Malalika
Mosi, "Serikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025" - Dibaji ya Sera.
Naona waliotunga hii sera walikuwa katika njozi nzito, leo ni 2015, sera hii izalishe Watanzania wenye maarifa na kuwezesha uchumi wa nchi kuwa wa kati ndani ya miaka 10 ijayo. Uchumi wenye nguvu sawa na uchumi wa Afrika Kusini, Nigeria, Malaysia, Brazili, n.k
Pili, li kuthibitisha ya kwamba wamebugi vibaya sana, hata maana ya vifupisho wameshindwa kuandika kwa Kiswahili - lugha ya kufundishia inayopendekezwa na sera. Mfano CA - Continous Assessment, na URT - United Republic of Tanzania.
Tatu, sera hii imefuta sera nne kwa pamoja. Kwa mashaka makubwa kabisa, je mambo yalioainishwa ndani ya kurasa 68 yatakuwa na nguvu kufidia ya sera nne zilizofutwa?
Nne, sera ya elimu iliyofutwa iliandikwa mwaka 1980, ikaanza kutekelezwa mwaka 1995 (miaka 15 baadaye) kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, je tafiti zilizofanywa zimeonyesha, kadiri ya uchumi wetu unaosusua, sera hii itaanza kutekelezwa lini?
Tano, je miundombinu yetu inawezesha kufanya mageuzi makubwa katika Elimi - kubadili lugha ya kufundishia katika ngazi ya sekondari? Ifahamike idadi kubwa ya shule za msingi hazina madawati, wananchi wamelezimishwa kujenga madarasa ya shule za sekondari za Kata, nyumba za waalimu, na maabara.
Nasikitika sana pale wasomi wanalewa siasa na kukurupuka, bila ya kupima madhara ya maamuzi yao. Sera hii ni ishara ya wazi ya makosa makuu serikali inayowafanyia Watanzania.