Mtindo wa uwekezaji wa Waarabu ndio kama tunavyoona Loliondo

Mtindo wa uwekezaji wa Waarabu ndio kama tunavyoona Loliondo

Nyerere alijitahidi sana kutuondolea kasumba iliyojengwa kichwani mwetu na Wakoloni, Kuwa afanyalo Mzungu ndio zuri na lenye manufaa kwa Mtu mweusi, lakini lifanywalo na watu wengine ni baya kwa Muafrika.

Wanyama wetu wamesambaa Ulaya, Umarekani na nchi nyingi na wamsembazwa na Mashirika ya wazungu, hatulioni hilo na wala hatulisemi. kama ni Uwindaji hakuna wauwaji wa wanyama kama Wazungu na wamarekani, lakini hatuwaoni hao.

Mashirika yanayo somba mali asili zetu ni haoyo hayo Mashirika ya Magharibi, lakini hatuyasemi bali tuna yatetea, Mila zetu na watoto wetu wanaharibiwa na haohao Wazungu lakini bado tunawashangilia. Na bado anatuita NIGGERS na BLACK MONKEY bado tunamuona yuko sahihi.

Leo Serekali za Ulaya na Umarekani wanapigania uwekezaji wa hao Waarabu na kuwabembeleza wawekeze nchini mwao. Tumeona Mashirika mengi makubwa ya Ulaya na Umarekani wakienda Uarabuni na wakiwashawishi kuingia nao ubia na hao Wamagharibi eti wana Fursa nzuri Africa, na wao ndio wanaojua ku DEAL na WaAfrika.

Tutaendelea kutumika na wenye ngozi Nyeupe huku wakitushawishi kidini kuwachukia Waarabu wenye manufaa zaidi kwetu.

Raisi wa Kenya wiki hii anaenda UAE kutafuta uekezaji wa Biashara na Mikopo. na Tusisahau juzujuzi tuu Mwigula alikwenda ABU DHABI na akapata Mkopo Bila Riba.
 
Watu wote wenye fikara za mifumo ya kitumwa na kikabaila, kwamba watawala wana haki ya kiungu ya kumiliki mali na binafamu wenzao, ni adui wakubwa ubinadamu.

Lakini hasa ni maadui wa waafrika weusi.
 
Back
Top Bottom