Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

Mtikila ashinda tena kesi ya mgombea huru; Afungua upya Mahakama ya Afrika Mashariki

Mpendakwao.

Uchawi utakuwa nao wewe na Yebo yebo. kitendo cha yeye na Mtikila kugawa pipi wakati mwalimu Nyerere amefariki kwa tafsiri ya haraka ni uchawi.

mie sina personal issues tizama hiyo thread hapo juu inasema MSOLLA ANAISHI NCHI GANI? na aliyeanzisha kaomba namba za nyumbani na cellphone za Msolla na Mama Katunzi. jeee huoni hizo ni personal issue? sijaona comment zako kumwambia mwanakijiji hii ni personal issue kutaka namba za nyumbani za watu.

kuna thread ' Ngano YA BAKHRESSA" imeanzishwa na shy kama wewe unajifanya kudai personal issue ungemuuliza shy kuwa ngano ni ya bakhersa sisi wana JF inatuhusu nini? au msemo wako wa kusema mind ur own business ungemwambia ili amwache Bakhressa na Business zake.

Kuna thread ya hussein Abdallah "DR.MZINDAKAYA ANA PHD YA NINI NA TOKA CHUO GANI?" hilo nalo ni person issue imekuwaje alilete humu? na PHD ya Mzindakaya inatuhusu nini,

Mpendakwao ungeanza kuhoji huko kabla ya kuja kunihoji mimi kama ni mkweli.

kuna peter Kalleghe ashindwa kupandisha website Ikulu na Dr.WHO. na Lunyungu akaleta thread "JK UMEAMUA KUMUOKOA MTU WAKO ALLAN MENGI" ambayo nayo ni too personal bwana mpendakwao hujahoji?.

Chinga akaleta habari "kuwa Mbowe anafanyiwa mitihani" sikusikia Mpendakwao ukisema au kumsaidia mheshimiwa Mbowe kuwa hii issue ni person na haitusaidii wananchi.

Mnafiki Mpendakwao kuna thread ya Fd inasema "MZUMBE UNIVERSITY MALECTURERS WAO WANA PHD FEKI" AKAMTAJA DR.WARIOBA KUWA ANA PHD FEKI. kama ni mkweli Mpendakwao ungemwambia Fikiraduni kuwa ni wivu tu mwenzenu kapata phd bila kukaa darasani.

Na kuna wanabodi wengi wanawasakama DR.Nchimbi. Kamala,DR.Mathayo. NAGU na Mahanga kuwa wana phd feki. ilikuwa mpendakwao uwakemehe hao watu kwa kuwaambia waaache WIVU NA UCHAWI, bahati ya wenzao wasiilalie milango wazi waache tu ni personal issues. kwani Nchimbi na wenzake si medical doctors tukawa na hofu kuwa phd zao zinaweza kupelekea kuua watu. au Phd zao si za urubani tukahofu wanaweza kuua watu tukiwapa ndege waendeshe na pia si waalimu tukawa na wasi wasi wataambukiza ujinga.

phd zao ni personal issues kwetu. lakini Mnafiki Mpendakwao hujajibu wala kuchangia kwa kusema kama unavyoniambia mimi.

nakubali niMIND MY BUSINESS lakini jumuiya si mali yenu.lazima tuseme kuwa Yebo yebo ni bomu. lazima tuseme kama ana kadi mbili nakubaliana na usemi wako U can fool some people sometime but u can't all the times. hili ndilo alilolipata Yebo yebo amejaribu kuwa fool watu kwa kuitumia jumuiya kwa ajili ya family yake au kuwa mwanachama wa vyama viwili na hawezi kum fool Balozi all the times kuwa MISS-Tanzania ni kitu kinacholeta watalii Tanzania. amemfool this time not next times.
Mwisho.
wewe si senior Members humu na si regular contributor kama Mwanasiasa. Mwanakijiji au ES na wengine wengi tu ambao ningewasikiliza.

sikusikilizi nakuona mjinga tu huna tofauti na Yebo yebo ungesema nimuache Yebo yebo kwani weeks hizi yuko busy na shopping za Mamiss hapo ningekulewa ila mkileta kelele tupo hatuja lala. mpe ushauri wangu YEBO YEBO kuwa lips stick za Mamiss zinapatikana kwenye maduka pale Oxford street.

Yebo Yebo.

