Mtendaji wa Kijiji cha Hydom amshindilia makonde mwanakijiji. Asimamishwa kazi kupisha uchunguzi

Kwani chanzo ni nini wadau kwa mwenye kujua
Watendaji wa ngazi za chini wanakutana na madhila makubwa sana kukabiliana/kuongoza watanzania wale halisi wa huko chini.
Wanafuatilia au walio karibu kidogo na serikali za mitaa na shughuli za maendeleo za huko chini wanaweza Kuelewa na wakajipa nafasi ya kuchambua na kusubiri taarifa ya uchunguzi.

Katika hali ya kawaida ni vigumu sana kwa kiongozi wa ngazi yoyote kufanya hivi bila sababu za msingi. Majibu na vitendo vya wananchi kwa viongozi hawa ni hatarishi.

Si ajabu kwa kiongozi kuweka pembeni busara na makatazo ya kiuongozi na kuvaa ubinadamu km wengine. Hata wao wana roho za damu na nyama, wana nyongo hawa, wanakerwa sana sana na mapambano magumu ya kuhamasisha maendeleo.
 
Na kama mfereji unaonekana uwezekano kuwa kufuli hakuna ndani ni mkubwa.
Sexual frustration ni ugonjwa pia. Ukute mtendaji hapati hai yake ipaswavyo ndio anazusha ugomvi ili tu apate ule msuguano.

Kati ya style zote za ngumi kaona ya kumkalia jamaa juu ndio style pekee.
 
Nakuunga mkono kwa 200%
 
Nchi hii bwana, kila mtu mbabe, wakuu waserikali, wameibaka demokrasia, wameteka taasisi zote nyeti, usalama, Hazina, Mahakama,sasa wanakula, wanaiba, wanajilimbikizia mali, Mwananchi anabaki anatazama.

Sasa huku chini, kwa vile Kuna polisi, na Hawa watendaji wadogo, ambao wanaona wakubwa zao wanavyoiba, Ili wasipige kelele na wao wanaruhusiwa kuwatwanga Raia, wapole, waibe, waumize, na hutasikia Waziri akikemea Hili.

Sasa huku watendaji wanatutwanga ngumi
Wakuu wa wilaya wanatuchapa bakora
Vijana wa mabakamabaka, wanatupa mateso, vipigo, harafu wanaona ni sifa.
Kilichobaki hapa, mwananchi hana mtetezi
 
Hili ni tatizo sugu nakumbuka Waziri Mkuchika alitoa semina namna ya kufuata sheria na haki lakini imekuwa ngumu sana kwa watendaji wengi.

Wengine wameanza hata kuwachapa viboko wanao waona ni wakosaji,wengine wanawadhalilisha watumishi mbele ya kadamnasi,wengine wanawasimamisha kazi watumishi bila kuwapa haki ya kusikilizwa nk.

Ni kweli tunahitaji maendeleo tunataka wabadhilifu wachukuliwe hatua nk lakini bila kufuata taratibu za kisheria na haki za binadamu itakuwa ni sawa na kuzuia uhalifu kwa kufanya uhalifu mkubwa.

Hivi hawa jamaa wakipata madaraka mbona wanasahau utu na busara? Hivi kiburi na majigambo yote wanatoa wapi? Hivi ni kweli kuwapigania kwa jasho na damu ili washinde na watuongoze ilikuwa na maana hiyo wanayotufanyia?

Bado tuna mapenzi mema kwa viongozi lakini ni muhimu wakajitafakari naona kama wanakwenda nje ya mstari wa matarajio yetu,Muhimu hapa wabadili fikra sheria zipo zitumike kusimama mbele ya kadamnasi na kufanya udhalilishaji ili upigiwe makofi ni kasoro mojawapo na inapelekea viongozi wengi kuiga na kuamini ndiyo taratibu za uongozi.
 
Mitano Tena[emoji1787][emoji1787]
 
Tumemjua mtendaji naye anatimiza majukumu yake, sema tu hakuwa na fimbo hapo kulikuwa na majani!

Everyday is Saturday........................ 😎
 
Na hao walio pembeni wamekosa utu, Mtu anapigwa wao wanaangalia tu na kuishia kusema "Adela achana nae" hawawezi hata kuamulia. Mtu anapigwa kichwani, vipi kama huyo angeuwawa hapo?
 
Video zilisambaa kwenye mitandao zikionyesha namna Watanzania wanachezea viboko kutoka kwa viongozi wao. Naona wenzetu wamepandisha ngazi na sasa imekua ni mwendo wa ngumi.

Kuna hii video inayosambaa inaonyesha mtendaji anamtembeza makonde mwananchi maskini, aisei poleni sana bandugu. Endeleeni na hizo show zenu mwisho mtatuambia yupi ndiye starring.

Hii hapa video, mtatia akili raundii hii.

https://www.jamiiforums.com/data/video/2670/2670669-8aea8dd2bf2a6f283ac0c544ac090301.mp4
 
Hahahahaa.. we jamaa inaonesha umetumiss sana.

Njoo huku bongo kidogo ule maisha basi maana inaonekana huko kwenu hali si hali.
 
Hahahahaa.. we jamaa inaonesha umetumiss sana.

Njoo huku bongo kidogo ule maisha basi maana inaonekana huko kwenu hali si hali..

Bado hamjanyooka....mtafundishwa nini maana ya uzalendo wa kijamaa.
 
Matukio Kama haya huwa najiuliza ni Nani huwa anapiga picha!!??

Huwa anapiga kwa lengo gani?? Na je Nani huwa anaisambaza??
 
Tatizo Magufuli ndo anawapenda watu violent kama huyo Mtendaji, tusishangae akapandishwa cheo kuwa Afisa Tarafa
 
Tusimlaumu sana mtendaji,unaezakuta msela ndo alianza kutaka kumpiga,akakuta mama naye yuko fiti...badala ya kumdunda mama akazidiwa yeye na ndo mana wananchi wakaacha
 
Halafu mbona ni Mwanamke imekaa vp hap na anay pingwa MBN mwanaume kaaen mtafakar wakuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…