Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Binafsi naona ni jaribio la kushughulika na mkakati ulioshindwa.Huwezi kujaribu kuiga China Urusi nk,huku ukiwa masikini kiasi hicho.Hao wanafunzi utakao waburuza toka msingi mpaka form four bila mchujo wowote lazima utegemee kuongeza umbumbu nchini

Waalimu wakiaminiwa na kuthaminiwa ikiwa ni pamoja na kulipwa mshahara mzuri umbumbumbu hautakuwepo hata bila mitihani
 
Hii nchi imeoza na serikali yake. Tatizo wanaotoa maamuzi ni wazee wa miaka 70 na kuendelea ambayo wanashikilia madaraka utafikiri nchi yao. Huu ni upuuzi Kikwete na serikali yako acheni kuliangamiza taifa.

Mnakuza ujinga badala ya kuondoa ujinga. Hope serikali mpya itafutilia Bali huu ujinga. Eti kiswahili lugha ya kufundishia kuongea majumbani na Mitanni inatosha mashuleni twende na wakati Kiingereza ni lugha mama kwa mataifa mengi.
 
KipimaPembe,

Watu wanaandika siasa tu? wachina Microsoft ni ya kwao? warusi benzi ni za kwao? lakini wauza microsoft na benz wanalazimika kutengeneza kwa ajili ya masoko hayo ili wauze?

Nenda Turkey, china, russia, france, germany Eastern europe yote? hujui lugha yao hata darasani kwao huingi.
 
Last edited by a moderator:
Yani kampeni za kisiasa zimekua kama promosheni za mitandao ya simu.
NINA UHAKIKA RAIS AJAYE HATA ATOKE CCM AU AWE RIZ1 atapinga tu huu ujinga.
 
Nimekoswa koswa mfumo huu wa mazingaombwe
Tuandae kupokea taifa la mambummbu
 
Hongera sana Rais kwa mipango yako ya kuboresha elimu. Pamoja na hongera hizo ningekushauri kupembua kwa undani kuhusu matokeo ya maamuzi yako. Nasema hivi kwa sababu, mara nyingi maamuzi na mipango yako hayajaleta malengo uliyoyatazamia, kwa mfano sera yako ya kilimo kwanza...

kadili yangu mimi nadhani kuhuwa umejiandaa vilivyo kuifanyia kazi sera hiyo ndio maana hukuweza kugundua kuwa unapoongeza uzalishaji, lazima uongeze nguvu katika kutafuta masoko. Watanzania wengi wameadhirika sana kwa kilimo na wengine kukata tamaa ya kujishughulisha na kilimo baada ya kulazimika kuuza mahindi kwa bei ya sh 500 kwa dumla lenye kilo nne.

Kwa upande wa elimu kutumia kiswahili kunamanufaa mengi yakiwemo kuuenzi utamaduni wa kiswahili na kukikuza kwa msamiati na matumizi. Hata hivyo usipokuwa makini, unaweza au kupoteza fedha nyingi sana kwenye mikakati na mipango ambayo mwisho wa siku utaona haiekelezeki, au elimu ya Tanzania inaweza kushuka kwa kuzalisha wahitimu watakaokuwa chini ya viwango.

Mataifa yaliyoendelea wanatumia lugha zao kufundishia, lakini wameweka pia mikakati madhubuti ya kuhakikisha wahitimu wao wanajifunza kikamilifu lugha mbalimbali zinazoweza kuwaongezea uwezo, kikiwemo kiingereza, je watanania tutaweza kama hata baada ya kujifunza kwa kiingereza kwiaka zaidi ya sita bado hatukuongei ipasavyo?

Tukitaka kufanikiwa katika hilo, basi pamoja na jitihada za kuanzisha shule katika kata mbalimbali hapa nchini, tukazane kuongeza uwezo katika kupata wataalamu watakaokidhi mahitaji ya kukiandaa kiswahili kwa ajili ya kufundishia, na hata kukiimarisha kiswahili kwa wakufunzi. Pengine hili linaweza kuonekana sio tatizo kwa sasa kwa vile wahadhili wengi wanatumia kiswahili,

lakini ukweli ni kwamba kunaudhaifu mkubwa upande wa usanifu wa lugha hii. Ombi langu ni kuwa watanzania tubadilike na kuwa wabunifu badala ya kuendelea kuiga yale tunayozani ni mazuri kutoka kwa majirani.
 
Ndio hawa the so called "viongozi" wa Tanzania wanaingamiza elimu nchini kila kukicha kwa madai kwamba wanaiboresha na wakati huo huo watoto wao wote hawakanyagi katika shule hizi. Huu ni ujinga wa hali ya juu wa kutaka kufundisha darasa la kwanza hadi la O'level kwa kiswahili tena bila mitihani ya Taifa kwa miaka 11. Hili lipingwe na wadau wote wa Elimu nchini kwa nguvu zote.

Upuuzi wa hali ya juu huu.

Rwanda wameongeza kiingereza sisi tunapunguza lugha. Katika hao rais, waziri wa elimu, katibu mkuu watoto wao wanasoma njee halafu wanawadanganya watanzania
 
wakifuta kiingereza na kutaka lugha ya kiswahili itumike, binafsi sina tatizo na hilo wacha tu elimu hiyo iendelee, lakini watoto wangu wote watasoma shule za international.
 
its kiswahili language and not Swahili language

Kiswahili = noun
Swahili = adjective
Swahili language is correct because SWAHILI as an adjective modifies the noun LANGUAGE.
KISWAHILI stands alone as a noun.
 
Watanzania wanaumwa sana. Sijui wanawaza nini? Walipunguza viwango vya ufaulu sasa wanazika elimu ya msingi! Na Rais anatuambia kuwa hii sera mpya itaongeza ufanisi na kulikomboa taifa ifikapo 2025! Anasahau kuwa tuna miaka 9 tu kufikia 2025. Watu wakiwepo maprofesa waliosoma wakapiga makofi. Mimi naona sera hii itatuzamisha kabisa ifikapo 2061.
 
Du ila hii kuondoa mitihani ya michujo kama ya darasa la saba sio suluhisho la kuimarisha misingi ya elimu hapa bongo
 
vichwa nazi wanapenda kukopi na kupest bila kuangalia hali halisi ya nchi yetu.
 
Mjenda Chilo,

Naamini ni moja kati ya maamuz kibinafsi sidhan kama yataleta tija. Nafananisha sawa na maamuz mabovu kabisa ambayo wakati ule Waziri Mungai alipotoka baada ya kufuta michezo mashuleni na kufuta mfumo wa shule za Ufundi.

Madhara yake hadi leo yapo, Tanzania imeendelea kusuasua kwenye michezo na tasnia ya vijana wenye vocational training ilishuka. Awamu ya nne ilipoingia ilirekebisha mfumo huo na kurudisha michezo na shule za ufundi kama zamani. Waligundua makosa.

Naamini hata hili la GPA, elimu mfululizo miaka11 nalo litabadilishwa tu awamu ya tano ikija, naamini havitakuwa na tija kwa elimu yetu
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii ni kama gheto la masela-Godbless Jonathan Lema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…