Mtindo wa uwekezaji wa Waarabu ndio kama tunavyoona Loliondo

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Awamu hii ya mama tunaona juhudi kubwa kuvutia uwekezaji kutoka nchi tajiri za Mashariki ya Kati. Wakati tunahangaika kuvutia Waarabu kuwekeza inafaa kuelewa desturi yao wakiwekeza kwako.

Wao kwa maoni yangu wakiwekeza nchini kwako hawatofautishi na kununua sehemu waliyowekeza. Pia huwa wanaendesha mambo kwa desturi ya mila na dini yao badala ya kufuata sheria na kanuni za nchi mwenyeji. Tumeona mifano jinsi hawajali haki kwenye ajira kwa wale waliyowahi kufanya kazi huko kwao.

Huwa wafanyakazi wasiyokuwa wenzao hasa Waafrika wanawaona kama watumwa tu. Mfano wa uwekezaji wa UAE ni Loliondo. Tumeona jinsi kitalu cha kampuni ya UAE kimegeuzwa kama sehemu ya nchi hiyo.

Kitalu wala huwa hakiingizwi kwenye kushindaniwa, kimekuwa chao kama kile kituo cha Wamarekani cha Guantanamo kule Cuba. Midege inashuka huko kila wakati bila wananchi kuelewa nini kinaendelea. Kwa kuwa hakuna uwazi, kuna shaka mambo hayafanyiki kwa mujibu wa sheria.

Kwa hivyo tunapoendelea kuvutia uwekezaji toka nchi za Kiarabu kuna mashaka ile concept ya faida 50/50 ikawekwa pembeni na nchi kugeuzwa shamba la bibi.

Watanzania tuko macho na aina ya wawekezaji wanaoletwa awamu ya sita.
 
Awamu hii ya mama tunaona juhufi kubwa kuvutia uwekezaji kutoka nchi tajiri za mashariki ya kati. Wakati tunahangaika kuvutia waarabu kuwekeza inafaa kuelewa desturi yao wakiwekeza kwako.
Wao kwa maoni yangu wakiwekeza nchini kwako hawatofautishi na kununua sehemu waliyowekeza. Pia hua wanaendesha mambo kwa desturi ya mila na dini yao badala ya kufuata sheria na kanuni za nchi mwenyeji. Tumeona mifano jinsi hawajali haki kwenye ajira kwa wale waliyowahi kufanya kazi huko kwao. Hua wafanyakazi wasiyokua wenzao hasa waafrika wanawaona kama watumwa tu.
Mfano wa uwekezaji wa UAE ni loliondo. Tumeona jinsi kitalu cha kampuni ya UAE kimegeuzwa kama sehemu ya nchi hiyo. Kitalu wala hua hakiingizwi kwenye kushindaniwa kimekua chao kama kile kituo cha wamarekanicha guantanamo kule cuba. Midege inashuka huko kila wakati bila wananchi kuelewa nini kinaendelea. Kwa kua hakuna uwazi kuna shaka mambo hayafanyiki kwa mujibu wa sheria.
Kwa hivyo tunapoendelea kuvutia uwekezaji toka nchi za kiarabu kuna mashaka ile concept ya faida 50 / 50 ikawekwa pembeni na nchi kugeuzwa shamba la bibi.
Watanzania tukoe macho na sina ya wawekezaji.
Bila picha ni uzushi

USSR
 
Yajayo.........Yana......
1677271000931.jpg

1677271010492.jpg
 
Zanzibar hawana wanyama pori ndio maana marais wa Muungano toka Zanzibar huwa hawana uchungu kabisa na wanyama wetu.
Tangu ujiunge JF leo umeongea jambo la maana sana.
 
Hawa Watu hawajawahi endeleza Nchi Yoyote Zaidi ya kuinyonya.Waarabu ni wafanya biashara na wanafocus kwenye faida tuuu..Tafuta Msaada wa Maana ambao wamewahi toa Zaidi ya Maslahi Yao binafsi.
 
Mpaka huyu mama akitoka, waaeabu watabaki nyakanyaka.......si kwa kusakamwa huku!!