Kutokana na ushauri wa mheshimiwa Nungwi nakuachia upumzike najua uko busy ila ukileta kujua na kuwadanganya watu ujue tuko macho wewe nyamaza tu na uwe na heshima. hapo utapata heshima na kumdhihaki baba wa taifa uache.
Ushauri wangu kwa
 
Wazee Wangu,

Heshima mbele, lakini mimi binafsi ninawaomba kwamba enough, mmesema ya kutosha tumewasikia, sasa imegeuka sio kukata ishu tena maana haya maneno mnayorushiana kwa nini msitumie pm, maana sisi wengine hatuelewi kabisa the beef, lakini inaonekana kuna some ishus huko London, mnahitaji kuziweka sawa huko huko wenyewe kwa wenyewe,

I mean tufikie mahali tuwafikirie na wengine kwenye hii forum, tumejaribu kufuatilia huu mjadala, lakini hatuelewi the problem, with all due respect na ushauri wa bure tu wazee heshima mbele, lakini imetosha,

Tumewasikia wazeee, sasa turudi kwenye ishu!
 
Jumatatu imewadia lakini kabla hatujaendelea ni bora tukakumbushana yaliyojiri JUMAMOSI ambako BALOZI pamoja na JUMUIYA YA ABUU FARAJI na LEO NYADUNGA ilijumuika kwenye HARUSI huko READING

Mijipicha ndo hii hapa
img_8089.jpg

huyu naye bora alivyoacha UKAPERA kwani it was too much

img_7915.jpg

HIVI HUYO MWENYE SUTI NYUMA YA BWANA HARUSI ANA FANANA NA NANI VILE?????

img_7917.jpg

ABUU FARAJI lazima atakuwa anataka DILI kwa huyu jamaa MBONA juzi hatukumuona kwenye HARUSI ya MTANZANIA MWENYE ASILI YA PEMBA hapo ILFORD au mambo ya kubaguana?
 
img_8111.jpg

as usual, ABUU is all over the place na hata picha tena sikuhizi hapigi, kazi hiyo kaachiwa Pinto...mambo ya specializations and division of labour..nimekubali Mangi
 
naomba katiba mpya utungwe haraka ili 2015 pachimbike.hivi vyama naona vinatutania.miaka 50 bado wanafunzi wanakaa chini chini ya mti!.wazungu,wahindi na warabu ndiyo watanzania wazawa.kwa sababu maisha wanayo ishi nchini mwetu ndo tulipaswa kuishi sisi.siyo kwamba wanaishi tu bali wanachuma na kupeleka kwao hata kile Mungu alichotujalia(madini) huku police ikiwapa ulinzi.hadi wanadiliki kujenga viwanja mbugani(loliondo) na kwenye machimbo ya madini.Tz yangu nakupenda.
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, akitaka kusikilizwa na kutolewa uamuzi wa kesi ya mgombea binafsi. Katika kesi iliyofunguliwa Juni 10 mwaka huu, Mtikila atatetewa na jopo la wanasheria watano wa kimataifa, wakiwamo wanasheria waandamizi wa Umoja wa Mataifa. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mtikila aliwataja wanasheria hao kuwa ni Profesa Setondji Adjovi na Thompson wa Shirika la Etudes Vihode la Benin, Profesa Charles Adeogun wa Shirika la Charles Anthony LLP la Nigeria na Francis Dako wa Benin huku wakisaidiwa na Birdi Njau.

“Wiki ijayo ndio itatolewa tarehe ya lini kesi hii itaanza kusikilizwa,”alisema Mtikila. Hatua ya Mtikila kufungua tena kesi hiyo inakuja takribani mwaka mmoja tangu jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufaa, kutoa hukumu iliyokubali rufaa ya Serikali iliyopinga ruhusa ya kuwapo kwa mgombea binafsi nchini.

Juni 17, 2010, majaji saba wa Mahakama ya Rufani wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhani, walitengua hukumu ya kuruhusu mgombea binafsi iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wakisema, suala hilo litaamuliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtikila ambaye aliyeenguliwa kugombea Urais katika uchaguzi Mkuu 2010 kutokana na kutotimiza masharti ya kuwa na wadhamini 10, alisema katika kesi hiyo ya msingi, anapinga vipengele vya Ibara 39, 67 na 77 vya Katiba ya Tanzania na mabadiliko ya mwaka 1992 na Desemba 1994.

“Mabadiliko haya yalibatilisha Haki ya Ibara ya 21(2) ya Katiba ya nchi, ya kila raia wa nchi yetu kugombea Urais, Ubunge na Udiwani bila kulazimishwa kujiunga na chama cha siasa iliyokuwa imetolewa na Mahakama Kuu, Oktoba 1994,” alisema Mtikila. Alisema madai mengine ya msingi katika kesi hiyo ni kulinda haki ya msingi ya binadamu ya uhuru wa kujumuika na kuirudishia mahakama uhuru wake na nguvu ya kisheria ya kukosoa makosa ya Bunge na dola.

