Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa


Kimsingi nakubaliana na wewe kabisa; lakini kwa uzoefu wetu hapa Tanzania resources peke yake Human and financial havitoshi; kunahitajika pia utashi wa kisiasa, dhamira ya dhati na hatua za makusudi kabisa;

Usimamizi na ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha hii sera mpya inatekelezwa.
 
sere nzuri ya wao kuendelelea kututawala maana watoto wao watasoma hizo shule kama faiza na santi meri sisi wa kwetu za kata

ina maana wao wataendelea kututawala maana sisi tutakuwa hatuna elimu...

ntakula nao sahani moja

Hiki ndicho nachokiona, wanazidi kuweka matabaka
 
Huyu alietuwekea hawa viongozi wetu safari hii ametuweza.
 
Swaga za uchaguzi hizi!

NB:A leader who takes advantage of events to make history is a leader whose peformance leaves no history-Salary Slip wa Jamiiforums.
 
Upuuzi wa hali ya juu huu.

Rwanda wameongeza kiingereza sisi tunapunguza lugha. Katika hao rais, waziri wa elimu, katibu mkuu watoto wao wanasoma njee halafu wanawadanganya watanzania

Safi sana nafikiri tutaacha kuchekana sasa.
 
Kina Kayumba sahauni ajira baada ya shule hata kama utamaliza chuo kikuu. Tuachieni tulio na watoto english medium, maana sisi hatutaathirika. Labda tupigwe marufuku.

Hata wakipiga stop,tutaanza tena kupeleka watoto Kenya,Uganda, Rwanda, India, n.k. Soko la ajira Jumuiya ya Afrika Mashariki liko wazi kwa wanajumuiya. Kwa hakika kina Kayumba inwezekana hata kazi za houseboy na house girl hamtapata.

Kila la heri Prof. Mchome japo sijui wanao na wajukuu zako umewazingatia hadi kufikia hapa. Kiingereza ni lugha ya Dunia hata kama hatutaki.

Hata China wanapotaka kuingia soko la dunia hutumia english kwenye bidhaa zao isipokuwa zile zinazokusudiwa kwenye soko lao ndani. Nakutakia tena Prof. Mchome mafanikio lakini rudi tena mezani.
 
Sera ya kipuuzi kabisa. Tunarudi nyuma. Kiingerza hakikwepeki. Tunajifanya fanya tuuu eti mbona wachina wantumia lugha yao. Sasa kwa nini nao wanajifunza kiingereza.
 
Kufuta mtihani wa darasa la saba ni step nzuri kabisa, ila kufanya kiswahili kama medium ya kila kitu kuanzia chini hadi secondary ni kitu ambacho hata wasijaribu kufanya, tushachelewa kwenye world market, english imetawala kila kona.

Bora ngeli ianzie darasa la kwanza kabisa kwenda hadi juu, mtoto ni rahisi sana kushika lugha kuliko mtu mzima, mbona nilitupwa Kenya darasa la kwanza miaka hiyo kila mtu anaongea ngeli ndani ya miezi nikawa nawakimbiza kila somo pamoja na kwamba kila kitu kilikua kingereza..

Inawezekana sana mtoto kusoma kwa kingereza kuanzia chini kuliko kukomaa na kiswahili afu unakuja kuanza kutranslate kila terminology ukifika ngazi za juu... Ndo maana hata wanigeria wanatula kichwa, ngeli inawasaidia sana kuvuka boda hawa jamaa. Yani viongozi wa bongo, ukifikiria + wanafikiria -, ukifikiria - wanafikiria +, wako tofauti siku zote... Hii nchi niliahidi kuchukua uraia nchi nyingine endapo wataendelea na ujinga, naona wakati umekaribia.

Afu kwa nini wasiwe wanakaa na wataalam, wafanye discussions, wafanye research methods zipi zitafanya kazi... Yani wanaenda kwa kiongozi wa elimu, wanamwambia tunataka tufanye hivi, anafikiria hapohapo anatoa jibu fasta, tayari wanaandaa watu kuanza kuandika madocument ya kitakachofanywa, hamna hata kusema wafuatilie wajue njia ipi itawork.. Tunaongozwa na watu tunaowazidi akili
 
Mimi nitaungana na Mbunge Tundu Lissu kuwa watoto wangu hawatasoma hizi shule; nitawavusha mpaka ili wawe sawa na hao wa viongozi wakuu wa Serikali.

Kusema shule za binafsi zitoe elimu bure ni sawa na kusema shule hizo zitataifishwa ili kudhoofisha viwango vyao vya ufundishaji jambo ambalo halikubaliki.

