Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

Mtanzania

Huku nilipo wasaa wa kuja kuchangia mara kwa mara unakuwa mgumu sio kama nilivyokuwa UK. Mzee Kifimbo amekuja juzi juzi tu kwenye hii bodi bado ana mengi ya kujifunza maana mpaka sasa anachofanya ni kuleta burudani bodini. Ndio maana hoja zake nyingi ni Yebo Yebo hana la zaidi.

Mzee Kifimbo

Endeleza burudani kwenye hii topic; siasa tu bila burudani inaweza kufanya mtu upasuke kichwa na kukata tamaa.

Mpendakwao, Lunyungu et al

Huyu Mzee Kifimbo hajui analoongea; ningempa heshima sana kama angalikuwa mkweli lakini anapoteza muda wake mwingi sana kubahatisha mambo asiyoyajua. Nawashauri endeleeni kusoma burudani yake humu bodini akishapata uzoefu wa kutumia na keyboard na kuchambua mambo ataanza kutoa hoja za msingi za kujenga taifa.
 
wewe kifimbo na wenzako wote wa misheni town hapo UK acheni uozo huu . Mtakuwa lini ? kaeni mtunze familia baada ya kuosha masufuria badala kuwagawa watanzania wa u DP na u CCM

Wewe samvulachole wewe hebu tulia bwana tukate issues hapa . Msije niudhi nikaanza kuwamwagia mambo yenu bure hapa mkaniona mbaya kumbe mnataka ubaya wenyewe .Mwacheni awe DP na CCM at the same time maana CCM hawana maana hata mara moja .Mkitaka issues zenu za CCM ondokeni hapa nendeni kwenye vikao vyenu hapa hakuna mambo ya vyama .
 
SHEKHE LUNYUNGU hakuna ishu ya kukatwa hapa

wenye ishu ni hao akina MASATU na mwenzie KYOMA....sasa sisi tuna taizo ni huyu GESTAPO maana ukisema ni KGB itakuwa unamsingizia

Mbwaya zaidi nilikuwa sijui kama jamaa ni PADRI..haya iweje padri anakuwa mwongo?

Makubwa haya...maana naona bora huo ukatibu akapewa huyo PINTO mara mia tukajua moja kuliko huyu Mtu wa MUNGU ambaye anataka kila kitu..CCM yuko, UT yumo, DP yumo, KANISANI yumo, UBALOZINI nako anataka kushindana na hawa waheshimiwa hapa chini

img_7445.jpg


Makubwa haya
 
Yebo yebo.
UNAJIFANYA HAUKO UK? akili zako zina matatizo huko nyuma na sehemu mbali mbali unachangia na kutoa habari za ndani za jumuiya ya U.K ambazo mtu asiyehusika na jumuiya hawezi kujua.
umetetea sana sherehe za muungano na ukajichanganya kutaja hadi wajumbe waliohudhuria sherehe hiyo na kumjibia Abuu Faraj na tuhuma za Chombeza kampuni ya mkobani wameweka website fake www.chombeza.com.
unamdanganya nani? padri mzima unadanganya hauko UK?


Mzee Kifimbo

Ngoja nikuridhishe...maana naona uwezo wako wa kufikiri ni 0, yaani ZERO kabisa....Haya ni hivi...Niko UK nimefungiwa jela kifungo cha maisha siwezi kutoka mpaka siku yangu ikifika nitakufa nikiwa UK...umenipata wangu?...

Lunyungu

Hawa either wametumwa hapa au wana matatizo...yaani wako nyuma sana...kifikra, kimawazo, kimtazamo, kiakili, kutafakari n.k yaani akili zao naona sio nzuri.

Damn...poleni sana.
 
Kifimbo
Kwa umri wako , your looks , heshima ya kuwa na mke na watoto , maneno haya ni ya kipuuzi hayafai . Umesema wewe si mwanachama wa Chama chochote bado unamsakama Yeboyebo wana CCM si wako basi wamuulize .Wewe unaumia wapi kama si mwana CCM ?Fauls ngapi wana CCM wamezicheza na wanazidi kucheza mbona sijawahi kukusikia unasimama na kupayuka namna hii . Tafadhali angalia familia yako achana na tabia hizi za mitandao. Tumia huu muda wako mzuri kuwapeleka wanao swimming pool badala kufanya unavyo wafanyia .Ona aibu tafadhali .Mambo yenu ya CCM hapa si mahala pake.Nenda CCM UK ana Reading tuache sisi tukate issues hapa .
 
