Mti ulioanguka na baadae kusimama wenyewe Geita ni sayansi wala siyo ushirikina kama wengi wanavyoripoti

Mti ulioanguka na baadae kusimama wenyewe Geita ni sayansi wala siyo ushirikina kama wengi wanavyoripoti

Bila picha 😕😕
Iko hivi!

Kuna taarifa ya mti uliokuwa umeanguka kuonekana umesimama tena baada ya kukatwa matawi huko geita.

Tukio hili wengi wamelihusisha na imani mbalimbali za dini zao!

Lakini kiuhalisia mambo kama haya hutokea na kwa sisi tulioishi porini tushashuhudia sana wala si mara moja!

Sayansi ya ukuaji wa miti iko hivi!

Uelekeo wa matawi ya mti huwa uko sambamba na ukuwaji wa mizizi ili kubalansi!

Yaani ukiona tawi linakua kuelekea upande mmoja kwa ukubwa basi tambua huko chini lazima kuwepo mzizi unaoelekea kinyume chake ili kubalansi matawi kwa mizizi yake yenyewe!

Hivyo matawi yakizidi uzito kuliko uwezo wa mzizi huo mti lazima uanguke!

Sasa katika mazingira hayo haliya hewa ya mvua ya upepo unaosukuma kuelekea matawi yalipo huongeza uzito kwenye matawi kiasi cha mizizi kuelemewa hata kuchomoka ardhini endapo ardhi itakuwa imelowa hada kwenye ardhi ya kichanga!

Mti ulioangushwa kwa style hii ukiukata likabakia shina endapo ile mizizi iliyonyofoka ardhini itakuwa mizito kuriko shina lazima mti utasimama na mizizi kurudia sehem yake ili kubalansi!
Inaweza isiwe ndani ya siku moja lakini ikichagizwa na mvua au upepo utakaosaidia kusukuma lileshina hurudia sehem yake na kuendelea kuota endapo mtu utakuwa haujafa

Hii haina tofauti na baisikeli au pikipiki au gari iliyobeba magunia mazito kubinuka na ukipunguza magunia tairi zinarudi chini!

Mawazo ya watu wanaowaza ushirikina huwa yamefungwa kuwaza uhalisia, wambie wakazi wa Geita waachane na imani potofu!

Ule mti ungekuwa una mazingira ya kichawi kwa nilivyowahi kuona ule mti usingekubali kukatwa kizembe ..mkataji angepata shida na pengine ungeelea hewani bila mizizi.

View attachment 3278968
 
ubishi ni calamity , kuna kipindi tabora aka mboka kuna mti ulikatwaga na kisiki kikakokwa moto na wazee wa mkaa aka ma scavengers ikapit miaka kadhaa ule mti ukaota ghafla yaani kama umepita asubuhi umeenda town then mchana unarudi bushi unakutana na mti uko fresh kabisa ,na viongoz wa serekale walifika kushuhudia jambo kustaajabisha , kwako mzee wa nguri wa maporini na allied sciences ushawahi kukutana na hii scenario au utajifariji ni stori ya kijiweni tu?
 
Kuna jamaa kasema huo mti ni dawa ya nguvu za kiume, na keshaanza kupokea orders kutoka kwa wale...
 
ubishi ni calamity , kuna kipindi tabora aka mboka kuna mti ulikatwaga na kisiki kikakokwa moto na wazee wa mkaa aka ma scavengers ikapit miaka kadhaa ule mti ukaota ghafla yaani kama umepita asubuhi umeenda town then mchana unarudi bushi unakutana na mti uko fresh kabisa ,na viongoz wa serekale walifika kushuhudia jambo kustaajabisha , kwako mzee wa nguri wa maporini na allied sciences ushawahi kukutana na hii scenario au utajifariji ni stori ya kijiweni tu?
Miti ya kichawi ipo! Lakini kwa hili tukio ni sayansi ya gravitational tu hakuna uchawi hapo!
Walipoukata uzito ukapungua ukasimama kwa uzito wa mizizi ni kama mzani tu unavyofanya kazi
 
weka equation tuelewane vizur maana theory(maelezo) tupu nayo ni ushirikina mmojawapo.
 
Back
Top Bottom