Mtemi Ng'wanamalundi (Mwanamalundi) - Yesu wa Afrika?

Mtemi Ng'wanamalundi (Mwanamalundi) - Yesu wa Afrika?

Kuna wakati fulani nakumbuka kuna shule zilifungwa kwa baadhi ya mikoa ya mwanza na shinyanga, sababu ya Gamboshi. Nini na ni wapi Gamboshi?
 
Kuna wakati fulani nakumbuka kuna shule zilifungwa kwa baadhi ya mikoa ya mwanza na shinyanga, sababu ya Gamboshi. Nini na ni wapi Gamboshi?

Gamboshi ishabaki jina tu ndg hata mimi nimekuwa nikisimuliwa tu wakati nina ndugu zangu huko.
 
Ni kweli mkuu ulichokisema hata mimi hicho kitabu nilikisoma miaka ya mwanzo ya tisini na kama ulivyoelekeza akienda Bujora lazima atakipata.

Hata hivyo usukumani kuna simulizi za watu wengi sana zaidi ya Ng'wanaMalundi. Kuna simulizi za watu wengine kama Ng'wanagasasala, Samike, na kuna mwingine nimemsahau jina alikuwa na uwezo wa kuruhusu mwili wake ujae na kufiti chumba, kuna simulizi zingine za visima kuwa na uwezo wa kumeza watu na kuwatoa baada ya siku kadhaa wakiwa hai, simulizi za maajabu ni nyingi sana.
Ibhambanguru,
 
nimependa sana habari za mashujaa wetu, endeleeni kuturithisha tamaduni zetu.
 
Njia ya kuelekea Musoma ukitokea Mwanza kuna kitongoji ambacho jina silikumbuki lakini kutoka barabarani unaweza kuona alama za unyayo wa huyu Bwana kwenye jiwe. Yumkini alikuwa mtu wa ajabu. Kuna vitabu vinaelezea historia yake.

Tiba

Labda kama kuna sehemu mbili, kijiji hizo nyayo ziko kijijini kwake huyo mzee, kwa treni reli ya kati ukitoka shinyanya unashuka stesheni inaitwa seke, ni kijiji hicho mkuu, na ndiko alikozikwa, na ndugu zake wapo mpaka leo. Nikipata safari ya mikoa ya huko mimi pia ningependa kwenda kushuhudia na kujifunza historia.
 
I am among the remaining heirs of Ngw'anamalundi

Kweli mkuu? safi sana, nitawatembelea kijijini kwenu kujifunza nitapokuwa na safari kanda ya ziwa. BTW, kuna yeyote mzee kabisa mwenye angalau habari za "mkono wa tatu au wa pili"...mtu mwenye lau masimulizi yenye uhakika?
 
Labda kama kuna sehemu mbili, kijiji hizo nyayo ziko kijijini kwake huyo mzee, kwa treni reli ya kati ukitoka shinyanya unashuka stesheni inaitwa seke, ni kijiji hicho mkuu, na ndiko alikozikwa, na ndugu zake wapo mpaka leo. Nikipata safari ya mikoa ya huko mimi pia ningependa kwenda kushuhudia na kujifunza historia.

Mkuu mimi huko kijijini kwa huyu Bwana sikuwahi kufika ila nilionyeshwa nyayo kwenye jiwe moja along side barabara ya kutoka Mwanza kwenda Sirari kama sikosei ni maeneo ya Magu.

Tiba
 
Gamboshi ishabaki jina tu ndg hata mimi nimekuwa nikisimuliwa tu wakati nina ndugu zangu huko.

Na wewe ni wa huko gamboshi, wakati tuko shule tulikuwa tunasoma na jamaa wa kutoka gamboshi tulikuwa tunamtania vibaya mno...lol
 
Mkuu mimi huko kijijini kwa huyu Bwana sikuwahi kufika ila nilionyeshwa nyayo kwenye jiwe moja along side barabara ya kutoka Mwanza kwenda Sirari kama sikosei ni maeneo ya Magu.

Tiba

Kweli mkuu, tatizo vitu kama hivi haviko well documented, ngoja tumuulize ndugu yake mwanamalunde donlucchese
 
