Mtindo mpya wa trafiki kula rushwa (picha)

Mtindo mpya wa trafiki kula rushwa (picha)

pichani ni kaka mtanashati anayejifanya muuza magazeti, hapa ni mataa ya moroko kinondoni daladala zinazotoka maeneo ya shoppers yanasimamishwa na Askari kisha kondakta ana shuka na kumalizana na na huyo kaka muuza magazeti mheshiwa alisema watoa taarifa tutalindwa hivyo sitegemei vitisho wala uzi huu kufutwa picha ya kwanza amenyoosha mkono juu kupeana ishara na Askari ambao wako upande wa mpiga picha, picha ya pili anapanga fedha alizoweka katikati ya gazeti

View attachment 1742159

View attachment 1742160

View attachment 1742161

View attachment 1742162
Astagafilulahi
 
Hukuna ushahidi kwenye maelezo yako...

Ni roho mbaya tu...
 
Acha ushamba basi halafu akishikwa akikosa kazi watoto wale nn ? Ndo furaha yako ?


Una roho ya kichawi sana mtoa mada

Fackeni
 
Pesa huwekwa kwenye leseni.
Mara nyungu huweka 2000 au 1000.
Traffic hujifanya kukagua leseni kumbe anachukua hela
 
Mimi nadhani tuanze kuwaambia wenye magari waweke magari yao vzr ili wasiwashawishi vijana weir.
Wakiamua kuwaandikia kwa kila kosa wanalolikuta haitapendeza sana. Acha wivu
 
Pichani ni kaka mtanashati anayejifanya muuza magazeti, hapa ni mataa ya Morocco (Kinondoni) daladala zinazotoka maeneo ya Shoppers/Kawe/Msasani zinasimamishwa na Askari kisha kondakta anashuka na kumalizana na na huyo kaka muuza magazeti.

Mheshimiwa alisema watoa taarifa tutalindwa hivyo sitegemei vitisho wala uzi huu kufutwa. Picha ya kwanza amenyoosha mkono juu kupeana ishara na Askari ambao wako upande wa mpiga picha. Picha ya pili anapanga fedha alizoweka katikati ya gazeti

View attachment 1742159

View attachment 1742160

View attachment 1742161

View attachment 1742162

Hii njia ya kutoka kibaha mpaka mbezi hawana shida hata ya kuweka muuza gazeti wanachukua na ndio utaratibu kila gari ya abiria bajaji na zinazobeba mchanga lazima isimame iache hela iondoke
 
Probably unachosema ni kweli. Ila huyu jamaa akiamua kukushtaki na kudai fidia kwa kumdhalilisha na kumzushia uongo kwenye mitandao (defamation) anashinda asubuhi na mapema. Maana akisema yeye ni kweli hapo anauza magazeti na si kupokea rushwa utakataa vipi? Hapo kuna ushahidi gani sasa kuwa anapokea rushwa kwa niaba ya trafiki?
 
Kinacho sikitisha zaidi yale mabwanyenye ya kwenye ile taasisi yakuzuia mlungula yame jazana ofisi yakisubiri yapelekewe taarifa kama hizi, huku yakiwa ubunifu na weledi wa kupambana na mlungula....
Kati ya Taasisi ya Hovyo ni Toakuku, yan huwa sielew utendaj kaz wao! Wanasubir uzinguane na chanel zao au na mwana siasa ndo watumike kukusumbua.
Ila rushwa kwa trafik barabaran ipo nje kabisa kila abiria ruksa kushuhudia.

Ukija mahakaman rushwa nje kabisa, wale makalan ukifika tu anakuangalia jicho la kwamba jiongeze, yan uingie viunga vya mahakama uondoke bila kuchomoa rushwa basi itakiwa sio Tanzania hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Takukuru nchi hii ingefutwa haifanyi kazi vizuri INA double standard. Rushwa kwa matrafik inaombwa na kuchukuliwa ni utaratibu na hiki kikundi cha kuzuia na kupambana na rushwa kikiwepo wakijipatia mishahara minono pamoja na marupurupu bila kuwajibika ipasavyo.Nchi yetu inamambo mengi tufute taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa huku barabarani jeshi wakae kuchek usalama tutaokoa pesa nyingi zinazopotea.
 
Polisi wamembuni bwinu, kumradhi..
wamebwinu mbuni
wamembwinu buni

Aahhhh!!!
 
Pichani ni kaka mtanashati anayejifanya muuza magazeti, hapa ni mataa ya Morocco (Kinondoni) daladala zinazotoka maeneo ya Shoppers/Kawe/Msasani zinasimamishwa na Askari kisha kondakta anashuka na kumalizana na na huyo kaka muuza magazeti.

Mheshimiwa alisema watoa taarifa tutalindwa hivyo sitegemei vitisho wala uzi huu kufutwa. Picha ya kwanza amenyoosha mkono juu kupeana ishara na Askari ambao wako upande wa mpiga picha. Picha ya pili anapanga fedha alizoweka katikati ya gazeti

View attachment 1742159

View attachment 1742160

View attachment 1742161

View attachment 1742162
Wacha wale rushwa tu,maana serikali haiwapandishi madaraja.Haiwalipi maxeni yao.Sasa suluhisho ni kutengeneza mazingira ya kujilipa tu
 
Njoo njia ya Mbezi - Goba asubuhi ushuhudie jinsi wanavyozikusanya shs 1500/- kwa kila daladala. Kuna sehemu pana msikiti wanapaita kwa Ulomi. Yaani mpaka raha. Daladala inapigwa mkono, konda anashuka fasta kashika buku abiria mnaona, kisha anarudi fasta. KAMA UNATAKA KUONA KONDAKTA ANASALIMIANA KWA VIGANJA NA TRAFIKI NJOO HUKU. HAWAOGOPI UVIKO-19
Hapo kwa ulomi pakihuni Sana wako Police Wana vaaa kombati gari lazima zisimame
 
Hawa wa sinza hapa junction ya mawasiliano ni balaa sana
 
Tupo bize kuokoa mabilioni ya b o t na wahujumu uchumi!Hatutaki umbea wenu wa buku buku. Ova,
 
Hii mbinu ni ya kitambo; Wanatumiwa hadi wauzaa biskuti, juice, na karanga.
 
dah mm mwenyewe nikajua mweka thread ni muongo but nmrpita hlo eneo leo ni kweli
 
Back
Top Bottom