Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
WanaJF, kuna watu maarufu waliowahi kuvuma katika historia za bara letu, na mmojwapo ni huyu MWANAMALUNDI kutoka kabila la wasukuma. Niliwahi kusoma kitabu kilichokuwa kinaelezea historia yake kwa ufupi na maajabu aliyowahi kufanya wakati wa uhai. Moja ya maajabu ni pamoja na kupona wagonjwa, kupita katikati ya ziwa huku maji yakiacha njia, kuacha nyao zake kwenye mawe, kukausha miti kwa ajili ya kuni nk.
Nimekuwa nikijiuliza sana, maajabu/uwezo aliokuwa nao huyu MWANAMALUNDI si ndiyo ule ule aliokuwa nao Bwana YESU kristo? Basi kama ni kweli, MWANAMALUNDI ndiye haswa YESU WA AFRIKA. Kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo, wazee wetu hawakuweza kujiandikia mambo mengi kuhusu huyu bwana na pengine leo hii tungekuwa hatumuabudu YESU bali angekuwa ni huyu yesu wetu MWANAMALUNDI.
WanaJF, mwenye kitabu au historia zaidi au maoni zaidi kuhusu MWANALUNDI na maisha yake, amwage hapa ili tuweze kuelimishana.
Mkuu Baba V, fuatilia comments za wadau utapata kitu si bure. Pengine unaweza ukawa na jibu zuriiii.Kwa nini umfananishe NG'WANAMALUNDI na yesu, mwache yesu abaki kuwa yesu na ng'wanamalundi abaki kuwa yeye. usijaribu kuwalinganisha
Hilo ndilo neno haswaaa, ukienda Asia na maeneo mengine ya karibu karibu kama Australia, wanaimani zao pamoja na baadhi ya watu kukubali masimulizi ya wazee wa kiyahudi lakini bado kundi kubwa linaamini katika tamaduni zao, dini, mila na desturi zao. Na hata utakuta kuna maeneo mengi ya yenye kumbukumbu nyingi za tamaduni zao, hawazitupi wala kuchoma moto, watu wanazisoma na kuhitimu. Kuna mambo mengi sana ambayo sisi bado tunayaona ni mambo ya ajabu kumbe ni lulu, ni neema kwa vizazi vijavyo. Siku hizi watoto badala ya kukaa chini na mabibi au mababu wapate hadithi za kale na simulizi kuhusu tamaduni za koo zao au kabila zao, wanakalishwa kwenye TV na kuangalia Cartoons au mieleka (a 5 years old kid watching cartoon or restling). Ni mambo mengi, ila kwa kuanza tu ni hii ya historia ya MWANAMALUNDI.hakuna kitu kitu kibaya kama kujidharau sasa hawajamaa walichofanya ni kuwafanya waafrika wajidharau na kujiona hawaposahihi kwenye yale wanayoyafanya katika maisha yao..
RIP watemi wote wa kiafrika
Kwa nini umfananishe NG'WANAMALUNDI na yesu, mwache yesu abaki kuwa yesu na ng'wanamalundi abaki kuwa yeye. usijaribu kuwalinganisha
Kwenye hiyo njia uliyotaja hamna kitu kama hicho mkuu, labda kuna makumbusho ya Bujora ambapo unaweza kupata historia yake.
Alama za nyayo zake nadhan zinaweza kupatikana wilaya za Kwimba, Maswa, Sengerema labda na Geita au Kahama.
Missionaries brought the Bible.They ordered us to close our eyes for prayers. When we opened our eyes, they had grabbed all our fertile land, taken our minerals and in return left us with the Bible. Nenda Ulaya, brothers, you will be surprised there are some families that has never had the name JESUS!!!
Mkuu Baba V, fuatilia comments za wadau utapata kitu si bure. Pengine unaweza ukawa na jibu zuriiii.
ilitabiliwa kuwa siku za mwisho kutatokea wapinga kristo wengi sana,na haya twayaona sasa
naona watu wanataka kujifunza ''uchawi'