Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,205
- 33,287
siku moja bana mwanamalundi alikua kwenye mkutano watu wengi wamekusanyika kusikiliza kitu wenyewe wanaita mbina.WanaJF, kuna watu maarufu waliowahi kuvuma katika historia za bara letu, na mmojwapo ni huyu MWANAMALUNDI kutoka kabila la wasukuma. Niliwahi kusoma kitabu kilichokuwa kinaelezea historia yake kwa ufupi na maajabu aliyowahi kufanya wakati wa uhai. Moja ya maajabu ni pamoja na kupona wagonjwa, kupita katikati ya ziwa huku maji yakiacha njia, kuacha nyao zake kwenye mawe, kukausha miti kwa ajili ya kuni nk.
Nimekuwa nikijiuliza sana, maajabu/uwezo aliokuwa nao huyu MWANAMALUNDI si ndiyo ule ule aliokuwa nao Bwana YESU kristo? Basi kama ni kweli, MWANAMALUNDI ndiye haswa YESU WA AFRIKA. Kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo, wazee wetu hawakuweza kujiandikia mambo mengi kuhusu huyu bwana na pengine leo hii tungekuwa hatumuabudu YESU bali angekuwa ni huyu yesu wetu MWANAMALUNDI.
WanaJF, mwenye kitabu au historia zaidi au maoni zaidi kuhusu MWANALUNDI na maisha yake, amwage hapa ili tuweze kuelimishana.
Basi watu wakamfata mwanamalundi na kumtaarifu kwamba kuni za kupikia chakula cha watu wa mkutano ule zimeisha.
Aliposikia hivyo aligeuka kuelekea upande ambapo ulikuwepo msitu akanyoosha mkono kuelekea huo msitu na kusema,''Batemagi pye abenaba''.
Yaani wakateni wote hawa..akimaanisha ile miti iliyokua msituni.Ghafla miti yote aliyoinyeshea mkono ilikauka yote.
Watu waliokua upande wa huo msitu nao walikauka pia.