Mtihani mkubwa kwa Rais Samia ni kuongeza mishahara ya Watumishi wa Umma. Je, ataweza?

Duh kweli uelewa nao ni tofauti kati ya mtu na mtu....

Hivi unadhani ni kazi kuchukua mapato huku na kule na kubana sekta zote ili kupelekea budget hata asilimia 95 kwa hizo sekta ? Huo sio mtihani mgumu ni uamuzi tu...

Mtihani ni kuhakikisha zinatengenezwa policies za kuweza kuinua kipato cha asilimia kubwa ya wananchi ambao wengi wao hawapo kwenye sekta za serikali...

Na kuonyesha ni jinsi gani fikra zako zilivyo unaangalia kwamba afanye kitu (sio kwamba kitu hicho ni manufaa ya nchi) bali afanye kitu ili yeye aendelee kukaa pale, fikra hizi na ubinafsi huu ndio umepelekea wanasiasa kufanya vitu vidogovidogo vinavyoonekana (short term plans) na sio vitu endelevu vyenye impact kubwa ambavyo vinachukua muda na huenda visionekane haraka (long term plans) kwa kuhofia kukosa kura/kula
 
Dogo jiongeze maisha sio kulia lia..utazeekea home na kushindwa kuhudumia familia ukikaa uasubiri ajira..graduates mko wengi hakuna serikali duniani inayoweza ajiri wote.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi waziri wa hii mifuko ni nani? Nimwandikie barua
 
Hilo linawezekana , suala ni utashi tu wa serikali! Zanzibar watumishi wameongezewa mishahara kwa miaka yote 5 ya Rais Shein na mwaka huu pia suala hilo lipo kwenye bajeti, je kwanini huku bara serikali ishindwe?
Maendeleo ya watu ndio kipimo sahihi cha maedeleo ya Taifa lolote duniani! Hivyo watumishi ni lazima sasa wakumbukwe kwani wengi sana kwa miaka hii 5 wamedumaa mno kimaendeleo!
 
Kabla ya kujibu tafuta kuelewa, siyo usome ili ujibu...Hakuna sehemu nimesema wajiongezee kipato nimesema waongeze ufanisi kwenye kazi zao ili zilete tija kisha kipato cha taifa kitapanda na wao wataweza kupata mafao mazuri zaidi ikiwemo mishahara mikubwa...Sasa unaongezaje ndiyo hapo waache kuamka asubuhi kwenda kazini na kufanya kazi kwa mazoea; wawe wabunifu...Nimetoa na mifano...
 
Kwahiyo bado hujaelewa watumishi ndiyo wakutengeneza ajira? Daah kazi kweli kweli!

Haya kazi na iendelee...
Watumishi kudai stahiki zetu na wengine kudai ajira mpya kuna uhusiano gani?

kama ningeelewa nisingeuliza kama unaelewa toa maelezo kama hueleweki unapita.
 
Am listening🤔
Watumishi kudai stahiki zetu na wengine kudai ajira mpya kuna uhusiano gani?

kama ningeelewa nisingeuliza kama unaelewa toa maelezo kama hueleweki unapita.
Huo utumishi maana yake ni nini?

Unamtumikia nani basi kama huwezi kuwasaidia kwa mahitaji yao including kuwatengenezea ajira?
 
Umesikika mtumishi wa Umma kutoka stand ya Msamvu.
 
Reactions: Ame
Umesikika mtumishi wa Umma kutoka stand ya Msamvu.
Na hapo pia pafanyieni ubunifu...Kweli vyumba vya ticket mmeviweka chini nani atapanda juu kwenye hayo maduka ya juu mliyokuwa mmepanga yawe huko?

Tutumie mali zetu tulizoachiwa urithi kwa ubunifu kama anavyotuhimiza mama, Mh. Rais wetu Samia Suluhu Hassan; hii ni ili kuongeza ufanisi na tija kwa uchumi ili hata madai yetu yapate maaana...

Uchumi una dai kuwa lazima ule ulichokizalisha na siyo ule mbegu, siyo endelevu wajameni watumishi wa umma...Tumepewa keki ya taifa kwanza ili tupate nguvu za kuwatengenezea na wenzetu walio wengi cake zao...Tuache mazoea na tuache ubinafsi...Nchi hii ni yetu na hakuna mjomba wakuja kutusaidia...

Nitakutembelea, maana nipo tu hapo jirani na wewe!
 
Am listening🤔

Huo utumishi maana yake ni nini?

Unamtumikia nani basi kama huwezi kuwasaidia kwa mahitaji yao including kuwatengenezea ajira?
Skuelewi unachobishia!!una maanisha ni heri kuwa na lundo la watumishi serikalini hata Kama wanalipwa vijisenti ambavyo havitoshi hata kula tu?!!kama unamaanisha hivo basi ww unasumbuliwa na Wivu ulioambatana na uvivu wa kufikiria

Hakuna serikali Duniani ambayo itaajili nusu ya raia wake,serikali kazi yake ni kuandaa mazingira ya watu kujiajiri na kuajiriwa private sectors! serikali haiwez kumuajili kila graduate wa chuo kikuu😲😲

Tumia elimu yako kupata pesa,ukifanya hivo hata hiyo ajira ya setrikali utaiona haina maana.
 
🙏

Na hutuweza kunielewa kwakua tupo level za tofauti...Kila la heri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…