Mtikila amefungua kesi hiyo wakati tayari Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wameishtaki Serikali ya Tanzania katika Mahakama hiyo iliyopo mkoani Arusha, wakidai kusikilizwa na kutoa uwamuzi wa suala la mgombea binafsi. TLS na LHRC walidai kuwa suala la kuwapo mgombea binafsi ambalo liliwahi kuzua mjadala na gumzo nchini, ni haki ya msingi ya kikatiba.

Oktoba 24 mwaka 1994, Mwenyekiti wa Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila alishinda kesi dhidi ya Serikali katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ambayo iliruhusu kuwapo kwa wagombea binafsi. Hata hivyo, baada ya kushinda, Serikali ilifanya marekebisho ya Katiba, badala ya kukata rufaa, ili mgombea binafsi asiwepo nchini. Mei 5, 2006 jopo la Majaji watatu wa Mahakama Kuu, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo, lilitoa hukumu nyingine iliyompa ushindi Mtikila kwa kukubali kuwapo kwa wagombea binafsi, uamuzi ambao Serikali iliupinga kwa kukata rufaa.

Mwananchi
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Democratic (DP),
Mchungaji Christopher Mtikila amefungua
kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania katika
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu,
akitaka kusikilizwa na kutolewa uamuzi wa
kesi ya mgombea binafsi.
Katika kesi iliyofunguliwa Juni 10 mwaka
huu, Mtikila atatetewa na jopo la wanasheria
watano wa kimataifa, wakiwamo
wanasheria waandamizi wa Umoja wa
Mataifa. Akizungumza na waandishi wa
habari jana, Mtikila aliwataja wanasheria
hao kuwa ni Profesa Setondji Adjovi na
Thompson wa Shirika la Etudes Vihode la
Benin, Profesa Charles Adeogun wa Shirika
la Charles Anthony LLP la Nigeria na Francis
Dako wa Benin huku wakisaidiwa na Birdi
Njau.
“Wiki ijayo ndio itatolewa tarehe ya lini kesi
hii itaanza kusikilizwa,”alisema Mtikila.
Hatua ya Mtikila kufungua tena kesi hiyo
inakuja takribani mwaka mmoja tangu jopo
la majaji saba wa Mahakama ya Rufaa, kutoa
hukumu iliyokubali rufaa ya Serikali
iliyopinga ruhusa ya kuwapo kwa mgombea
binafsi nchini.
Juni 17, 2010, majaji saba wa Mahakama ya
Rufani wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu
wa Tanzania, Agustino Ramadhani,
walitengua hukumu ya kuruhusu mgombea
binafsi iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda
ya Dar es Salaam wakisema, suala hilo
litaamuliwa na Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Mtikila ambaye aliyeenguliwa kugombea
Urais katika uchaguzi Mkuu 2010 kutokana
na kutotimiza masharti ya kuwa na
wadhamini 10, alisema katika kesi hiyo ya
msingi, anapinga vipengele vya Ibara 39, 67
na 77 vya Katiba ya Tanzania na mabadiliko
ya mwaka 1992 na Desemba 1994.
“Mabadiliko haya yalibatilisha Haki ya Ibara
ya 21(2) ya Katiba ya nchi, ya kila raia wa
nchi yetu kugombea Urais, Ubunge na
Udiwani bila kulazimishwa kujiunga na
chama cha siasa iliyokuwa imetolewa na
Mahakama Kuu, Oktoba 1994,” alisema
Mtikila. Alisema madai mengine ya msingi
katika kesi hiyo ni kulinda haki ya msingi ya
binadamu ya uhuru wa kujumuika na
kuirudishia mahakama uhuru wake na
nguvu ya kisheria ya kukosoa makosa ya
Bunge na dola.
Mtikila amefungua kesi hiyo wakati tayari
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS)
na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC), wameishtaki Serikali ya Tanzania
katika Mahakama hiyo iliyopo mkoani
Arusha, wakidai kusikilizwa na kutoa
uwamuzi wa suala la mgombea binafsi.
TLS na LHRC walidai kuwa suala la kuwapo
mgombea binafsi ambalo liliwahi kuzua
mjadala na gumzo nchini, ni haki ya msingi
ya kikatiba.
Historia ya mgombea binafsi
Oktoba 24 mwaka 1994, Mwenyekiti wa
Democratic Party, Mchungaji Christopher
Mtikila alishinda kesi dhidi ya Serikali katika
Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma ambayo
iliruhusu kuwapo kwa wagombea binafsi.
Hata hivyo, baada ya kushinda, Serikali
ilifanya marekebisho ya Katiba, badala ya
kukata rufaa, ili mgombea binafsi asiwepo
nchini.
Mei 5, 2006 jopo la Majaji watatu wa
Mahakama Kuu, Amir Manento, Salum
Massati na Thomas Mihayo, lilitoa hukumu
nyingine iliyompa ushindi Mtikila kwa
kukubali kuwapo kwa wagombea binafsi,
uamuzi ambao Serikali iliupinga kwa kukata
rufaa.

