tutazungumzia jiwe la "nyasaolo"katika kijiji cha Busolo, ambako ukifanya tambiko na kuliomba likatikisika ujue maombi yako yamekubalika.

utaliiupdate@gmail.com , 0766959349
 
Kiranja na wewe tafuta story nyingine za Ng'wanamalundi ili tuzihifadhi tusishupalie tu kulaumu wakati sisi wenyewe hatujafanya effort yeyote.
 
Kuna maelezo mengi sana ya uchawi. Lakini uchawi ambao umekuja kujulikana duniani kwa jinsi dunia yenyewe ilivyo,umekuwa ukibadilika kimwelekeo lakini kimsingi sayansi hii ambayo kwa miaka mingi hufundishwa kwa siri na wanaojua kwa wanaotaka kuijua na wakati mwingine kurithisha, ni ada ya wanadamu wengi hasa katika Bara la Afrika. Wale wasomi hukataa na kukana uwapo wake, wanaikataa dhana yenyewe na wanasema kwamba si kitu kujadili na mgeuko wake ni fikra za dini tulizonazo za Kiislamu na Kikristo ambazo zinatambua uwapo wake na kusema ni kazi ya shetani na matumizi mabaya ya maarifa ambayo ni nadra kila mtu kuyajua.

Unaweza kujua vitu au kitu kinachoitwa uchawi kutokana na mambo kadhaa hasa yaliyoandikwa au kufanyiwa masimulizi katika vitabu mbalimbali vikiwamo vya Kurani na Biblia. Kila mwaka wenzetu wa Haiti,vitukuu na vilembwe vya waliofikishwa utumwani hufanya tamasha kubwa la wachawi, wao wana dini yao ambayo ni ya kuabudu kitu wanachoita voodoo. Watu hawa wanachofanya kwa wengine ni uchawi lakini kwao ni imani kali ya kujisalimisha kwa roho mbalimbali zisizoonekana ambazo ndizo wanazodai kuwatawala. Nadharia na suala zima la uchawi limezungumziwa na kujadiliwa tena na tena na watu mbalimbali na kwa namna mbalimbali. Lakini taabu kubwa ni tafsiri ya uchawi. Hivi unawezaje kuuzungumzia uchawi ukasahau wanga na ganga, upo wakati uchawi , uganga na wanga huwa ni kitu kimoja kwa wengi wetu.

Uchawi umewekwa katika dhana kwamba watumiaji na waathirika ni washenzi lakini kama utakuwa umesikiliza gumzo la Ng'wanamalundi ipo tafsiri ndani ya waungwana kuhusiana na shauri hili na kusema kwamba uchawi unawahusu watu washenzi, kidogo inapoteza ukweli wa mambo. Katika filamu ya Ng'wanamalundi, mchawi aliyewakilisha kundi la wachawi alisema yale ni maarifa na ufundi wa kufanya mambo, sasa kama washenzi wanayapata maarifa haya sijui inakuwaje hasa. Lakini tafsiri ya karibu kabisa ya watu kuhusu uchawi na hata katika makamusi yetu ni matumizi mabaya ya maarifa
aliyonayo mtu kudhuru mtu mwingine au mali zake. Kamusi ya Kiswahili sanifu inasema kwamba uchawi ni ufundi wa kutumia dawa, aghalabu mitishamba na vitabu maalumu vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe. Katika hili ni wazi siri ndio jawabu la maana la maana ya uchawi , ufundi wa kuleta madhara.mwanga kwa upande wake ni mcheza mahepe afanyaye mazingaombwe ya kichawi usiku.

Ni tatizo sana kuzungumzia uchawi kama sihiri lakini shauri la kusema watu washenzi yaani wasiostaarabika ni kasheshe kubwa kwani wapo wachawi wanaoendelea na matajiri wakubwa wakiabudu uchawi kama chanzo kikuu cha utajiri wao, sasa nini hasa kipimo cha uchawi? Uchawi huu ambao huathiri viumbe kuna wakati hutumika kwa manufaa makubwa, ikiwa ni pamoja na kuzuia uharibifu mkubwa wa madhara ya uchawi katika jamii kwa kuwapo na mtu anayedhibiti wachawi wadogo na kuwaumbua.

Zipo nadharia zinazozungumza shauri zima la uchawi na Profesa Haward Safari katika mada yake ya uchawi katika Riwaya za Kiswahili mwaka 1993, alizungumzia shauri zima la uchawi na ushahidi wake. Alikuwa anazungumza katika mkeka mkubwa na waandishi wa vitabu, UWAVITA, na mfano wake wa bomu na nyutroni unaweza kukuweka hoi. Ni kweli kuwa utaalamu wa kutengeneza bomu hili ni siri kubwa na wataalamu wake wanalindwa sana, kwa hiyo kama shauri hili la ufundi na usiri ni uchawi basi nyutroni ni uchawi na umetengenezwa kwa minajili ya kudhuru binadamu. Imani za kiuchawi ambazo zimekumba nchi yetu kwa kasi, ipo pia katika Bara la Afrika na Ulaya ambako ndiko inakoaminika imeanzia katika karne za kati.

