Mtihani usahihishwe upya

Mtihani usahihishwe upya

Joined
Feb 13, 2013
Posts
98
Reaction score
15
Siamin kama 60% ya wanafunz ni bomu. Pia shule za serikali ndo zimeharibu balaa. Iundwe tume irudie kusahihisha mitihani mana nchi hi imekuwa ya kukomoana.
 
Siamin kama 60% ya wanafunz ni bomu. Pia shule za serikali ndo zimeharibu balaa. Iundwe tume irudie kusahihisha mitihani mana nchi hi imekuwa ya kukomoana.
Kwanini huamini kama mitahini yenyewe ya darasa la saba wanafeli mpaka wabebwe na form 2 hivyo hivyo, je ukisahihishwa upya matusi au mashairi ya mapenzi na wasiojibu kitu yakutakuwa majibu sahihi?
 
Mi nashauri wale wanaosema wamefeli sababu ya mfumo Kristo waanzishe baraza lao la mitihani.
Wasahishaji wawe majini ndio haki itatendeka. Maana wakisahihisha binadamu wataanza tena kusema huyu Sunni, huyu Mohamadia.... malalamiko kamwe hayataisha
 
Haina maana kwamba usaishaji ulikuwa na matatizo,bali majibu yaliyosaishwa hayakuwa sahihi na hii inasababishwa na mfumo wa elimu tulionao haupo sawa,tunasahau kwamba elimu na siasa ni vitu viwili tofauti!
 
ni gharama sana kusahisha tena upya. jamani inabidii tuionee huruma serikali yetu maana inamajukumu kibao. we kama unaona umeonewa appeal na kunakiasi unalipia!
 
ni gharama sana kusahisha tena upya. jamani inabidii tuionee huruma serikali yetu maana inamajukumu kibao. we kama unaona umeonewa appeal na kunakiasi unalipia!
kaka mie niko masters Open University so the issue I raised here I have made a minor research and siamin kama wat zaid ya laki mbili wapate ziro. Basi huenda ile chanjo waliopigwa ya kupunguza uwezo wa kufikir inaeanya kaz.
 
Siamin kama 60% ya wanafunz ni bomu. Pia shule za serikali ndo zimeharibu balaa. Iundwe tume irudie kusahihisha mitihani mana nchi hi imekuwa ya kukomoana.

Niliwahi kuwa mwalimu katika madaraja tofauti, katika shule na taasisi tofauti! asikuambie vilaza wameongezeka sana katika karne hii ya sayansi na teknelojia! Naamini hayo ni matokeo sahihi ingawa miaka mingi huwa wanayachakachua kuongeza ufaulu wa watoto wetu.
 
Tena sio hao tu hadi waliopata division four nao ni bomu. Wanafunzi hawasomi kazi yao kubwa kwenda disco,facebook,bbm kusoma magazeti ya udaku na kusikiliza radio mbao
 
Siamin kama 60% ya wanafunz ni bomu. Pia shule za serikali ndo zimeharibu balaa. Iundwe tume irudie kusahihisha mitihani mana nchi hi imekuwa ya kukomoana.
Hao waliochora vikatuni na kuandika mashairi ya bongo fleva nao wasahihishiwe upya??

Vipi wasiojaza kitu katika answer sheet?? Ndalichako anadai kuna shule ambazo watahiniwa woote hawajajaza kitu kwenye karatasi za kujibia walipouliza wakaambiwa watoto hawjawahi kufundishwa hayo masomo kwa kuwa hakuna mwalimu wa somo..Kwa hiyo hawa nao waundiwe tume?? kwa kodi ya nani??

Tatizo laelimu tanzania ni la kimfumo si la kimatukio kama tunavyodhani...
 
