GE2025 Mtia nia Urais CUF atawapa Vijana Ajira

GE2025 Mtia nia Urais CUF atawapa Vijana Ajira

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mtia nia wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi mkuu kupitia Chama cha Wananchi CUF Nkunyuntila Siwale amesema endapo Chama chake kitampa ridhaa ya kuwania nafasi ya Urais atawapa ajira Vijana wote nchini kwani anazijua mbinu zote.

Mzee Siwale ameyasema hayo Julai 15, 2025 baada ya kukabidhiwa fomu ya Kuwania Urais na Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Momba Enock Mwalukasa, "Mimi nikipita, nataka vijana wote wa Tanzania wapate ajira. Mbinu za kupata ajira nazifahamu, mpaka nikipata ridhaa kwa wananchi, Nazifahamu" Alisema Mzee Siwale

Soma pia:


Aidha Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa Bw. Yasin Mlotwa amebainisha idadi ya watia nia wa nafasi ya Urais kupitia chama hicho cha kufikia sita huku Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Momba Enock Mwalukasa akifurahishwa na mchakato wa kuwania nafasi hizo za uongozi ndani ya Chama cha Wananchi (CUF).


​
Chanzo: Manara TV
 
Vijana wanataka hela ya bundle tu waweze ku flex mitandaoni.
 
Back
Top Bottom