Mtindo mpya wa trafiki kula rushwa (picha)

Kinacho sikitisha zaidi yale mabwanyenye ya kwenye ile taasisi yakuzuia mlungula yame jazana ofisi yakisubiri yapelekewe taarifa kama hizi, huku yakiwa ubunifu na weledi wa kupambana na mlungula....
Hawajapata taarifa za kiitelejensia.
 
mbona hii ni mbinu ya zamani sana
 
Huu Ni uchawi wa kishamba Sana..Ni vyema ukakomaa na akina flani wanaosemekana Kuiba billion 180 baada ya mzee kufariki..kuliko huu uchawi wako
 
Acha wapunguze vifurushi tu maana si kwa kuwaumbua huku.....

Teknolojia noma sana
 
Aisee kuna limama limenikamata wiki iliyopita,kweli leseni yangu ilikuwa imeisha na mimi nilikuwa sijaiangalia, hilo kosa nikiri ni uzembe wangu, tatizo hakuwa na zile mashine zao,aliandika kwenye kidaftari akaniambia nipitie risiti kesho yake, jioni naangalia kwenye tms nakuta kaniandikia fine mbili,la leseni na mkanda😰. ..yaani babu yangu angekuwa mchawi lile limama jeusi linene lingenikoma!!!!
 
Bora ukutane na Mzee ama jamaa lakini sio hawa wamama... Ni wagumu sana.. huchomoi
 
Mbona makonda huwa wanashuka wanawafuata hao trafiki moja kwa moja kutoa ya kubrashia, na wakishatoka huko wanamruhusu dereva aondoe gari? au na hii ni mpya...
 
Pale bucha kuna mmoja anakuambia kabisa .
Namnukuu:fungua hela yako tena iwe mpya kabisa na iww hela halili kwa malipo ya mtanzania,isiifichefiche unaficha kwani sio halili hiyo?
 
Bora kutoa 1500 kuliko 30k..acha umbea mkuu.
 
Rushwa Rushwa Rushwa Rushwa Rushwa .... Vipi niendelee au ..
 
jamani mbona mnapenda sana kuwa nanga hao polisi...kwa inavyo jua mimi polisi huwezi kumpa rushwa kama wewe gari yako ni safi...ila kama gari yako ina umagumashi magumashi ndio mnaanza kujikomba kwao na virushwa vyenu visivyo maana....

ila kwakweli hakuna mtanzania msafi, wote kwenye nafasi zenu mnakula rushwa ambayo haielezeki.
 
Lisemwalo lipo. TAKUKURU kama kweli wanafanya kazi basi watafanyia kazi hii na kuleta mrejesho.
 
Tulishauri kuwe na checkpoint maalumu na hizo checkpoint ziwe na camera, hakuna mtu kuongea na askari hao mbali na ofisi ya checkpoint
 
Mi naona mapichapicha tu, huyo kondakta aliyeshuka na hela yuko wapi? mijitu mingine mna roho mbaya hata pa kuanzia hamjui!! we kwako ni msafi sana? waacheni wapate ya kiwi
Hizi mambo za kutetea uovu sio sawa kabisa, kila mtu afanye uovu kwenye nafasi yake. sijui utakuwa na hali gani huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…