tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
MTENDAJI MKUU WA TANROADS AHIMIZA WATUMISHI KUSHIRIKI KUPIGA KURA OKTOBA 29, 2025
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta, amewahimiza wafanyakazi wote wa TANROADS nchini kote kujitokeza kushiriki katika zoezi la kupiga kura litakalofanyika Jumatano, Oktoba 29, 2025.
Soma pia: Dkt Samia: Wasiwatishe kwenda Kupiga Kura ,Tumejipanga Kuwalinda
Akizungumza katika ujumbe wake kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo, Mhandisi Besta amesema ni muhimu kwa kila mtumishi wa TANROADS kutumia haki yake ya msingi ya kidemokrasia kwa kuchagua viongozi wanaowataka katika ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani.
“Ninaungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuwahimiza wafanyakazi wote wa TANROADS kushiriki kikamilifu katika kupiga kura siku ya Jumatano, Oktoba 29, 2025,” alisema Mhandisi Besta.
Aidha, Mtendaji Mkuu huyo amewataka Mameneja wa TANROADS katika mikoa yote 26 nchini kuhakikisha wanawahamasisha wafanyakazi walioko chini yao kujitokeza kwa wingi siku hiyo muhimu ya uchaguzi.
“Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) pamoja na Serikali imetenga siku ya Oktoba 29 kuwa siku rasmi ya kupiga kura. Hivyo, ni jukumu letu kutumia nafasi hiyo kuchagua viongozi tunaowataka,” aliongeza Mhandisi Besta.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kuwa moja ya matukio muhimu ya kidemokrasia nchini, ambapo wananchi watapata fursa ya kuwachagua viongozi wao watakaowaongoza katika kipindi kijacho cha miaka mitano.