Alifariki miaka ya 1940's sikumbuki mwaka exactly hata ugonjwa wake sikumbuki kutokana na hicho kitabu, alizikwa kwao ambayo kwa sasa ni eneo la wilaya ya Kwimba-Mwanza, na inasemekena baada ya Mazishi yake kulikuwa na manyunyu na yalivyokatika moshi ukawa unatoka kwenye kaburi lake watu wakajiridhisha kwamba Ng'wanamalundi kaenda mbinguni.Hivi alifariki mwaka gani? Na nini chanzo cha kifo chake? Je kaburi lake liko wapi? Au naye alichukuliwa na gari la moto linalovutwa na farasi kama nabii Elia Mtishibi?
Alishitakiwa kwa kosa la kuua watu pamoja na mifugo na mazao ya watu, kulikuwa na mashindano ya ngoma (mbina) wakati mashindano yanaendelea wakaja wasaidizi wake waliokuwa wanashughulika na kupika na kumwambia hawakuwa na kuni sasa yeye alichofanya ni kunyanyua mkono kuelekea upande kulikokuwa na miti na kuamrisha umagi pye abing'we akiwa na maana vyote vilivyokuwa upande kule alikoelekeza mkono wake vikauke ili wapate kuni, badala ya miti pekee kukauka kila kitu kilichokuwa upande ule kilikauka.