Tume mpya yoyote ikiundwa ni kodi zetu wenyewe zinatumika tena kwa kufuja, tulitizame upya wenyewe suala hili.Uongozi wetu na malezi ya wazazi na walimu yanachangia yaliyotokea, em pata picha ya zile kata K za wadogo zetu, full maFB na maTwita, hata kama wamekataliwa kumiliki simu na wazazi na walimu wao bado watakuwa nazo tu kiufichouficho, kama sio simu basi line..Halafu, motisha hakuna kwa walimu, mada za walimu bungeni zinapingwa, we unategemea nini? Hayo ndo matokeo tukatae tukubali..
 
Kwani kuna mtahiniwa kaonewa? Iundwe tume ya nini na kwa pesa zipi?
Naamini asilimia zaidi ya tisini ya watahiniwa wavevuna walichopanda hata kama hakuna waalimu wa kutosha kwa miaka minne mwanafunzi anakosa walau alama D kwa masomo matatu tuu? Tatizo wanafunzi wa kizazi hiki wana mambo mengi na wajuvi wa mambo ambayo hata hayana msingi wala faida. Utakuta mwanafunzi yuko kwenye mitaandao ya kijamii muda wote.Kama unataka kujua ukweli tafuta sample ya wanafunzi 10 uwaulize maswali yanayohusu masomo yao utaishiwa nguvu.
Asilimia kumi zilizobaki zinachangiwa na mgomo baridi wa walimu,wazazi wa wanafunzi pamoja na malezi watoto wamepewa demokrasia iliyopitiliza.
Mwisho hili ni la kwetu wote watanzania aliyefefanya mtihani,wazazi,jirani na jamii kwa ujumla tushirikiane kwani kuna wengine wanajitoa kwa kusema oo sina mtoto,ndugU aliyefeli........
 
Mi nashauri wale wanaosema wamefeli sababu ya mfumo Kristo waanzishe baraza lao la mitihani.
Wasahishaji wawe majini ndio haki itatendeka. Maana wakisahihisha binadamu wataanza tena kusema huyu Sunni, huyu Mohamadia.... malalamiko kamwe hayataisha

Kafiri ni kafiri tu !
 
Tena sio hao tu hadi waliopata division four nao ni bomu. Wanafunzi hawasomi kazi yao kubwa kwenda disco,facebook,bbm kusoma magazeti ya udaku na kusikiliza radio mbao

Hapo kwenye udaku hapoo.........!
 
kaka mie niko masters Open University so the issue I raised here I have made a minor research and siamin kama wat zaid ya laki mbili wapate ziro. Basi huenda ile chanjo waliopigwa ya kupunguza uwezo wa kufikir inaeanya kaz.

Kama kuvuja kwa mitihani kumezibwa, unategemea nini !? .........kipindi chote cha Mkapa na cha kwanza cha Kikwete, deal zilikuwa ni wizi wa mitihani !
Kuna Mkurugenzi wa Baraza alifukuzwa na Mkapa kwa 'manufaa ya umma' kwa ushiriki wake kwa hilo.
Ndalichako akaingia akajikuta hali ni hiyo hiyo, kumbe ni kada ya kati ya uongozi ndo inavujisha. Ni wazi safarii hii wamefanikiwa. Sasa picha halisi imejitokeza !
 
Niliwahi kuwa mwalimu katika madaraja tofauti, katika shule na taasisi tofauti! asikuambie vilaza wameongezeka sana katika karne hii ya sayansi na teknelojia! Naamini hayo ni matokeo sahihi ingawa miaka mingi huwa wanayachakachua kuongeza ufaulu wa watoto wetu.

huo ndo ukweli kabisa, matokeo ni reflection ya hali halisi iliopo, watoto hawana majibu ndo maana wanamchora messi..zimeanzishwa shule (majengo) nyingi bila kujali elimu si majengo tu, ndo tumefika hapa..kama jamaa alimsikia vizuri kawambwa na sababu zake utaona tatizo kubwa liko katika mfumo...unategemea nini shule haina mwalimu wa biology afu mtihani unakuja, hao wenye mwalimu tu mambo magumu..wenye maabara wanafanya mtihani sawa na wasio nayo...kuna watu walihoji ufaulu wa watoto wao darasa la saba ilhali hawajui kusoma..TUMEFIKA HAPA KWA MIPANGO NA MITAZAMO DUNI YA TULIOWACHAGUA TUKADHANI WATATUONGOZA KUMBE WANATUNYONYA
 
kaka mie niko masters Open University so the issue I raised here I have made a minor research and siamin kama wat zaid ya laki mbili wapate ziro. Basi huenda ile chanjo waliopigwa ya kupunguza uwezo wa kufikir inaeanya kaz.

