Mtihani mkubwa kwa Rais Samia ni kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma. Je, ataweza?

Mtihani mkubwa kwa Rais Samia ni kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma. Je, ataweza?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,734
Reaction score
5,750
Watumishi wa umma wanamaumivu makubwa mioyoni mwao sio siri, hata kama kipaumbele ilikuwa kumaliza kwanza mambo ya msingi kama ujenzi wa miundo mbinu, kuimarisha sekta ya afya na elimu lakini waalihitaji kuonewa huruma.

Waziri mkuu alikatisha watu tamaa kabisa pale aliposema eti kuongeza mishahara watumishi wa umma ni kusababisha maisha kuwa ghali. Jambo ambalo sio kweli maana kwa miaka hii mitano watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara na maisha yamepanda pia.

Siku hazigandi na leo ni tarehe nne na mei mosi ipo karibu, watumishi wa umma watapata faraja kama wakisikia wameongezwa mishahara yao. Swali linabaki kuwa je, mama Samia rais wa JMT ataweza kufanya maamuzi ya msingi kwa ajiri ya watumishi wa umma?
 
Inawezekana tena sana tu, apitie bajeti ya mwisho ya Kikwete alipoongeza mshahara July 2015 halafu warekebishe bajeti yao 2021/22
 
Mtihani mwingine Mkubwa Ni unyanyasaji wafanyakazi sekta binafsi na ulipwaji wa MAFAO.

Mfano Sekta binafsi, watu wengi wanapoteza kazi kwa sababu mbali Mbali. FAO LA KUJITOA ni muhimu.

Watu walipwe mafao yao, ili wafungue biashara zao na wawe walipa Kodi wapya.

Mtu akipoteza Kazi mfano wenye elimu, wengi wanapoteza mafao yao. Wanaambiwa wasubiri 55 years

Wabunge wa CCM wanapitisha miswada bungeni ya kunyanyasa Wanyonge'.

Hao watetezi wa Wanyonge' wako wapi?
 
Watumishi mngetuonea huruma na sisi ndugu zenu tuajiriwe kwanza japo nasi tufaidi kidogo keki ya taifa kama nyinyi!!
Sasa mbona kuajiriwa kwenu hakuna kabisa uhusiano na kuongezewa mishahara wafanyakazi, au kupandishwa madaraja yao?

Yaani na nyinyi mnatakiwa muililie Serikali kwa wakati wenu ili iwaajiri! Lakini kutaka sisi wafanyakazi tuwaonee huruma, haileti mantiki! Maana ajira zinatolewa na Serikali na sekta binafai! Na siyo watumishi wa umma.
 
Watumishi tumezulumiwa mishahara nyongeza na vyeo kwa Takriban 6yrs

Sasa kupandisha madaraja kiholela utakuta watumishi wanafanana madaraja na vyeo wakati wameanza kwa nyakati tofauti

Tofauti ni kubwa mpaka watumishi mmeajiriwa mwaka mmoja kazi moja elimu moja ila mnatofautina kwa sababu za ajabu ajabu tu

Ni lazima tathimini ya kina ufanye hata kama hawataongeza mishahara sawa tu
 
Sasa mbona kuajiriwa kwenu hakuna kabisa uhusiano na kuongezewa mishahara wafanyakazi, au kupandishwa madaraja yao?

Yaani na nyinyi mnatakiwa muililie Serikali kwa wakati wenu ili iwaajiri! Lakini kutaka sisi wafanyakazi tuwaonee huruma, haileti mantiki! Maana ajira zinatolewa na Serikali ma sekta binafai! Na siyo watumishi wa umma.