Anyway, ngoja tuwakumbatie makaburu na wazungu waliojaa utu........kwi kwi kwi kwiiii
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Kwa hivyo tunapoendelea kuvutia uwekezaji toka nchi za Kiarabu kuna mashaka ile concept ya faida 50/50 ikawekwa pembeni na nchi kugeuzwa shamba la bibi.

Watanzania tuko macho na aina ya wawekezaji wanaoletwa awamu ya sita.
Hivi ni kweli Watanzania tuko makini? Kama tungekuwa makini kweli hivi ndio vitu tungekuwa tunajadili. (Maslahi ya Taifa).
 
Awamu hii ya mama tunaona juhudi kubwa kuvutia uwekezaji kutoka nchi tajiri za Mashariki ya Kati. Wakati tunahangaika kuvutia Waarabu kuwekeza inafaa kuelewa desturi yao wakiwekeza kwako.

Wao kwa maoni yangu wakiwekeza nchini kwako hawatofautishi na kununua sehemu waliyowekeza. Pia huwa wanaendesha mambo kwa desturi ya mila na dini yao badala ya kufuata sheria na kanuni za nchi mwenyeji. Tumeona mifano jinsi hawajali haki kwenye ajira kwa wale waliyowahi kufanya kazi huko kwao.

Huwa wafanyakazi wasiyokuwa wenzao hasa Waafrika wanawaona kama watumwa tu. Mfano wa uwekezaji wa UAE ni Loliondo. Tumeona jinsi kitalu cha kampuni ya UAE kimegeuzwa kama sehemu ya nchi hiyo.

Kitalu wala huwa hakiingizwi kwenye kushindaniwa, kimekuwa chao kama kile kituo cha Wamarekani cha Guantanamo kule Cuba. Midege inashuka huko kila wakati bila wananchi kuelewa nini kinaendelea. Kwa kuwa hakuna uwazi, kuna shaka mambo hayafanyiki kwa mujibu wa sheria.

Kwa hivyo tunapoendelea kuvutia uwekezaji toka nchi za Kiarabu kuna mashaka ile concept ya faida 50/50 ikawekwa pembeni na nchi kugeuzwa shamba la bibi.

Watanzania tuko macho na aina ya wawekezaji wanaoletwa awamu ya sita.
Swali
Unadhani nini matajiri wa UAE wanacho faidi Loliondo zaidi ya utalii?
Unafahamu binti Mfalme wa Saudia alinununua haki ya kutumia beach moja Ufaransa pekee yake kwa mwezi mzima seuze Loliondo, haya ni mambo ya fweza jombi.
 
Unaweza kuthibitisha kuwa Zanzibar hawana Wanyamapori.
Chogo Kakosea kudharau zenji mji mkongwe kwenye urojo wa kushiba basi msamehe ATI Ami yangu, au vipi maana ni kweli kule mfereji wa wima niliona nguchiro na digidigi, kule mchambawima nikaona komba wakinywa mnazi na hata kule nungwi kulikuwa na kanga pori na kware
 
Bila kuwasau Mbega na Tumbili Papa na Nyangumi.
 
Swali
Unadhani nini matajiri wa UAE wanacho faidi Loliondo zaidi ya utalii?
Unafahamu binti Mfalme wa Saudia alinununua haki ya kutumia beach moja Ufaransa pekee yake kwa mwezi mzima seuze Loliondo, haya ni mambo ya fweza jombi.
Hao jamaa wakati sisi tunachukua uhuru wao walikuwa masikini wa kutupwa sisi tukaanza experiment na uhuru wetu mara tuhamie China mara Urusi mpaka Nchi ikawa dimbwi la uharo na umasikini wa kutisha.

Wenzetu wakajikita kwenye kunyanyua uchumi wao kwa kutumia rasilimali zao.
 
[QUOTE="imhotep, post: 45438387, member: 105391"
Unaweza kuthibitisha kuwa Zanzibar hawana Wanyamapori.
[/QUOTE]
Zanzibar wana utalii ila hawana wanyama pori hapo tu ndio tumewashinda .

Marais wote wa jamhuri wakitoka Zanzibar wanahakikisha wanapunguza wanyama kadri wanavyoweza ili tulingane.

Tusipokuwa makini watawamaliza wote.
 
Back
Top Bottom