Kuwa masters ya out sio hoja, nina mashaka na hiyo reseach yako maana imekupa majibu dhaifu. Ninashawishika research yako ni copy and paste. Shule ina walimu 2, bila mabara watafauluje. Kama kuna ndugu yako aliefeli mpatie tena huo mtihani aliofeli alafu msahihishie, baada ya hapo hoja jenga hoja bila kukurupuka. Haihitaji elimu ya masters katika hili jambo. Katika kufaulu population haimati,muhimu ni namna ambavo mtahiniwa kaandaliwa.
 
Siamin kama 60% ya wanafunz ni bomu. Pia shule za serikali ndo zimeharibu balaa. Iundwe tume irudie kusahihisha mitihani mana nchi hi imekuwa ya kukomoana.

warudie kusahihisha bongo fleva, katuni za mesi au matusi?

Watanzania mnajua kulaumu mlipodondikea badala ya kukata mzizi ya fitna na kusahihisha chanzo. Nchi mitaala tu hamna halagu mnataka wanafunzo wafaulu? Hawana walimu lakini mnategemea wafaulu? Hamna vitabu wala maabara ila wanafunzi wafaulu? Akili au tope hizi?
 
Yatasemwa mengi lakini mfumo wa elimu umekuwa si mzuri. Hautoi haki. Hivi mtihani unatungwa kupima kitu gani. Utatungaje mtihani ule ule kwa shule ambazo una uhakika hazikuwa na walimu, vitabu wala maabara wakati shule zingine zina walimu na vifaa vya kutosha?
 
Kama kuvuja kwa mitihani kumezibwa, unategemea nini !? .........kipindi chote cha Mkapa na cha kwanza cha Kikwete, deal zilikuwa ni wizi wa mitihani !
Kuna Mkurugenzi wa Baraza alifukuzwa na Mkapa kwa 'manufaa ya umma' kwa ushiriki wake kwa hilo.
Ndalichako akaingia akajikuta hali ni hiyo hiyo, kumbe ni kada ya kati ya uongozi ndo inavujisha. Ni wazi safarii hii wamefanikiwa. Sasa picha halisi imejitokeza !

yaani watanzania tukiandamana kisa wanafunzi wamefeli hakika tutakuwa twakosea hawa wanafunzi hawasomi kabisa we angalia mtu anaandika nyimbo unategemea huyo aje afaulu?
Mtu anaandika matusi badala ya jibu la swali huyo tutegemee nae afaulu?
Mtu anachola zombi unategemea huyo nae afaulu?
Mtu amekutwa na maandishi kwenye mikono,mapaja tutegemee huyo nae afaulu?
Mtu amekutwa na daftari ndani ya chumba cha mtihani huyo nae tutegemee aje afaulu?
Mtu kaandika matusi huyo nae tutegemee aje afaulu?

Tusiilalamikie serikali na necta sababu NECTA wao wanasahihisha,kutunga,kutoa matokeo
 
Hivi ndivyo watoto tulivyo walea sasa kila mmoja analalamika watoto,watoto,mitandao ,facebook. Wewe kama unaye mtoto na unajua maana ya mtoto weka mbali na mitandao hiyo ya kijinga
mtoto anavaa kimini toka ndani unamuona wala hukemie kesho ana zero ndo unaanza ushabiki wa kisiasa hapa kwani wewe hukuchangia hapo?, mabadiliko yanaaza na wewe mzazi - serikali then watoto= matokeo mazuri
 
Back
Top Bottom