Mtitu: Sababu ya kuamua kuzambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuuza Steps Entertainment

Hiyo omega nini sijui niliikuta somewhr niliangalia part one tu tena nilitumia dakika 20 tu nikaimaliza mana haina hata mvuto, jitahidini kuanza na utata mwanzo wa filamu atleast kumshawishi mtu kutaman kujua nini kitafuata mfano muvi ya sarafina ilivyoanza unataman kujua sababu ya kisa kilivyoanza
 
bila shaka wasanii mnapaswa kuwa wa moja kwanza hili kupambana na huu unyonyaji.

lakini bado najiuliza kwa nini wasanii hasa we mtitu usitumie hili jina lako hili na hata wema ume comment as if ni msanii kwa nini mnajiicha wakati mnapigania haki zenu.
 
Last edited by a moderator:
MTAZAMO

daa nimesikitika Sana kusikia company ya kanumba imesambaratika kabisa na huku aliacha movie ambayo ili uza kuliko zote.

huu unyonyaji utakomeshwa vipi bila umoja? asante mtitu kwa kuchukua hatua bila shaka na wengine wata kuunga mkono.

ila please weka jina lako huna sababu ya kujificha.
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi Naomba kujua filamu mtitu aliyoigiza hata moja tuu maana mimi namfahamu kama msambazaji na siyo msanii wa filamu

Tazama.....sandra, omega, miss bongo, blind side of marriage, division of love....zipo nyingi mkuu ambazo Mtitu ameigiza
 
Kwa hiyo mtitu na yeye si msambazaji?amesambaza kazi kadhaa za kanumba na wengineo wengi, je ananua haki zote za wasanii katika filamu au kuna makubaliano tofauti?mbona hujaliweka hili wazi?

Mimi sisambazi filamu ya mtu kwa sasa....nimejiwekea malengo nitaanza kusambaza filamu za watu baada ya miaka 3....na mkataba wangu unasema kwangu unauza haki ya kusambaza tu filamu itaendelea kuwa yako.
 
William Mtitu,

Umefanya maamuzi mazuri kusimama mwenyewe kuliko kuendelea kunyonywa, umekuwa rafiki wa kanumba kama sijakosea sasa sijui utafanya nini kuhakikisha Kampuni alio iacha inapata nafuu?

Hakika kwa maelezo yako ni wazi mama kanumba ana hitaji msaada wenu.
 
Last edited by a moderator:
Big up Mtitu.
Najua utapigwa sana vita lakini utashinda. Bora kula chako kidogo kihalali kuliko kupata mafao ya muda mfupi na ukaishi kwa kudhalilika baadae.

Ungeendelea kuwepo Steps hao wanaokupiga vita wangekukejeli wakati unadhalilika uzeeni! "Tulikuwa naye lakini alichezea maisha".

Note:

Mtiririko wako wa kuandika umenifurahisha sana. Inaonyesha umakini wako hata kama mtu hajaonana na wewe ana kwa ana. Kudos
 
Kumbe mnakwendaga ikulu kujadiliana na mkulu mambo ya bongo movie?
Very cheap president.

Sasa unataka wajadili siasa kwani wao ni wanasaisa.

Mwanasoka atajadili mambo ya soka,
Mwanamziki atajadili mambo ya mziki,
vivyo hivyo na mchumi watajidili uchumi nk.!!
 

Tatizo la huyo mama....haitaji ushauri wa mtu.....kanumba mpaka kifo kinamkuta alimwacha ndugu yake anaitwa seti na namini set anaulewa mzuri tu wa mambo haya ya filamu lakini kil kitu anachojaribu kutoa(mawazo) huyu mama hataki na kila kitu kinachomuhusu kanumba mama hataki mtu yoyote akiulizie....hii ndio imepelekea kuuza kila kitu cha mwanae na hatimae kubaki omba omba.
 
Last edited by a moderator:
kumbe yale matangazo ya kupinga wizi wa kazi za wasanii....... kazi zenyewe sio za wasanii ni za steps.

kuanzia sasa hivi mbadili uwasilishaji wa hayo matangazo..

"kununua kazi fake ni kumwibia steps"
 
kumbe yale matangazo ya kupinga wizi wa kazi za wasanii....... kazi zenyewe sio za wasanii ni za steps.

kuanzia sasa hivi mbadili uwasilishaji wa hayo matangazo..

"kununua kazi fake ni kumwibia steps"


aisee hata mie katika hili nilikuwa blind,kumbe steps ni wezi kiasi hiki? asante William Mtitu kwa kutufungua macho.
 
Last edited by a moderator:

Asante kwa kusikiliza ombi langu William Mtitu.

So sad kuona kila alicho kiacha kanumba kinasambaratika na halijaisaidia family yake kabisa.

Sikutegemea kama itafika kipindi kampuni ya kanumba itakufa kwakweli,lakini si nilisikia wana andaa movie?

lakini unafikiri kwenye hili na steps wana husika?

Mimi bado naamini mama kanumba ana hitaji msaada wenu, yeye hajui chochote na sikutegemea kama atafikia kwenye hatua ya kuwa omba omba .

Kwakweli kanumba aliwekeza nguvu nyingi kwenye hii tasnia na mama yake hastahili kuwa omba omba mnatakiwa kufanya jambo.
 
Last edited by a moderator:

Sio mada iliyopo mezani. Tunaongelea issue muhimu zaidi for the future of the film industry. Personal tests zitavuruga thread.
 
Hongera kwa uamuzi wa busara, jitahidi kuwasaidia wengine ili wasinyonywe pia nawe wakati unawasaidia pata faida kwa msaada wako lakini usiwanyonye. Na mimi ni scriptwritter ninatafut pa kuanzia tusaidieni.
 
safi sana na hongera
ktk kila jambo ni lazima kuwe na mtu wa kulianzisha,umeanzisha na songa mbele,huna haja ya kuangalia nyuma tena,huwezi kufanya kazi ya kupiga ugari na kumpa mgeni huku wewe ukiendelea kulamba mwiko na kuumia kwa njaa.
Hongera kwa hilo na endeleza kile unachokiamini
kama wao wameweza iweje wewe ushindwe?
 
Kumbe mnakwendaga ikulu kujadiliana na mkulu mambo ya bongo movie?
Very cheap president.

Wasanii wangekuwa na akili, umoja na VISION ya kuiona Tanzania inakuwa na film industry, sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine...lakni wamejaa ubinafsi, ujinga na ujuaji usio na tija matokeo yake wanashindwa kuitumia nafasi vizuri...mheshimiwa akimaliza muda wake ndio utawasikia...TUNAMKUMBUKA KIKWETE.........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…