Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Duh kweli uelewa nao ni tofauti kati ya mtu na mtu....Unaangalia uchache au athari za hao wachache? Unadhani watumishi ni walimu na manesi tu kuna madaktari wanajeshi polisi n.k na huwezi kwenda kinyume na hilo kundi kwa miaka mingi ukadhani Mungu atakupa kibali cha kuongoza kwa miaka mingi. Lazima tukupeleke chato kukuzika. Kwasababu haohao unaowaita wachache ndio aenye uwezo wa kukufanyia figisu yoyote au hata kushirikiana na mabeberu kukuangamiza bila wewe kujua. Upo au haupo?
Hivi unadhani ni kazi kuchukua mapato huku na kule na kubana sekta zote ili kupelekea budget hata asilimia 95 kwa hizo sekta ? Huo sio mtihani mgumu ni uamuzi tu...
Mtihani ni kuhakikisha zinatengenezwa policies za kuweza kuinua kipato cha asilimia kubwa ya wananchi ambao wengi wao hawapo kwenye sekta za serikali...
Na kuonyesha ni jinsi gani fikra zako zilivyo unaangalia kwamba afanye kitu (sio kwamba kitu hicho ni manufaa ya nchi) bali afanye kitu ili yeye aendelee kukaa pale, fikra hizi na ubinafsi huu ndio umepelekea wanasiasa kufanya vitu vidogovidogo vinavyoonekana (short term plans) na sio vitu endelevu vyenye impact kubwa ambavyo vinachukua muda na huenda visionekane haraka (long term plans) kwa kuhofia kukosa kura/kula