Kifimbo eeh ! aacha Wivu! Noma Mwana CCM kumuonea kijicho mwenzie

This is just to advise you. Inaoenakana wazi kuwa unashida binafsi na yebo yebo. Maana unajidai kupose kama Mwana-CCM, lakini evidence zote hazionyeshi hivyo. Unadai kuwa Mtikila amefanikiwa kumpenyeza SHUSHU wake , utajuaje kuwa huyo alikuwa KADA WA CCM aliyepenyezwa DP ?

Ushauri wangu ni huu kama wewe ni CCM then malizaaneni huko huko msituletee humu JF. Maana tone ya malalamiko yako yana tuelement twa kawivu fulani kama siyo kachuki fulani. Maana kama Yebo Yebo ni shuhuhu, sijui kina Lamwai walio kuwa NCCR wakajiunga CCM na kutupiwa mfupa wa ubunge wa kuteuliwa ni nini. Acheni huyo Bwana mdogo naye ale vyake.

Mtikila na DP waalipata usajili wa kudumu baada ya kukubali kwenda Zanzibar hivyo hiyo line ya polarising imepitwa na wakati.

Kifimbo . have a nice Time

Kigumu Chama Cha Mapinduzi
 
Wanabodi,
Mnajua huyu Kifimbo ka raise hoja moja kali sana!

Hivi kweli huyu Mtikila kufurahia kifo cha Nyerere hadharani alikuwa na akili timamu kweli?...
 
uanachama wa Yebo yebo DP uko wazi kabisa mtafute mtikila atakuambia. katika DP mchungaji Mtikila alikuwa na wadhifa wa Uchungaji na yebo yebo ni padri kazi anayoifanya hadi sasa. na hakuwa mwanachama wa kawaida alikuwa kiongozi mwandamizi, huyu Yebo yebo alikuwa akigawa pipi siku Mwalimu Nyerere alipofariki, leo yeye ndiye wakufanya sherehe ya kumuenzi mwalimu Nyerere? YEBO YEBO acha hadaa.

Nafikiri mwenyewe inabidi aje alijibu hili?
 
waache this is pure Drama

kuna jambo humu


Niliwambieni Mzee Kifimbo analeta burudani kwenye bulogu. Mwacheni aendelee lakini kama alivyosema Lunyungu wanae wanakosa nafasi yake ya kupelekwa Swimming Pool.
 
Wanabodi,
Mnajua huyu Kifimbo ka raise hoja moja kali sana!

Hivi kweli huyu Mtikila kufurahia kifo cha Nyerere hadharani alikuwa na akili timamu kweli?...


Mkandara,

Unajua Mtikila kuna siku nyingine ukisikia vituko vyake utasikitika au kuvunjika mbavu...lakini pia kuna majungu mengi sana yanalorushwa na system dhidi yake. Hili la kugawa pipi...wala sishangai maana alimchukia Nyerere sana kwa sababu ya Muungano na U-CCM wake wa damu.
 
Yebo yebo,

Kumbe mtani wangu wa jadi?.....haya baba nimekupata vizuri sasa hivi.

Huyu Mtikila majuzi nilipokuwa Bongo tulimfuata na jamaa yangu mmoja anaitwa Raphael Chobuyaga ambaye ni mkereketwa wa kutupa. Huyu jamaa ni Mjamaa damu na kesha kwenda TLP lakini mawazo yake yanawatisha wote hawa jamaa. Mtikila na Shayo wote wameingia mitini kwani hoja za huyu bwana zinafunga kabisa Ulaji kwa viongozi.
Kutokana na hayo madogo tu niliyoweza kuyaona nimegundua kuwa hakuna MWANASIASA bongo kabisa wote wanatafuta ulaji na kinachofanyika ni kila mmoja wao kutafuta nafasi yake ktk Ulaji.

Mtikila hakumpenda Nyerer kwa sababu nyingi zaidi ya Muungano na haiwezekani mtu kufurahia kifo cha Nyerere wakati Muungano bado umesimama. Sherehekea kifo cha Muungano na sio kifo cha mtu ambaye ni baba wa Taifa. Hii inanipa picha mbaya sana kwa huyu Mchungaji kwa sababu kwanza hailingani na imani ya dini yake.
Haya ndio ya Bush kusherehekea kifo cha Saadam hali yeye leo hii ameua ama amesababisha vifo vya watu wengi kuliko Kiongozi yeyote ndani ya nchi ile.
 
