Namnukuu marehemu mtikila........
1. Kagame amemwaga kinyama sana damu ya mamilioni ya Wahutu, ambao bado anaendelea kuwaua usiku na mchana, kuliko Adolf Hitler alivyowaua Wayahudi.
2. Kagame anaendesha mauaji dunia nzima, kwa kutumia kikosi chake maalum cha Escadron de la mort, ambacho ndicho alichotumia hata kumwangamiza Bingwa wetu wa Sheria, Hayati Profesa Jwani Mwaikusa, kwa kosa la kuweka wazi katika ICTR kwamba mtuhumiwa mkuu wa genocide katika Maziwa Makuu ni dikteta Paul Kagame. Kagame alihofia kwamba kutokana na majumuisho ya mwisho ya Mwanasheria huyo, lazima Ulimwengu ungelazimisha kukamatwa kwake na kufikishwa mbele ya Sheria.
3. Kagame akiwa na cheo cha Meja alikuwa mstari wa mbele kumwua Rais Thomas Sankara wa Burkina Faso, kule Uagadougou.
4. Kagame alikuwa Burundi kwa ushirikiano wake muhimu na Jean Bikomagu, katika mauaji ya kikatili sana ya marehemu Rais Melchior Ndadaye.
5. Kagame ndiye aliyehusika kikamilifu na utunguaji wa ndege iliyomchukua Rais Juvenal Habyarimana wa Rwanda pamoja na Rais Cyprien Ntaryamira wa Burundi.
6. Kagame analaaniwa na dunia nzima kwa kumfanyia unyama wa kutisha mwanasiasa mwanamke, shujaa Victoire Ingabire, ambaye amemtupa gerezani kwa kosa la kugombea Urais wa Rwanda akiwa Mhutu, na kosa la kuwa na kibali kwa wananchi wa Rwanda kuliko yeye aliyeloa damu ya mamilioni ya binadamu aliowaua kinyama.
7. Kagame amemwaga majasusi zaidi ya 1,000 katika Nchi yetu, wanaotumia ufisadi wa mapesa, ngono n.k katika kutengeneza mazingira ya kutekwa utawala wa nchi yetu na Watusi na hatimaye nchi yetu kuwa mkoa wa Himaya yao. Kama ilivyoelezwa juu, maelfu yao wamefanikiwa kujipenyeza katika taasisi zote nyeti za dola ya Nchi yetu. Walipoishika Uhamiaji waliitumia kujipa uraia na kukamata nafasi nyeti na ardhi yetu pia.
8. Maelfu ya majasusi wa Kagame wanajifanya wanashughulikia mizigo ya Rwanda na Uganda, wengine wanajifanya wafanyabiashara au wanatafuta kuwekeza, wengine wanajifanya wanafunzi. Lakini ukweli ni kwamba Taifa letu liko uchi kwa Kagame, kwa sababu kila tunachokifanya katika Nchi yetu kinaripotiwa Rwanda masaa 24. Katika Jiji la Dar es Salaam, Mikocheni ndiko walikojaa Wanyarwanda hao kama kwao.