Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Mtihani wa Darasa la Saba wafutwa

Ni rahisi sana kumharibu mwanadamu kuliko kumjenga kwenye elimu na kujielewa
 
Ni shida kuamini kuwa mtihani ndo elimu.

Unajitoa ufahamu bure. Ili ujue kuendesha gari lazima utapewa mtihani wa kurudisha reverse huku mawe yamepangwa. Ukiendesha bila kugonga unaonekana umefuzu. Mitihani ni muhimu sana kwa scenario hiyo ndogo tu. Kichwa hakiwez kuchaji kama mitihan hamna. Ndiyo maana shule makini hutoa mitihani kwa wanafunzi wake mara kwa mara.
 
MKWANO

Mkuu ni vema kuwa na lugha za staha unapojadili ilikupata elim ambayo labda hauyo kwa mapana yake. Mie sio wa BRN Mkuu.

1. Nikueleze kidogo kuwa ili utengeneze mtaala unaouhitaji cha kwanza ni kuwa na sera. Sera ndio kwanza imetungwa kinafuata mtaala then syllabi na baadaye mwl anaexcute kwa maandalio yake na actual teaching.

Sasa wewe unaleta kimbelembele ya ujuaji mwingi kwa madesa ya darasani! Pata muda bwanamdogo soma sera, baada ya hapo kuwa na mwangaza wakujadili hayonulotaja yatakapo kuja kwa wakati wake!
 
Last edited by a moderator:
Afadhali umenielewa mkuu. Kwa hiyo hapo mtu ukitaka kumponya mwanao inabidi umsomeshe nje kuanzia chekechea!

Samaritan;
Penda usipende uzazi wa majira unakulazim kama weye ni mwoga wa kulea majambazi na makahaba. Wawili toshaaa. Kama weye upo lile kundi la kuoa uwezavyo bora umelipa mahari basi, muda si muda mtaanza Oh! wenzetu wanajifanya wamesoma etc.

Toka chekechea hadi chuo kikuu. Mmesema elim ni bure. Sawa, lakini angalia matokeo ya kidato cha 4. Bila Private mwanao ka wa kiume mnunulie bunduki aende amboni caves. Ka wa kike mpe sabuni aende K' makaburini akamulikwe na taa za magari kwa wateja na Ohio.
 
Upuuzi wa hali ya juu huu.

Rwanda wameongeza kiingereza sisi tunapunguza lugha. Katika hao rais, waziri wa elimu, katibu mkuu watoto wao wanasoma njee halafu wanawadanganya watanzania

Hapa nakubaliana na wewe 100%. Huu ni ulaghai mbaya sana kwa Taifa. Hapa panahitaji uelewa kidogo tu kugundua chujio hili ni la ubaguzi na haifahamiki litalifikisha wapi Taifa letu la Tanzania.
 
mangatara
Mkuu acha kabisa, unajua kuna kipindi hata kama hawafaulu vizuri lakini walikua wanapokelewa angalau kwa kiwango cha elimu ya juu huko nje, sasa kwa hali hii ya sasa mtoto wako akisoma kwa mfumo unaopendekezwa wa kutumia kiswahili hadi tuje tukae sawa ina maana aidha mtoto asome hapahapa na ukubaliane na matokeo au umpeleke akasome nje kuanzia hatua ya mwanzo kabisa.

Serikali yetu haijawahi kuja na kitu ikakipa uzito unaostahili....leo utasikia MKURABITA, bado haujatulia unasikia KUKUTA, wakati unajiandaa kuuelewa wanaongelea nini unaambiwa Big Results Now (BRN) sasa hii ya elimu naona ni BRN......
 
Last edited by a moderator:
Malalika

Sina imani kama hata wewe umesoma sera zaidi ya kuisikia au kuletewa mezani hata bila kuijua, kama hujui omba ushauri wa Kisheria, kwa Elimu yangu ya darasa la nne enzi za Mwl, ni kwamba project ya kitaifa kama hio inatakiwa kufuata hatua zote (Project cycle) ili ifanikishe malengo, sasa nyie mlipofikia hapo ni stage ipi?

Who is the stakeholder if not just pressure from somewhere else? Hiyo sera watanzania Wanataka kwa sasa? Kana sio kukurupikia mambo then yanawashinda kutimiza, pia usiwazie hako kaelimu Kako Bali mstakabali wa Taifa na vizazi vijavyo
 
Last edited by a moderator:
Samaritan

Yaani sasa umefunguka macho, angalia usilale tena.

Serikali yetu haijawahi kuja na kitu ikakipa uzito unaostahili....leo utasikia MKURABITA, bado haujatulia unasikia KUKUTA, wakati unajiandaa kuuelewa wanaongelea nini unaambiwa Big Results Now (BRN) sasa hii ya elimu naona ni BRN......

Ni namna ya kukunyima uwezo wa kufikiri, ukipata nafasi utaona hiyo kitu ilofichika humo. Nachogopa ni jinsi ambavyo serekali imekuwa kama haiamini kuwa itakuwepo tena milele. Ndo maana wamehamua kuharibu kiila kitu.

Barabara inatengenezwa kabla haija kabidhiwa ati ina mashimo. Jamani ni nini hii?

Form iv akiona mzungu anakuja anakwepa njia, huku mnasema ati tutashindana ka EAC. Ni vituko vya mwaka, labda siye tubaki kufagia barabara.
 
