Mtemi Ng'wanamalundi (Mwanamalundi) - Yesu wa Afrika?

Nilitaka kuandika andiko kuwa mwana malundi ni Yesu wa Tanzania, ni Yesu wa Kabila la wasukuma. Laiti tungethamini mzimu wake kuutii na kuutukuza kama ilivyo kwa Yesu tusingekuwa hapa tulipo unajua ukiwa na elimu ya kiroho na yenye tafakari kubwa **** hisia za mengi unazipata.


Mungu amlaze mahali pema mwana malundi.

Yesu si kitu hakuwa na tofauti na mwanamalundi sidhani kama walikuwa na tofauti sana, sikatai Yesu alikuwa kiboko na historia inasema alikuwa kiboko haswa ila nadhani kutukuzwa kwake kunafanya aonekane kiboko zaidi, hata nasi tungemtukuza mwanamakundi naamini hata roho wake angetenda kwetu, miujiza na upako wa utakatifu wake ungekuwa tiba kwetu.


Asante. Niishie hapo
 
Akili kwani tunazo basi?
 
Kupitia hii post, nimeshaanza kutilia mashaka juu ya uwepo wa huyu mwamba na mambo aliyowahi kuyafanya kwasababu kuna ubishani mkubwa humu,
Mimi nachoweza kukiuliza hizo nyayo nani alijui kweli nizamwanamalundi? Kama jiwe automatically lipo hivyo na mtu akaja kukuambia kuwa ni nyayo zangu utakataa?
Kuna jiwe moja hivi nilionaga kwenye picha linafanana na mb** je hiyo aliiacha nani? Hya mambo inabidi tuelewe mwanamalundi alikuwa mtu mjanja sana kama akina yesu na mohamedi huku ulaya ya mashariki.
 
Reactions: EEX
I think your right
 
Siyo kweli, kwa 95% story ya huyo mtu ni ya kweli, na hata leo unaweza kusikia nguvu hizo kwa mtu ukakataa kwa sababu hujaona, ukijaribiwa tena kwa kuambiwa utaweza kuamini, kiufupi wewe hata dini huna, kama unayo unaaminije yaliyo andikwa? Na kama unaamini yaliyo andikwa kwenye kitabu Cha Imani yako kwa kua tu yaliandikwa miaka 2000 iliyo pita ndiyo kigezo Cha wewe usiamini yaliyo andikwa ktk miaka 100 iliyo pita? Dunia iko na mambo mengi kwa baadhi ya watu na story ya Ngw'wana Malundi ni ya kweli
 
Kwa ufupi yeye dini hana na kama anayo???
Ivi unaelewa hata ulichoandika? Hajakataa kwamba mwanamalundi alishawahi kuwepo, ila anakuambia kulingana na uwezo wake wa kufanya vitu ambavyo wengi walishindwa kufanya basi akawa maarufu katika jamii yake, ila walivyokuja kuandika historia hatakama iwe ni miaka 2000 iliyopita walikoleza au kwa maana nyingine walipamba baaadhi ya matukio yake yaani kwa maana nyingine walioandika walikoleza na nikitu cha kawaida katika historia za wengi zilizoandikwa kama akina yesu akina Mohammed nawengineo....... usibishane kisa wewe ni msukuma kuna mda unaweza kubisha ili kujiona mshindi lakini unajidanganya mwenyewe.
 
Sawa. Ila binafsi sijashawishika kuamini huo ujinga kumhusu Mwanamalundi. Kama kweli alikuwa na uwezo huo wa kipekee mbona alishindwa kuua hata mzungu mmoja miongoni mwa wale wazungu waliokuwa wakitawala Tanganyika huku na yeye akiwa anaathirika na udhalimu wao hadi kuwekwa kizuizini? Kama alifanya hivyo tupate ushahidi wake. Tunaambiwa tu kwamba aliweza kuwatoroka yeye kama yeye. Kwamba niamini alikuwa na uwezo wa kunyoosha kidole upande fulani na WATU WOTE wa direction hiyo wakafa kama inavyosimuliwa? Aah bana achani basi utani. Kama alifanya hivyo naamini bado kuna watoto na wajukuu wa waliokufa kutokana na Mwanamalundi kunyoosha kidole upande huo na tupate ushahidi kutoka kwao juu ya upuuzi huu. Tusipende kukuza mambo bila logical analysis.
 
Kule DRC yuko mtu aliyekua anaitwa Kimbangu ..huyu mpk leo anawafuasi wake..wanaamini ndio Yesu
 
Mlisahau ya kwenu mkakumbatia Yesu aliyezaliwa huko Uyahudini. DNA ya Mwafrika na ya Kiyahudi wapi zinaendana? Tuzingatie imani zetu za asili! Tutaandamwa tu na laana za kuacha uhalisia wetu, mababu wamekasikika. Tutafute Yesu wa Afrika.
 

Wasukuma bwana. Wanaamini yasiyoaminika. Kama alikuwa na nguvu za aina hiyo? Zimepotelea wapi? Han generation mpya alioiachia hizo nguvu?
Sababu ya kuamini sana haya madudu, wamebaki kutoana kafara za kupata mali na utajiri. Geita mauaji ya ajabu ajabu kama Njombe na Katavi
 
Naelewa...kumbe alipewa uganga na bibi mmoja ili acheze ngoma. Halafu uganga ukaishiwa nguvu ukapotea πŸ˜‚ πŸ˜‚ 😎 😎 🀣🀣
 
Yesu nguvu zake kamwachia nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…