Hapa nchini vipo vitabu vingi vinazungumzia dhana hiyo katika mifumo mbalimbali ingawa vinavyoeleza kwa lugha ya kukua sana ni kama Mirathi ya Hatari kwa upande wa hadithi za kubuni, hadithi za dini hasa hadithi ya taaluma ya uchawi , Maalim Kisisina na ile ya Mussa na Wachawi wa Farao katika Biblia. Katika simulizi la Maalim Kisisina, inaelezwa kulizuka matatizo makubwa wakati wa kunyang'anyana kitabu cha uchawi kati ya Jibril na maalim huyo na mwishoni Jibril alimwachia maalim huyo kitabu na ndio uchawi uliopo sasa duniani. Hadithi ya maalim huyu ipo katika Kurani na Biblia, kwa namna yake imezungumzia shauri la Musa na wachawi wa Farao ambao nao waliweza kugeuza fimbo zao kuwa kama nyoka kwa jinsi Musa alivyoweza. Kama kwa Jibril, Musa naye alionyesha ukuu wa uchawi dhidi ya shauri la Mungu na Mungu kuonekana kuwa mkubwa wa yote, fimbo ya Musa iliwalamba nyoka wale wa Farao. Mashauri ya uchawi yapo hata Ulaya. Nchi kama Uingereza na Ujerumani ndizo zinazoongozwa kwa masimulizi ya uchawi kwa kuungama kwa wahusika. Kimsingi uchawi ni sanaa ambayo ipo katika kila mahali na ina vitisho vikubwa.

Siku za karibuni kumezuka mganga anayejulikana kwa jina la Manyaunyau ambaye anatoa vitu vinavyoitwa vya kichawi na watu wanashukuru kwa kufanyiwa hivyo. Watu katika hekaheka hizo wanaokumbwa na mikasa ya kunaswa katika anga za mganga Manyaunyau, wanazungumzia ndege zao wanazosafiria nyingine zikiwa na uwezo wa kubeba hadi abiria 16 (sawa na Cessna), kitu kinachoitwa mwanga chenye jicho moja kama kilichodaiwa kudakwa huko Kimara King'ongo ambacho kilifanyiwa hila ya kunaswa. Si Kimara tu maeneo mengi ya Dar es Salaam yana matatizo hayo kukiwa na
historia ya kitaifa ya uganga na ulozi. Mathalani watu wengi hawatasahau

Mandondo wa Korogwe, Tekelo wa Dar es salaam, Kabwere wa Tanga, hao walikuwa waganga maarufu wa kufichua wachawi bila kumsahau mganga Kalembwana wa Malinyi. Katika mtafaruku huo kuna mafuvu, vyungu vya kupikia nyama za watu, mikono ya biashara ya watu waliokufa ilipatikana.

Kuna sababu nyingi za uchawi lakini nyingi ni za kiuchumi zaidi hasa kupata msukule, mifugo, mavuno na kimantiki majina haya ya msukule, ndondocha na kizuu yanaashiria mambo yaliyopo katika jamii na yote haya ni mashauri ya kiuchumi. Kuna mauaji yanafanyika katika Nyanda za Juu na Kanda ya Ziwa, siri kubwa ni uchumi watu wanataka kupatiwa utajiri kwa kuchanganya dawa na sehemu za mtu aliyeuawa. Maiti zinazokatwa sehemu za siri zinadaiwa kufanywa hivyo kuvutia biashara, kwa hiyo shauri la kiuchumi husababisha kukomaa kwa imani hizi za kishirikina. Sifa na ujasiri ni sababu nyingine ya kichawi huku starehe ikiwa ni ya mwisho.

Yapo maelezo kwamba wachawi wanatumia uchawi kuwafanyia fidhuli watu, kula nyama zao, kucheza uchi usiku na watu huwapora wake wenzao kwa kuthubutu kuua waume zao. Uchawi ni sehemu ya utamaduni na inaonekana wazi uchawi hustawi zaidi katika umasikini. Kinjeketile alitumia uchawi kuhamasisha watu kupambana na Wakoloni je kwanini leo wachawi wasitumie kuleta maendeleo kwa jamii? Hii taaluma yao ya kuingia maeneo bila kujulikana, kuruka na taaluma nyingine nyingi walizonazo, ni kwa nini wasiwafundishe watu bila kificho?
 
