habari hii nimeisoma sijaimaliza maana machozi yamenitoka, sisi nyumbani kwa kweli tulikuwa tumejaliwa maana kilimo cha kahawa kilitutoa sana kabla ya CCM na Vibaraka wake kuua KCU, tulikuwa na wapagazi wawili, moja ni mtusi, mmoja mnyarwanda, wote walikuwa wanaongea lugha zinafanana hata sisi warijaribu kutufundisha. Nyarwandwa alikuwa anatuchungia ng'ombe wetu, Mrundi alikuwa akilima magugu maji (Rumbungu) na kupalilia. Wakati vita imepamba moto nyarwanda alimuua mwenzie na kukimbilia rwanda, tukaajiri wengine, nao vita ilivyopamba moto waliiba ngombe wetu 30 na kutokomea wakatuachia umaskini, tulianza kusoma kwa shida sana kwani kahawa zilikosa mbolea na kufa, angalau ulikuwa ukikosa karo baba anakuambia tafta soko la ng'ombe wawili uuze. Wdogo wangu wengi waliishia form 2 kwa sababu ya umaskini. watu hawa huwa sitaki kuwasikia kabisa walitutia umaskini sana. Mtikila ongeza juhuzi tukomeshe hawa ngedele.