Mtihani: Siyo kila anayeoa au kuolewa anataka Ndoa. Jadili

Mtihani: Siyo kila anayeoa au kuolewa anataka Ndoa. Jadili

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Kukaa kwenye dawati kufungua ukurasa kwa kwanza tu wa kitabu cha mtihani wa Utu Uzima. Hilo swali la kwanza. Jadili.

Hakuna kuchagua na hakuna "kweli si kweli". Yaani watu wanafunga ndoa ili kiwe nini. Kuzaa watoto? Kupata free kula/la/na? Kuwa na hadhi katika jamii? Kutimiza wajibu? Au ni ile sherehe ya harusi watu wafinye pilau na kurudisha deni la michango.

Najiandaa kusahihisha swali la kwanza.
 
Kukaa kwenye dawati..kufungua ukurasa kwa kwanza tu wa kitabu cha mtihani wa Utu Uzima. Hilo swali la kwanza. Jadili.

Hakuna kuchagua na hakuna "kweli si kweli". Yaani watu wanafunga ndoa ili kiwe nini. Kuzaa watoto? Kupata free kula/la/na? Kuwa na hadhi katika jamii? Kutimizq wajibu? Au ni ile sherehe ya harusi watu wafinye pilau na kurudisha deni la michango...


Najiandaa kusahihisha swali la kwanza.
Unawezaje kujadili kwenye chumba cha mtihani
 
Inorder to make this examination a fair assessment, I think each and everyone, including a threader should start by making an inquiry from his own parents.

Ask your father, why did he marry your mother.​
 
Ndio MM, na hiyo ndio sababu ya mvurugano huu unaoendelea .

Sababu kubwa ya watu kuoana bila kuitaka ndoa ni “Msukumo kutoka kwenye jamii” kunyooshewa vidole na kuitwa majina. Siku jamii ikibadili huu mtazamo, ndoa zitabaki kwa wale wanaozihitaji tu sio wazugaji.

Sababu nyingine ni benefits/entitlements zinazokuja na ndoa , au tunazodhani zitakuja na ndoa, nimetumia neno kudhani sababu yawezekana si kila muingia ndoani atazipata. (Tunayaona kwenye jamii)

Purely ndoa inahitaji watu wawili walioamua kuishi pamoja kwa umoja, kama si hivi hiyo “siyo”
 
Tusikilize ule wimbo wa dizasata vina unaoitwa ndoano.
"Wanandoa na binadamu wanaofugwa."
 
Kimtazamo wangu, Ndoa inafaida kubwa kwa mwanamke, mwanaume ktk Ndoa atumia Nguvu nyingi.
1.Utaangaika kutongoza.
2. Kumfikisha kileleni.
3.Kumuhudumia.
4. Kumlipia mahari
5.Upoteze mda wako kuakikisha anakua na Furaha.
Note:Ndoa Isikufanye ufanye mambo yalio nje ya uwezo wako.
 
Back
Top Bottom