Sorcez: Mwananchi
 
Na Muhibu Said
Mwenyekiti wa DP, Christopher Mtikila, amefungua kesi katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu akiendelea kudai kuwapo mgombea binafsi katika uongozi wa kisiasa nchini.
Kesi hiyo namba 011 ya mwaka 2011, imefunguliwa na Mtikila dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mahakama hiyo mjini Arusha, Juni 10, mwaka huu.
Mtikila anawakilishwa na jopo la wanasheria waandamizi sita wa kimataifa kutoka Benin na Nigeria.
Mtikila anaiomba mahakama hiyo, kubatilisha hukumu ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyotengua uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambayo iliamua katika kesi iliyofunguliwa naye (Mtikila) kuwa sheria inayozuia mgombea binafsi inakiuka katiba ya nchi.
Alisema uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ndio pekee unaolinda haki za msingi za raia wa nchi zote pamoja na haki ya msingi ya binadamu ya kutolazimishwa kujiunga na chama chochote cha siasa.
Hukumu hiyo ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, ilitolewa na jopo la majaji saba walioongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, Juni 16, mwaka jana. Wengine waliounda jopo hilo la majaji saba, ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri.
Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo, walibatilisha sheria hiyo inayozuia mgombea binafsi katika hukumu yao ya Mei 5, 2006 na kuipa serikali miezi sita kuweka kifungu kinachoruhusu kuwepo kwa mgombea wa aina hiyo. Hata hivyo, serikali ilikata rufaa.



CHANZO: NIPASHE
 
Ameweka wanasheria 7 ama 6 mmoja toaka nigeria wengine toka benini. Source bbc radio jioni hii
 
Kilicho nichekesha ni hao wanasheria wake nadhani ni saba ama sita, wote wanatoka west africa mmoja nigeria. Anadai serikali ya tanzania imenyima haki raia wake kugombea pasipo kuwa wanachama.
 
Serikali za ccm 'zinazofuata utawala wa sheria' zimeshindwa nini kutii hukumu halali ya mahakama???
 
Warema alipopigiwa simu anadai hana lakusema anasubiri waitwe ayaone mashitaka...

Mtikila kanifurahisha sana... Anasema kesi yake ya mwaka 1994 alishinda serikali ikakata rufaa wakamlete mizengwe hata kesi haikuisha ikatupiliwa mbali!
 
Ameweka wanasheria 7 ama 6 mmoja toaka nigeria wengine toka benini. Source bbc radio jioni hii

Shapu,
Naomba nikusahihishe kidogo. Mtikila hana locus wala uwezo wa kufungua kesi katika mahamama ya Afrika. Kesi imefunguliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Legal and Human Rights Centre.

Nakuambatanishia hapa hati ya madai ili uweze kuisoma na kuielewa.
 

Attachments

Mbona hawaishtaki Serikali kuhusu mahuaji ya Nyamongo au kunamtu wanamuandaa kuwa mgombea Binafsi!?
 
Shapu,Naomba nikusahihishe kidogo. Mtikila hana locus wala uwezo wa kufungua kesi katika mahamama ya Afrika. Kesi imefunguliwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Legal and Human Rights Centre. Nakuambatanishia hapa hati ya madai ili uweze kuisoma na kuielewa.
Caren, nashukuru kwa ufafanuzi, mm sio mtaalamu wa sheria ila nimeleta nilichosikia toka bbc wao walisema ni mtikila. Anyway lkn la msingi ni kuwepo kwa kesi. Nashukuru umeweka details zaidi.
 
ghghbghvfvftrrrrrhhjgggttffffffdggdffrdrysddddcddddhddddhffdfddhddhfhfddffffvffhffhffjffhfftfvcvcffvfg
 
Back
Top Bottom