Tunao mifano ya vyuo vikuu vilivyokubaliwa kupokea wanafunzi wanagharamiwa na mikopo kinachotokea sasa hivyo vyuo havipewi wanafunzi matokeo watashindwa kulipa mishahara na kuua elimu; hospitali "Desginated District Hospital" nazo shida lukuki pesa za uendeshaji hazipelekwe hivyo kufanya hali kuwa mbaya zaidi ya zilivyokuwa za kulipia
 
Duh hapa kazi ipo maana kiswahili tu chenyewe watu itabidi wakisoma maana pia watanzania wengi hatukifahamu,maneno mengi ya kisayansi yako kwa Kiswahili kama yalivyo sidhani kama hapo kitaeleweka kitu dah
 
Is it a revolution in our education system?

Nadhani suala hili linahitaji mjadala wa kitaifa wanachi waamue wanahitaji elimu ya namna gani. Kuhusu matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia naona kuna tatizo hapa. Japo mtu kusoma kwa lugha yake kuna faida, kwa mazingira ya sasa hakutasaidia taifa hili. hii ni kwa sababu idadi kubwa ya watanzania watazipuuza shule za kiswahili na kuwapeleka watoto wao katika shule zinazotumia kiingereza.

hali hii ipo hata sasa ambapo viongozi karibu wote hawasomeshi watoto wao katika public schools. wenye kipato kizuri hawafanyi hivo. hata wasion na kipato wanajitesa kwa mikopo ili watoto wao waende english medium schools.

Hatari iliyopo

Hali ya matabaka itaongezeka miongoni mwa watanzania. kwa hiyo ni heri tungeamua lungha ya kufundishia iwe kiingereza ambacho wanachi wengi wanaokipenda hasa hao watunga sera. la sivyo basi Kiingereza kipigwe marufuku kama lugha ya kufundishia kwa shule zote binafsi na za serikali. hapo tutaenda sawa.
 
kama elimu bora inapatikana shule za binafsi ni kwa nini iwe kwa kiingereza? kwani ikitolewa kwa kiswahili haitakuwa bora?
 
Upuuzi wa hali ya juu huu.

Rwanda wameongeza kiingereza sisi tunapunguza lugha. Katika hao rais, waziri wa elimu, katibu mkuu watoto wao wanasoma njee halafu wanawadanganya watanzania

Wanahakika waTanzania ni mbumbumbu
 

Kusadikika.
 
Huu ni mwanzo mwema kwa nchi yetu. Kiingereza kimetufanya watumwa katika nchi yetu. Futa kiingereza kwanza katika mfumo wa uendeshaji wa serikali. Machapisho yote ya kiserikali yawe yanatoka katika Lugha ya Kiswahili.

Andika sheria zote za nchi kwa Lugha ya kiswahili na mahakama zetu ziendeshwe kiswahili - Huu ujinga wa kiingereza utaisha na wote watajifunza kiswahili na kuwa wasomi wa ukweli badala ya wasomi wa kukalili.

Ni aibu kuwa nchi baada ya miaka 50 ya uhuru tunatumia lugha ya mkoloni kuendesha nchi - ni aibu kubwa. Kule South Africa lugha ya ki-Afrikaans - lugha ya watu wasiozidi milioni 5 inatumika hadi kutoa PHD ya uhandisi, udaktari, n.k. Lakini wataalamu waliosoma kwa lugha hiyo bado wako bora kimataifa.

Hapa Tanzania mtanzania anaona haiwezekani kusoma PHD kwa kiswahili - kifupi kama huwezi kuandika chapisho la kupata PHD kwa kiswahili huna PHD bali umenakiri PHD. Sisi kila tukisema lugha ibadirishwe watu wanakuja na madai oooh, uongozi utachukuliwa na waliosoma kiingereza!! Haya ni madahi mufilisi na ya Kisiasa tu.

Uongozi wa serikali inayoendeshwa kiswahili utahitaji Kiingereza cha kufanyia nini? Tujifunze kwa wenzetu. Lugha za kimataifa ziko nyingi, tuchague muhimu tuzifundishe, ila watu wetu wajifunze masomo yote ya msingi kwa Lugha zao. Mfano lugha za kufundisha iwe Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kichina na Kihindi.

Kazi ya kufasiri vitabu muhimu kutoka lugha mbali mbali kuja Kiswahili haiwezi kugharimu zaidi ya Sh. Billioni 200. Hizi fedha tunazo tena hatuhitaji kuomba senti tano. Huu utumwa wa kujitakia tuachane nao. Naunga mkono hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…