Majanga,
Najiuliza tu ma-housegirl... mimba nk miaka saba tu shughuli sasa unaweka mpaka form four.., saidia fundi watapatikana wapi? Mi mawazo yangu ni kuwa na wasomi haswa na kuwa vocational skilled labour force haswa.
Hivi ni shule gani za msingi cum secondari zitakazoweza kuwafundisha elimu ya ufundi haswaaa. Vifaa watavipata wapi?Bunsen burner tu wameshindwa kununua je wataweza kununua lathe machine?
Nilifikiri elimu ya msingi iwe mpaka darasa la tano, then unakuwa na wale wanaoenda michepuo ya vocational na wale wanaoendelea na pure shule hivyo hivyo mpaka secondary, na iwe compulsory.
Tatizo letu sasa tuna wasomi wavaa tai wasiojua kufunga tai. Graduates weeengiii lakini weupeeee , matokeo yake wachina wanakuja na nyundo za kunyoosha magari na wanapiga hela ya hatariii.
Dah, yani mi hata sielewi dunia watakayoishi watoto wetu.