Nilikuwa Mwanza na nilitembelea wilaya za Magu na Sengerema. Huko nilikutana na ngoma za kina Ng'wana Ituli,wanacheza MBINA. Hii ni ngoma inayochezwa kipindi cha kiangazi baada ya mavuno.
Wanajivunia uchawi na nguvu za miujiza walizonazo,wanawataja mashujaa wao kuwa ni kina Ng'wana Malundi, Iwambangulu, na Mtemi kapela.
Wanajivunia maajabu aliyoyafanya Ng'wana Malundi, ikiwa ni pamoja na kutembea juu ya bahari kule Zanzibar, kukausha misitu kwa kidole.
Kwa kweli ni historia nzuri sana na ya kujivunia na kuvutia pia, lakini kwa bahati mbaya hamna sehemu zilipo andikwa, ni masimulizi ya midomoni kwa watu.
Kuna haja sasa wataalam wetu wa historia, waende huko Usukumani wakasiklie na kuandika.
Inasikitisha kuona taifa letu halithamini historia yake yenyewe.
========================