Hongera sana Rais kwa mipango yako ya kuboresha elimu. Pamoja na hongera hizo ningekushauri kupembua kwa undani kuhusu matokeo ya maamuzi yako. Nasema hivi kwa sababu, mara nyingi maamuzi na mipango yako hayajaleta malengo uliyoyatazamia, kwa mfano sera yako ya kilimo kwanza...
kadili yangu mimi nadhani kuhuwa umejiandaa vilivyo kuifanyia kazi sera hiyo ndio maana hukuweza kugundua kuwa unapoongeza uzalishaji, lazima uongeze nguvu katika kutafuta masoko. Watanzania wengi wameadhirika sana kwa kilimo na wengine kukata tamaa ya kujishughulisha na kilimo baada ya kulazimika kuuza mahindi kwa bei ya sh 500 kwa dumla lenye kilo nne.
Kwa upande wa elimu kutumia kiswahili kunamanufaa mengi yakiwemo kuuenzi utamaduni wa kiswahili na kukikuza kwa msamiati na matumizi. Hata hivyo usipokuwa makini, unaweza au kupoteza fedha nyingi sana kwenye mikakati na mipango ambayo mwisho wa siku utaona haiekelezeki, au elimu ya Tanzania inaweza kushuka kwa kuzalisha wahitimu watakaokuwa chini ya viwango.
Mataifa yaliyoendelea wanatumia lugha zao kufundishia, lakini wameweka pia mikakati madhubuti ya kuhakikisha wahitimu wao wanajifunza kikamilifu lugha mbalimbali zinazoweza kuwaongezea uwezo, kikiwemo kiingereza, je watanania tutaweza kama hata baada ya kujifunza kwa kiingereza kwiaka zaidi ya sita bado hatukuongei ipasavyo?
Tukitaka kufanikiwa katika hilo, basi pamoja na jitihada za kuanzisha shule katika kata mbalimbali hapa nchini, tukazane kuongeza uwezo katika kupata wataalamu watakaokidhi mahitaji ya kukiandaa kiswahili kwa ajili ya kufundishia, na hata kukiimarisha kiswahili kwa wakufunzi. Pengine hili linaweza kuonekana sio tatizo kwa sasa kwa vile wahadhili wengi wanatumia kiswahili,
lakini ukweli ni kwamba kunaudhaifu mkubwa upande wa usanifu wa lugha hii. Ombi langu ni kuwa watanzania tubadilike na kuwa wabunifu badala ya kuendelea kuiga yale tunayozani ni mazuri kutoka kwa majirani.