Last edited by a moderator:
VITA VYA USUKUMANI.
Baada ya siku chache Kapela aliporudi nyumbani kwake, kutoka Ikonongo, Mirambo alituma habari kwa mjomba wake Kapela kuwa ajiandae maana anakuja kumsaidia kuwpigana na maadui wake.Kapela alikubali kupewa msaada huo. Mirambo alikuja na jeshi lake hadi Ukune katika Ikulu. Akapiga kambi yake katika mlima wa Mangua. Kapela akamwambia Mirambo kuwa safari yao ni kuelekea Usukumani kupita Ukamba, Luhombo na Tinde.
Walipofika katika mpaka wa Tinde na Usanda, Mirambo alisema kuwa yeye atapitia njia ya Shinyanga na Kapela apitie Nindo na kukutania Usumau. Mirambo alikuwa na fununu kuwa sehemu za Usia kuna ngombe wengi wa Wasukuma.Hivyo alikusudia kuteka nyara ng'ombe hao. Kapela alimwambia Mirambo kuwa ukifika Usanda asipige eneo hilo kwa kuwa huko kuna wajomba zake .Safari ya Mirambo haikuwa na mafanikio yoyote kwa kuwa Wasukuma walikuwa wamepata habari kuwa Mirambo atapita kuchukua ngombe wao. Wasukuma waliwaficha ng'ombe wao porini, Mirambo akaambulia wanawake tu. Akaendelea mpaka Seka huko alikuta kundi kubwa la ngombe ambao walikuwa ni wa Mwanamalundi, mtu maarufu sana kwa uchawi. Mirambo akashindwa kuwachukua na askari wake wengi wakafa kwa madawa ya mchawi huyo na kwa sababu ya njaa. Mirambo alienda moja kwa moja mpaka Usumau ambako waliahidiana kukutana na Kapela sehemu iitwayo Bungulwa . Kapela alifanikiwa kuteka ngombe wengi akiwemo ngombe dume wa mizimu wa Msukuma wa Nela .Ngombe huyo alikuwa anaitwa Ilindilo, yaani ngombe wa kulinda nchi. Mirambo akamwambia Kapela kuwa nimemkuta Msukuma moja huko ni mchawi kamaliza askari wangu Akamsimulia habari zote za Mwanamalundi. Mirambo aliona wivu kuwa yule ngombe dume na kuapa kuwa lazima amchukue. Kapela na Mirambo walikaa muda mrefu Usukumani Nela, Usumau na Uhungukila. Na walifaulu kuteka mali nyingi ng'ombe wengi pamoja na watu pia.

Safi Mkuu, hivi kuna vitabu hata vya hadithi vya nana hii, maana tumejazwa vya wazungu tu kwenye maktaba na maduka yetu ya vitabu!
 
Ukienda Tabora baada ya Kipalapala kuna jiwe moja ambalo hulia kama ngoma. Nadhani ndio mahali ambapo watemi wa kinyamwezi huwa wanaskimikwa u-temi. Ni kweli kule Sengerema kuna jiwe lenye nyayo za Ng'wanamalundi pamoja na mbwa wake. Tulienda kuliona jiwe hilo zamani sana nakumbuka ni miaka ya 1980's. kwa sasa sijui kama bado lipo. Kaburi la Ngw'anamalundi kwa ninavyofahamu liko wilaya ya Kwimba, maeneo ya Ngudu ingawa binafsi bado sijafika kuliona.

Ukitaka kupata historia na maajabu ya watu wa Usukumani tembelea Bujora Museum. Ina mengi ya kusisimua sana.

Loh, hiztoria zetu waafrika za kuabiana kwa mdomo zinapotosha sana, mtu unajikuta huku umeambiwa hivi huyu kakuambia hiki....unabaki katikati!!
 
Kwa nini umfananishe NG'WANAMALUNDI na yesu, mwache yesu abaki kuwa yesu na ng'wanamalundi abaki kuwa yeye. usijaribu kuwalinganisha

Hilo ndiyo jambo pekee la msingi, mleta mada naona alitereza. YESU na Mwanamalundi ni watu tofauti sana na culture zao ni tofauti sana, japo wote walikuwa na "maajabu". Kuwalinganisha si kosa sana kama unajaribu kuangalia similarities, lakini hawawezi kuwa interchangeable.
 
Tatizo hapa Yesu mwenyewe alikua mtu tu kama Ng'wana malundi. Ispokua wazee wa kiyahudi walizitunza hadithi zake ktk maandishi na kuendelea kuhadithiana kizazi na kizazi mpaka zikakufikia na wewe.

Amina kaka Mkubwa!
 
Ungefananisha kati ya Haile Selasie ( Mungu wa watu weusi-Ethiopia) ningekuelewa kidogo.
Jaribu kumfuatilia huyu rasta man utajua yeye ni nani na ni wapi alipozidiwa na Yesu.
 
Kuna kijiji kinaitwa ISOLO kata ya SHISHANI wilaya ya MAGU mkoa wa MWANZA hapo Kuna bao limechongwa vizuri ajabu kwenye mwamba/jiwe inasemekana ni miongoni mwa vituo alivyopita Ng'wanamalundi Enzi zake.

ISOLO means BAO
 
WanaJF, kuna watu maarufu waliowahi kuvuma katika historia za bara letu, na mmojwapo ni huyu MWANAMALUNDI kutoka kabila la wasukuma. Niliwahi kusoma kitabu kilichokuwa kinaelezea historia yake kwa ufupi na maajabu aliyowahi kufanya wakati wa uhai. Moja ya maajabu ni pamoja na kupona wagonjwa, kupita katikati ya ziwa huku maji yakiacha njia, kuacha nyao zake kwenye mawe, kukausha miti kwa ajili ya kuni nk.

Nimekuwa nikijiuliza sana, maajabu/uwezo aliokuwa nao huyu MWANAMALUNDI si ndiyo ule ule aliokuwa nao Bwana YESU kristo? Basi kama ni kweli, MWANAMALUNDI ndiye haswa YESU WA AFRIKA. Kutokana na kuwa nyuma kimaendeleo, wazee wetu hawakuweza kujiandikia mambo mengi kuhusu huyu bwana na pengine leo hii tungekuwa hatumuabudu YESU bali angekuwa ni huyu yesu wetu MWANAMALUNDI.

WanaJF, mwenye kitabu au historia zaidi au maoni zaidi kuhusu MWANALUNDI na maisha yake, amwage hapa ili tuweze kuelimishana.

endelea kumuabudu mbona umeshakubari kusema ni yesu wako.
 
Back
Top Bottom