Mi kama ngosha the don nimeipenda hii story,pia mama yake huyu mwanamalundi alikuwa na kishoka fulani,mwanae i.e Mwanamalundi kadiri anavyozidi kusafiri kwenda mbali,kile kishoka ambacho huning'inizwa ukutani,hupanda juu taratibu,akifika sehemu kupumzika,kile kishoka kina tulia,akianza safari kurudi kile kishoka kinashuka chini.Kile kishoka kikifika chini kabisa,mamake mwanamalundi anajua mwanae tayari yupo nje ya nyumba yake!
 
Huyu jamaa(ng'wanamalundi),siku alipokufa ilikuwa mchana wa kawaida tu lakini jua lilipotea kwa dakika kadhaa na kikatokea kiza totoro,wanyama watembeao usiku kama fisi wakaanza kupiga misele kama kawa,kuku wakaingia ndani,baada ya kitambo kidogo mwanga wa jua ulirejea.
 
kuna kitabu kuhusu historia ya Ng'wana malundi nilikisoma long time. Kinaelezea mambo yake huyu jamaa aliwatesa sana wajerumani walimsafirisha hadi ng'wani (pwani) lkn walimrudisha sababu ya viroja na wakati anaondoka alimwacchia mama yake maziwa na kumwambia kuwa maziwa yakiganda wajue kuwa amekufa na hayakuganda kwa muda wa mwaka na nusu. Nafkiri historia ya extra ordinary people ktk afrika ilipotoshwa na wazungu hasa wabritish kwa makusudi ili kujenga jamii ya inferior africans, hata historia ya Kinjekitile na uwezo wake wa ajabu hasa kufuga wanyama wa aina zote na habari za vita vya maji maji imepotoshwa sana. Mungu akinisaidia napenda sana niandike kitabu kuhusu ''pre-colonial tanganyika mighty men and women''ni mengi ya msingi yapo. Anyway hicho kitabu cha ng'wana malundi kipo nyumbani kwa dingi yangu nikienda ntajaribu kumuomba atleast nikiscan nikiweke huku coz he's very strict about his books. As historian kuna mengi nimeona na kusikia kuhusu jamii yetu ambayo vizazi vyetu vinahitaji kusikia
 
Nazjaz

Ahsante Nazjaz kwa kuleta hii kitu. Na ahsante kwa original author kwa article hii
 
Last edited by a moderator:

Pia pale mwaloni mwanza kwenye kivuko cha kamanga ferry penye mwamba wa bismarck kuna fito (pegs) ambazo inasemekana zilingongelewa na mwana malundi. Nani anaweza gonga fito katika jiwe na zikaingia bila mwamba huo kupasuka? Ni maajabu aisee
 

Naona hujafanya utafiti vizuri kujua haya mambo kama yameandikwa ama la!

Habari za Mwanamalundi tulizisoma siku nyingi sana miaka ya '70 ama '80 hivi kulikuwa na kitabu kidogo kwa jina la Mwanamalundi: Mtu Maarufu Katika Historia ya Usukuma.

Huyu Bwana hakuwa Mtemi kama unavyotaka kutuelezea isipokuwa alikuwa mcheza ngoma za Kisukuma (Wighashe) na uganga huo aliupata kwa bibi mmoja huko huko Usukumani. Masimulizi yalikuwa yanasema hivi aliondoka na vijana wenzake watatu kwenda kutafuta huo uganga lakini ni yeye tu aliyeshinda vimbwanga vya bibi huyo aliyejigeuza kuwa faru na wenzake wakatimua mbio.

Kama maktaba zet ziko makini hiki kitabu unaweza kukikuta kwenye archives zao! Maana enzi hizo za mwalimu vitabu hivi vilikuwa vinapatikana kwenye maktaba za shule za msingi. Au ukipata tena nafasi ya kwenda Mwanza jaribu pale Bujora (Kisesa - Magu) kwenye makumbusho ya Wasukuma. Hapo utapata mambo mengi sana watu maarufu katika historia za Usukumani (akina Ibamba Ngulu, Kapela, Nkanda, Gindu Nkima - huyu ndo alikuwa mpinzani mkubwa wa Mwanamalundi kwenye ngoma za Kisukuman.k)

Ukikipata kitabu hicho cha Mwanamalundi yote yameandikwa humo na jinsi alivyowasumbua wale askari waliokuja kumkamata na kumpeleka Gerezani kule Tabora na baadaye Zanzibar wakifikiri wamemkomesha kiasi kwamba hatarudi tena bara mpaka kifo. Lakini miujiza aliyokuwa anaifanya alikuwa anavuka bahari mpaka Dar kwa miguu mpaka mwisho wake wakaamua kumwachia.
 
