Mti ulioanguka na baadae kusimama wenyewe Geita ni sayansi wala siyo ushirikina kama wengi wanavyoripoti

Samico Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2022
Posts
791
Reaction score
1,852
Iko hivi!

Kuna taarifa ya mti uliokuwa umeanguka kuonekana umesimama tena baada ya kukatwa matawi huko geita.

Tukio hili wengi wamelihusisha na imani mbalimbali za dini zao!

Lakini kiuhalisia mambo kama haya hutokea na kwa sisi tulioishi porini tushashuhudia sana wala si mara moja!

Sayansi ya ukuaji wa miti iko hivi!

Uelekeo wa matawi ya mti huwa uko sambamba na ukuwaji wa mizizi ili kubalansi!

Yaani ukiona tawi linakua kuelekea upande mmoja kwa ukubwa basi tambua huko chini lazima kuwepo mzizi unaoelekea kinyume chake ili kubalansi matawi kwa mizizi yake yenyewe!

Hivyo matawi yakizidi uzito kuliko uwezo wa mzizi huo mti lazima uanguke!

Sasa katika mazingira hayo haliya hewa ya mvua ya upepo unaosukuma kuelekea matawi yalipo huongeza uzito kwenye matawi kiasi cha mizizi kuelemewa hata kuchomoka ardhini endapo ardhi itakuwa imelowa hada kwenye ardhi ya kichanga!

Mti ulioangushwa kwa style hii ukiukata likabakia shina endapo ile mizizi iliyonyofoka ardhini itakuwa mizito kuriko shina lazima mti utasimama na mizizi kurudia sehem yake ili kubalansi!
Inaweza isiwe ndani ya siku moja lakini ikichagizwa na mvua au upepo utakaosaidia kusukuma lileshina hurudia sehem yake na kuendelea kuota endapo mtu utakuwa haujafa

Hii haina tofauti na baisikeli au pikipiki au gari iliyobeba magunia mazito kubinuka na ukipunguza magunia tairi zinarudi chini!

Mawazo ya watu wanaowaza ushirikina huwa yamefungwa kuwaza uhalisia, wambie wakazi wa Geita waachane na imani potofu!

Ule mti ungekuwa una mazingira ya kichawi kwa nilivyowahi kuona ule mti usingekubali kukatwa kizembe ..mkataji angepata shida na pengine ungeelea hewani bila mizizi.

Screenshot_20250321-193953~2.png
 
Sisi ni wakali wa sayansi, lakini isiyo na maana na tija
 
View attachment 3278968
Mkuu inamaana unataka kusema mizizi ya mti ni elastic au ina shock ups?

Mi nadhani haiwezekani labda kuna watu walivizia usiku wakausimamisha.
 
Yaani mti uanguke leo siku 2...3 unyanyuke wenyewe as if as hapakua na hitilafu yoyote😳
 
Duh! Jamaa umepambana sana kutetea hoja yako lakini nina mashaka kwa asilimia kubwa
 
Back
Top Bottom