Hahahahahaha aseee duuh
 
Ataongeza lakini since Ni serikali mpya hawezi kuwa na maumivu Kama ya JPM kwahiyo tusitarajie kikubwa
 
Watumishi tumezulumiwa mishahara nyongeza na vyeo kwa Takriban 6yrs

Sasa kupandisha madaraja kiholela utakuta watumishi wanafanana madaraja na vyeo wakati wameanza kwa nyakati tofauti

Tofauti ni kubwa mpaka watumishi mmeajiriwa mwaka mmoja kazi moja elimu moja ila mnatofautina kwa sababu za ajabu ajabu tu

Ni lazima tathimini ya kina ufanye hata kama hawataongeza mishahara sawa tu
Acha wivu wa kike.
 
Ivi baba yake Mzee Suluhu Hassan yu hai?Maana alikuwa Mtumishi wa Umma,amstue basi mana asijifanye na yeye Jemedali kama Hayati
 
Tusubiri tuone.......lakini jambo la
hekima ni kuwapa watu haki zao.
Vinginevyo utawala wake nao
utapimwa katika mzani,na
utakataliwa kutoka kiti cha enzi
cha Mungu Baba Mwenyezi.
 
Watumishi wa umma wanamaumivu makubwa mioyoni mwao sio siri, hata kama kipaumbele ilikuwa kumaliza kwanza mambo ya msingi kama ujenzi wa miundo mbinu, kuimarisha sekta ya afya na elimu lakini waalihitaji kuonewa huruma.

Waziri mkuu alikatisha watu tamaa kabisa pale aliposema eti kuongeza mishahara watumishi wa umma ni kusababisha maisha kuwa ghali. Jambo ambalo sio kweli maana kwa miaka hii mitano watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara na maisha yamepanda pia.

Siku hazigandi na leo ni tarehe nne na mei mosi ipo karibu, watumishi wa umma watapata faraja kama wakisikia wameongezwa mishahara yao. Swali linabaki kuwa je, mama Samia rais wa JMT ataweza kufanya maamuzi ya msingi kwa ajiri ya watumishi wa umma?
Mimi pia ni mtumishi wa umma, na kama tupo serious basi wakati huu si wakati wakutia pressure kuongezewa mishahara, bali kuwezesha madaraja kuwa katika nafasi zake kwanza. Hii serikali inaliweza iwapo watumishi pia watakuwa na sense of humour...Watumishi wa umma waache ku duplicate activities na wawe wabunifu ili kuongeza pato la taifa bila hivyo hii miradi tuliyoianza inaweza shindwa kuendelea na tukajikuta tumepata hasara mara mbili, kwakujifunga mikanda miaka yote mitano kisha tusifikie ile target ambayo ingefikiwa itaongeza uchumi zaidi ya mara kumi...Tukifikia target mishahara itaongezeka mara hata 10 kwakua miundombinu ya nchi itakuwa imekamilika...

Tatizo ni hata kwa ambayo imeshakamilika bado haijatendewa haki na watumishi hao hao wa umma, haiongezi tija...Soko la Morogoro kwa mfano, ndani ya mwezi moja limesha kuwa chafu, sakafu ni kama imejengwa 5 years ago na hapo tuna mabwana afya etc...Hivi huyo unamwongezea mshahara kwa lipi? Masinki yameshaanza kubadili rangi, for serious?

Mie nilitegemea ongezeko la ajira kwakua usafi ungefanywa kwa status ya jengo na lina implications kwenye uchumi, wauzaji wana uniform hiyo ingeongeza ajira kwa mafundi cherehani; mazao yapo kwenye angalau packages zenye kueleweka locally made na wasuka mikeka etc...Lakini wapi, no creativity watu wamehamia kwenye nyumba bora wakiwa na tabia zilezile za matopeni...Basi wangewapiga hata semina kidogo, what was a need ya kujenga hilo jengo? Kama watu wako vilevile biashara zipo vilevile kisha eti mtumishi anawaza kuongezewa mshahara, kweli watumishi wenzangu?

Hivi tunajithamini kweli? Itatoka wapi hiyo pesa ya nyongeza kama wewe hujaongeza ufanisi?
 
Back
Top Bottom