Kuna story nyingi sana inawezekana pande zote za nchi. Huyu kiranja mkuu asingepita hiyo njia akanyoosha njia halisi ya kwenda Tabora kuna historia kuwa ilikuwa ni railline kutoka kahama hadi Tabora lakini hakuna evidence yoyote ya uwepo reli hiyo. Anyway back to the matter hiyo njia inatoka Kahama unanyoosha Nyihogo, Mhungula, wewe huyo Kiiza, Kilago hapo ndio kuna junction ya kwenda huko Nyandekwa zote ni barabara za gari ila hazina tarmac.

Sasa usingeenda huko Nyandekwa ukanyoosha hadi Tulole kwa mbele kidogo tu ukiendelea na hiyo barabara kuna mlima unaitwa KUNDIKILI. Hapo kuna jiwe lilikuwa kama pango sasa historia ni hivi kulikuwa na wa harusi vijana wakitembea toka kijiji kimoja hadi kingine. Walipofika mlimani hapo mvua kubwa ilianza kunyesha wakaamua kuji banza kwenye hilo pango.

Historia inasema liliwafunika lakini bado wapo hai inasemekana. Ukipita hapo baadhi ya siku unasikia watu wanaongea kwenye hilo pango. Historians mnaweza kwenda kuonana na wenyeji hapo then mtapata data.

Ila maajabu yapo sehemu nyingi lakini kuyatunza katika maandishi ndio issue ukizingatia tuna struggle kula, umeme hakuna, foleni muda wote, ukiandika vitabu huwezi kuishi kwa hilo, ukiachia distraction nyingi mara ufisadi na zingine.
 
tunahitaji na utamaduni wa hawa watu...wadumishajo wa mila MASAI.

Kule kigoma vijijini Kibondo kuna kijiji maarufu Makere ushingo...mbona ulikua mtu unaenda kuununua urozi tu. Na hapo hapo unafanya majaribio! Hizo zote ni hazina tunazo lakini wazungu walivyo wajanja wakaleta dhana zao na misaada yao ili watu wachukie maarifa yao...sasa vitu hivyo kwishneiii!

Hata mabwawa ya mvua tunashindwa kuyajaza kwa karama za babu zetu. Mimea na ukame kibao. Tumerogwa sana na hawa wazungu lakin hatujawajua .

Aibu kubwa sana. Hii ni uchawi mimi naona inafaa sana tena waipe kipau mbele mashindano mara kwa mara yafanyike ili tuwapate wataalam wakubwa. Bado tunahitaji hizi taaluma sio kuwadanganya watu eti uchawi unafanywa na wasio akili au maskini....nani anawadanganya? Wafalme zamani au ili kiongozi lazima uwe mtaalam ndio unaupata uongozi. Halafu kama hamjui maana ya MAgick = wiseman.

Tubadilike na tukubali mambo ni mengi tunayasahau na kuyadharau ajili ya kupewa pewa vijizawadi vya magari ya fahari na mambo mengine kwa mashart mabaya . Inaniuma sana!!!
 
Njia ya kuelekea Musoma ukitokea Mwanza kuna kitongoji ambacho jina silikumbuki lakini kutoka barabarani unaweza kuona alama za unyayo wa huyu Bwana kwenye jiwe. Yumkini alikuwa mtu wa ajabu. Kuna vitabu vinaelezea historia yake.

Tiba
 
Njia ya kuelekea Musoma ukitokea Mwanza kuna kitongoji ambacho jina silikumbuki lakini kutoka barabarani unaweza kuona alama za unyayo wa huyu Bwana kwenye jiwe. Yumkini alikuwa mtu wa ajabu. Kuna vitabu vinaelezea historia yake.Tiba
Pale Tabora kuna kitongoji kinaitwa Itobo, kuna unyao wa Mwanamalundi na mbwa wake kwenye jiwe kubwa, wenyewe wanaita Itare.
 
Hivi alifariki mwaka gani? Na nini chanzo cha kifo chake? Je kaburi lake liko wapi? Au naye alichukuliwa na gari la moto linalovutwa na farasi kama nabii Elia Mtishibi?
 

Ni kweli mkuu ulichokisema hata mimi hicho kitabu nilikisoma miaka ya mwanzo ya tisini na kama ulivyoelekeza akienda Bujora lazima atakipata.

Hata hivyo usukumani kuna simulizi za watu wengi sana zaidi ya Ng'wanaMalundi. Kuna simulizi za watu wengine kama Ng'wanagasasala, Samike, na kuna mwingine nimemsahau jina alikuwa na uwezo wa kuruhusu mwili wake ujae na kufiti chumba, kuna simulizi zingine za visima kuwa na uwezo wa kumeza watu na kuwatoa baada ya siku kadhaa wakiwa hai, simulizi za maajabu ni nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…