Last edited by a moderator:
Sina imani kama hata wewe umesoma sera zaidi ya kuisikia au kuletewa mezani hata bila kuijua, kama hujui omba ushauri wa Kisheria, kwa Elimu yangu ya darasa la nne enzi za Mwl, ni kwamba project ya kitaifa kama hio inatakiwa kufuata hatua zote (Project cycle) ili ifanikishe malengo, sasa nyie mlipofikia hapo ni stage ipi? Who is the stakeholder if not just pressure from somewhere else?

Hiyo sera watanzania Wanataka kwa sasa? Kana sio kukurupikia mambo then yanawashinda kutimiza, pia usiwazie hako kaelimu Kako Bali mstakabali wa Taifa na vizazi vijavyo

Haya mkuu nimekuelewa. Nashukuru kwa elimu ulonipa.
 
Malalika

Mkuu wa nchi kasema sera hii italikomboa taifa ifikapo mwaka 2025, au miaka 9 tu toka alipoizindua. Sidhani kama yeye ameisoma hii sera.
 
Last edited by a moderator:
mangatara

Tunaongea kama utani lakini nikipiga picha miaka mitano, kumi ishirini ijayo huko mbele naona giza. Japo mie sio mtalaamamu sana wala uelewa wangu huenda usiwe wa kiwango cha kutoa ushauri fasaha lakini inabidi ifike mahali tuwe na sera ya nchi tuwe na dira tuwe na malengo ya muda mrefu na ikiwezekana yakishapitishwa iwepo kwenye katiba kabisa kwamba haijalishi ni nani au chama gani kinaingia madarakani,

kazi yake inakua ni kuhakikisha kwamba katika kipindi kitakachokuwepo madarakani kinasaidia kutekeleza mambo yanayotuwezesha kuyafikia hayo malengo ya taifa.

Kama ulivyosema huo mfano, sisi wenyewe tuliojifunza kiingereza kwa kiswahili hadi leo hatujiwezi kwenye ushindani sasa watoto wetu itakuaje na mfumo huu mpya?
 
Malalika

Mosi, "Serikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025" - Dibaji ya Sera.

Naona waliotunga hii sera walikuwa katika njozi nzito, leo ni 2015, sera hii izalishe Watanzania wenye maarifa na kuwezesha uchumi wa nchi kuwa wa kati ndani ya miaka 10 ijayo. Uchumi wenye nguvu sawa na uchumi wa Afrika Kusini, Nigeria, Malaysia, Brazili, n.k

Pili, li kuthibitisha ya kwamba wamebugi vibaya sana, hata maana ya vifupisho wameshindwa kuandika kwa Kiswahili - lugha ya kufundishia inayopendekezwa na sera. Mfano CA - Continous Assessment, na URT - United Republic of Tanzania.

Tatu, sera hii imefuta sera nne kwa pamoja. Kwa mashaka makubwa kabisa, je mambo yalioainishwa ndani ya kurasa 68 yatakuwa na nguvu kufidia ya sera nne zilizofutwa?

Nne, sera ya elimu iliyofutwa iliandikwa mwaka 1980, ikaanza kutekelezwa mwaka 1995 (miaka 15 baadaye) kutokana na hali ngumu ya kiuchumi, je tafiti zilizofanywa zimeonyesha, kadiri ya uchumi wetu unaosusua, sera hii itaanza kutekelezwa lini?

Tano, je miundombinu yetu inawezesha kufanya mageuzi makubwa katika Elimi - kubadili lugha ya kufundishia katika ngazi ya sekondari? Ifahamike idadi kubwa ya shule za msingi hazina madawati, wananchi wamelezimishwa kujenga madarasa ya shule za sekondari za Kata, nyumba za waalimu, na maabara.

Nasikitika sana pale wasomi wanalewa siasa na kukurupuka, bila ya kupima madhara ya maamuzi yao. Sera hii ni ishara ya wazi ya makosa makuu serikali inayowafanyia Watanzania.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa nchi kasema sera hii italikomboa taifa ifikapo mwaka 2025, au miaka 9 tu toka alipoizindua. Sidhani kama yeye ameisoma hii sera.

Mkuu sera ni ramani itakayoonesha unapotaka kwenda ni muhim kanisa, lakini kama huna nia ya kwenda unapohitaji kwenda hata uwe na sera ya wino wa dhahabu kamwe huwezi fika inapotaka kwenda!

Kuna baadhi ya maeneo inejieleza vizuri mahali pengine mfn. matumizi ya kiswahili ktk ufundishaji unahitaji mjadala mpana zaidi.
 
majanga!! mbona anampa mzigo rais ajaye na mawaziri wake, iam still loading 2 understand the new education system!
 
changamoto ya serikali ni kitokutaka kushirikisha wadau wote ktk mambo muhimu kitaifa km sera hapa kuna wadau mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa mashirika yasiyo ya kiserikali wasomi wa sekta mbalimbali na hata wananchi wa kawaida,

viongozi wanadhani wakishajifungia kwenye warsha makongamano na kula visambusa na kupeana mabegi na kalamu inatosha ni waalimu wangapi wa shule za misingi wameshirikishwa utatungaje sera bila kuhusisha midahalo kwenye taasisi za elimu za juu? wanafunzi na wahadhiri watoe maono yao elimu ndiyo misingi ya yote
 
Nadhani kuna mambo ya kawaida sana lakini kwa umbumbu wetu tunashindwa kuelewa..

Hivi wakisema elimu ya msingi iwe miaka 11 then watoto wakafundishwa na waalimu wenye certificate darasa la kwanza had la saba wenye degree na diploma wakafundisha la nane had kumi kuna tatizo gani?

Au kimebadilika nn? Elimu itabak kama ilivyo kwa kiasi kikubwa mabadiliko ni majina ya madarasa tu

Sent from my BlackBerry 9720 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom