Mtendaji wa Kijiji cha Hydom amshindilia makonde mwanakijiji. Asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Safi sana Adella. Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutuletea watendaji wachapakazi kama Bibie Adella.

Adella ameona akitafuta bakora amchape mwananchi anachelewa sana akaamua atumie magumi kumsulubisha huyu mwananchi mnyonge. Hakika sote tutaisoma namba mpaka tuseme "ccm nambari one"
 
Mbona wengine wanawatembezea viboko hadharan raia hamsemi
 
Kimada wa RC Mnyeti huyo
 
Huyo pia ni kufuata na kumpa kipigo, KWA nini amfanyie hivi mwanakijiji
 
Mtendaji alikiuka utaratibu uliokubalika wa viboko,badala yake akatumia ngumi. Aadhibiwe tu hamna namna.
 
Mhe. Magufuli angalia watumishi wako walivyo na stress pamoja na hasira za jirani kutokana na Machungu ya kutoongezewa Mishahara pamoja na madaraja. Hatimaye Hasira zao zote wanahamishia kwa Wanakijiji wanaowaongoza.

Mambo haya hayakuwahi kujitokeza miaka ya nyuma ambapo JK alikuwa akiwapa nyongeza zao kila mwaka. Watumishi wa Umma walikuwa wamejaa nyuso za bashasha na furaha kila siku, sio kama nyakati hizi ambapo wamejaa na hasira inafikia kipindi ukicheka mbele yao wanahisi unawacheka waoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwakweli alichokifanya si kitendo cha kiungwana,lazima atakuwa na matatizo ya akili
 
Huo utaratibu wa viboko umekubalika wapi?
Utaratibu huu ni wa KITAIFA.waziri au naibu waziri anatenda kulingana na maamuzi ya baraza la mawaziri.Umesikia mahali popote wenye mamlaka ya uteuzi wakikemea watu kuchapwa au kuchapa viboko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…