Yebo Yebo,
Chuki za Mtikila kwa Nyerere hazikuwa ideological au kwa sababu ya Mwungano. Niliwahi kuongea na Mtikila wakati mmoja nikimdadisi nikagundua kuwa ana husuda/wivu kwa akili na kisomi alicho nacho Nyerere. Hence chuki zake. Haya ya Mwungano, na kwamba Nyerere katoka Burundi yalikuwa ni baibui tu ya kuficha ukweli wa hisia zake.
 
Yebo Yebo,
Chuki za Mtikila kwa Nyerere hazikuwa ideological au kwa sababu ya Mwungano. Niliwahi kuongea na Mtikila wakati mmoja nikimdadisi nikagundua kuwa ana husuda/wivu kwa akili na kisomi alicho nacho Nyerere. Hence chuki zake. Haya ya Mwungano, na kwamba Nyerere katoka Burundi yalikuwa ni baibui tu ya kuficha ukweli wa hisia zake.


Duh...Jasusi mimi naona Mtikila akuchezea akili kwa sababu katika wasomi wote pale bongo kwa nini Nyerere? Au ana tabia ya wivu wa kuvuka mipaka.

Mimi nilihisi ni kwa sababu ya muungano hasa kwa sababu niliwahi kusikiliza tapes zake miaka ya 90's na kwenye hizo tapes alikuwa akigusia muungano tu na jazba inakuja...nikahasi Muungano ndio unamkereketa zaidi.
 
Yebo Yebo,
Nyerere alikuwa kiongozi, na Nyerere alifanikisha mengi kukiwa pamoja na Mwungano. Mtikila hakumaliza hata chuo. Hata huo upadri alijipachika. Hakuwekewa mikono na kanisa lolote. Pia aliniambia aliwahi kufanya kazi za ukandarasi Zanzibar, lakini sikuelewa kilitokea nini huko kiasi kwamba akauchukia mwungano. Labda sikuwa mdadisi vya kutosha.
 
Mkandara.

Asikuburuze huyu Yebo Yebo ndio kiongozi Mwandamizi wa Mtikila, alijuaje hizo Tapes za 90s?
Kwa vile una contact za Mtikila fanya home work kumuuliza jina la katibu wa Jumuiya ya WaTanzania U.K na mwenyekiti wa CCM-Reading ambaye ndiye yebo yebo humu. jibu atakwambia ni kiongozi wake na alifanya nae kazi nzuri tu. huyu ndiye aliyekuwa akiratibu mikutano ya Mtikila na kulazimisha wananchi tumsukume kwenye gari Mtikila.

DR.Who.
Drama anacheza Yebo Yebo kwa kuwa mwanachama wa vyama viwili kwa wakati mmoja, na mtu aliyemfanyia sherehe wakati anakufa leo anadanganya kuwa system ndio ilimtungia Mtikila na anataka kutuzuga wananchi kwa kuandaa sherehe ya Mwalimu-UK. Yebo Yebo hilo haliondowi dhambi zako na Mtikila kama unataka kawaombe radhi familia ya Mwalimu Nyerere. kutufanyia sherehe ya Mwalimu UK, huku pipi mligawa Ilala-Dar-es-salaam nendeni huko huko mliko gawa pipi mkaandae sherehe.

Lunyungu.

sielewi unasema nini? hakatazwi mtu kuwa Chadema au DP kwenye umoja ila awe wazi na arudishe kadi ya chama kimoja. utaratibu wa kujiunga kwenye vyama ufuatwe kama Tevez na WestHam United. FA haikusema iachwe tu hatua za kisheria zimefuatwa.

mnajadili issue gani kama haya madogo yenye kujenga misingi ya ukweli mnataka tusiyaseme? hatuwezi kuwa na kiongozi mnafiki tukafanikiwa.
 
Mimi nilihisi ni kwa sababu ya muungano hasa kwa sababu niliwahi kusikiliza tapes zake miaka ya 90's na kwenye hizo tapes alikuwa akigusia muungano tu na jazba inakuja...nikahasi Muungano ndio unamkereketa zaidi.[/QUOTE]
Jasusi.

Asikuchezee akili yako. mtu timamu utasikiliza tapes zote za Mtikila na kujua aligusia muungano tu kama sio mtu wako wa karibu unayefanya naye kazi na kuratibu mambo yake? nakupa home work kama niliyompa Mkandara kwanini tuandikie mate na wino upo, Mtafute Mtikila mpe jina la katibu wa Jumuiya -UK muulize anamjua vipi utapata jibu.

Yebo Yebo.
utadanganya kwingine hapa tutakung'amua tu.tunasubiri sherehe ya Mwalimu ulikuwa wapi miaka yote iwe leo? kwanini sio jana iwe leo?
 
Back
Top Bottom