Mti wa Mkungu unafananaje?

Mti wa Mkungu unafananaje?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nimeambiwa ni mti wa asili unaofaa kwa kivuli. Sikukumbuki kama nimeshauona ulio mkubwa.

Kama kuna mtu mwenye picha ya mti mkubwa wa
Mkungu naomba aiweke hapa, na ya mti wa Mdodoma pia.

Ninataka kufanya maamuzi ya mti wa kupanda mahali fulani, MDODOMA au MKUNGU!

Naomba kuwasilisha🙏
 
Huo Hapo
Screenshot_20240723-130504_1.jpg
 
Nimeambiwa ni mti wa asili unaofaa kwa kivuli. Sikukumbuki kama nimeshauona ulio mkubwa.

Kama kuna mtu mwenye picha ya mti mkubwa wa
Mkungu naomba aiweke hapa, na ya mti wa Mdodoma pia.

Ninataka kufanya maamuzi ya mti wa kupanda mahali fulani, MDODOMA au MKUNGU!

Naomba kuwasilisha🙏
Hujui mkungu umezaliwa wapi? Mdodoma nimepanda kwangu lakini naona bora ile miamvuli.

Ila panda mstaferi uambulie matunda na majani yake ni dawa.

Kuna miembe ya kisasa inazaa mapema aiendi juu sana unapata kimvuli na matunda.
 
Nimeambiwa ni mti wa asili unaofaa kwa kivuli. Sikukumbuki kama nimeshauona ulio mkubwa.

Kama kuna mtu mwenye picha ya mti mkubwa wa
Mkungu naomba aiweke hapa, na ya mti wa Mdodoma pia.

Ninataka kufanya maamuzi ya mti wa kupanda mahali fulani, MDODOMA au MKUNGU!

Naomba kuwasilisha🙏
Kama una kiwanja cha 15Ă—20 mkungu unaweza kukijaza kiwanja chote hicho namna unavyozagaza matawi yake.

Sina picha yake, lakini ni mti mrefu una majani mapana na matunda yake ni mekundu matamtam watoto hupenda kuyafakamia.
 
Kama unataka mti bora wa kivuli (majani mengi na mapana sana), matunda, mandhari mazuri (pambo), kuzuia upepo mkali na vumbi pamoja na kushikilia ardhi ili kuzuia mmomonyoko wa udongo, mkungu ndio mti sahihi.

Unakunywa maji mengi na kuzuia pia uwepo wa vinamasi na magugu.

Faida ziko maridhawa. Mengine ni tibasili kwa kutumia majani, kokwa, maua, magome na miziz yake.

Wengi hawajui kutofautisha mtiki na mkungu.
 
duh! hauujui mkungu kweli wengine mnaishi ulaya!
Labda nilishauona bila kuutambua kama ndiyo unaoitwa kwa jina hilo. Pengine mimi ninautambua kwa jina la Kilugha.

Hata hivyo Tanzania ni kubwa. Inawezekana miti fulani ikawa inaota kwenye baadhi ya mikoa tu.
 
Back
Top Bottom