Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Huwezi kushinda Ubunge ccm bila rushwa, Labda uwaloge wagombea wengine, uwatishe ama uwauwe
kulinda kura umbali wa mita 200??Lindeni kura zenu. Si mnajifanya mnapinga reforms.
Hahahaaaaa!swali safi kabisa,maana hata kuja mtandaoni kulalamika ni kosa kabisa alitakiwa ufuate utaratibu wa chama uliowekwa.Umelalamika kwa nani?
Mmelalamika kwann wakat hiyo ni jadi!! Hakuna kipya hapo huo ndio utaratibu waoHuyo hapo kwenye video anaitwa Hamis Salum Hamis, ni mmoja wa watia nia kupitia CCM nafasi ya Ubunge kwenye jimbo la Meatu Mkoani Simiyu.
Hapo yupo katika moja ya kijiji uko kata ya Makao, na yupo na Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu anaitwa Anthony.
Hapo yupo kwenye mkutano na wanaCCM wa Kijiji hicho na ambao ni wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Wilaya. na hapo mkutano huo aliufanya hivi karibuni wakati katazo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg, Nchimbi alipokataza mikutano na makongamano kwa watia nia na watu wengine ndani ya CCM katika kipindi hiki cha mchakato.
Yeye alikaidi agizo hilo, na akaendelea kufanya mikutano licha tena viongozi wa CCM Wilaya nao wakimuona na kumnyamazia, hawakuchukua hatua yeyote hakuna onyo wala jambo lolote.
Watia nia wenzake tumetoa taarifa juu ya mtu huyu kuendelea na mikutano na kugawa pesa kwa wajumbe, lakini hatujasikilizwa badala yake tunatishiwa,
Tumeita vyombo vya habari kuzungumzia jambo hili lakini hakuna lolote ambalo limefanyiwa kazi, sasa tunajiuliza huyu mtu ni Nani? ndani ya CCM, anakichafua sana chama, kila siku anafanya mikutano na kugawa pesa kama ambavyo inaonekana kwenye hii video fupi.
Amefanya mikutano vijiji vyote vya Wilaya ya Meatu, na kila sehemu amegawa pesa kama njugu, tumetoa taarifa, tumewaambia viongozi wa Wilaya na mkoa lakini hawajachukua hatua, anagawa hizo pesa huku akisema viongozi wa CCM na Wilaya wote wapo chini yake.
Sasa tunaomba viongozi wetu wa CCM Taifa kuingilia jambo hili ambalo lipo kwenye Wilaya yetu ya Meatu, huyu siyo kiongozi mzuri, anatafuta madaraka kwa pesa, na siyo kwa hoja kama ambavyo tulivyo sisi wengine watia nia.
Na taarifa ambazo tunazo eti huyu ndiye amepitishwa kwenye vikao vya mchujo, jina lake ndilo la kwanza na ndiye amependekezwa na vikao vya CCM vya mchujo vya Wilaya, wakati amekiuka kanuni nyingi za ndani ya Chama.
Hahahaaaaa!swali safi kabisa,maana hata kuja mtandaoni kulalamika ni kosa kabisa alitakiwa ufuate utaratibu wa chama uliowekwa.
Ndiyooooo!Huyo si ndio mmiliki wa kiwanda cha jambo?
Ila tukumbuke 2020 kwenye kura za maoni aliangushwa na hawara yake! Na safari hii yumo sijui itakuwaje!Salum mbuzi,, huyo jamaa huko meatu anaepmbana nae ajipange sana.
Hawara yake hana nguvu hiyo......Ila tukumbuke 2020 kwenye kura za maoni aliangushwa na hawara yake! Na safari hii yumo sijui itakuwaje!